Mtembelee muuzaji wa Briggs & Stratton Aliyeidhibishwa
kwa maelezo ya marekebisho ya mwinuko wa juu.
Uendeshaji injini katika mwinuko wa chini ya mita
762 (futi 2,500) na marekebisho ya mwinuko wa juu
hayapendekezwi.
Kusafirisha
Unaposafirisha kifaa kwa gari au trela, zungusha vali ya
kufunga mafuta hadi eneo linaloonyesha ZIMA (OFF).
Usiinamishe injini au kifaa katika mkao unaosababisha
mafuta kumwagika.
Kusafisha
Kila siku au kabla ya kutumia, tazama jenereta juu,
chini na pande zote kama kuna dalili za mafuta kuvuja.
Safisha vifusi vyovyote vilivyokusanyika. Weka sehemu
inayozunguka mafla bila vifusi vyovyote.
• Tumia brashi laini ili kulegeza uchafu na oili ambayo
imekauka.
• Tumia kitambaa chenye unyevunyevu kupangusia.
ILANI Usiweke vipengee vyovyote kwenye mianaya ya
kupitisha hewa.
Hatua ya 3: Kuanzisha Jenereta Kielelezo
Ondoa vyombo vyote vya umeme vilivyounganishwa na
jenereta. Tumia maagizo yafuatayo ya kuwasha:
1. Hakikisha kifaa kiko nje kwenye eneo tambarare.
ILANI Kukosa kutumia kifaa hiki kwenye eneo
tambarare kunaweza kusababisha kifaa kuzima.
2. Zungusha vali ya mafuta (R) hadi eneo
linaloonyesha WASHA (ON) (I).
3. Songeza wenzo wa choki (P) hadi eneo
linaloonyesha CHOKI (
ILANI Kwa injini moto, hakikisha wenzo wa choki uko
katika eneo linaloonyesha ENDESHA (RUN) (
4. Zungusha na ushikilie swichi ya kuwasha (B) hadi eneo
linaloonyesha ANZA (START) ( ) mpaka jenereta
iwake. USISHIKILIE ufunguo wa katika eneo
linaloonyesha ANZA (START) ( ) kwa zaidi ya
sekunde 5. Subiri kwa angalau sekunde 30 kabla
ujaribu tena.
ILANI Ikiwa betri haina chaji, zungusha ufunguo hadi
eneo linaloonyesha ENDESHA (RUN), shika sehemu ya
kugurumisha na uvute polepole mpaka uhisi imekuwa
gumu. Kisha vuta kwa haraka mara moja pekee ili
kuwasha injini.
5. Huku injini ikiendelea kupata joto, songesha
polepole wenzo wa choki hadi eneo linaloonyesha
ENDESHA (RUN) (
ILANI Kifaa hiki kimewekwa kifaa cha kulinda
kupungua kwa oili. Ni lazima oili iwe ya kiwango sahihi
ili injini ifanye kazi. Iwapo oili ya injini itapungua kupita
kiwango kilichowekwa, swichi ya oili itazima injini. Kagua
kiwango cha oili ukitumia kifaa cha kupima oili.
ONYO! Joto/gesi za Eksozi zinaweza
kuwasha vitu, majengo au tangi la mafuta
lililoharibika zinazoweza kushika moto, na
kusababisha kifo au majeraha mabaya. Kugusana na
eneo hili la mafla kunaweza kusababisha kuchomeka na
hivyo basi kupelekea majeraha mabaya. Kuwa makini na
maonyo yaliyo kwenye jenereta. Usiguse sehemu moto
na uepuke gesi moto zinazotolewa.
).
).
).
Hatua ya 4: Kuunganisha Vinavyotumia
Umeme Kielelezo
Matumizi ya umeme ya jenereta hii, hayafai kupita uwezo
wa nguvu za umeme zilizopendekezwa, katika hali
iliyopendekezwa, kama ilivyoonyeshwa kwenye lebo ya
data ya kifaa. Punguza matumizi ya umeme unapotumia
jenereta katika hali ambazo hazijapendekezwa.
Tumia nyaya-enezi za ubora wa juu kuambatana na IEC
245-4 na nyaya za kutoa umeme za kutoa umeme wa
AC kwenye jenereta za volti 230. Kagua nyaya-enezi
kabla ya kila tumizi. Hakikisha kwamba nyaya-enezi zote
zina vipimo mwafaka na hazijaharibika. Unapotumia
nyaya-enezi chini ya 40° C, jumla ya urefu wa nyaya kwa
sehemu ya msalaba ya 1.5 mm² haifai kuzidi mita 50 au
kwa sehemu ya msalaba ya 2.5 mm² haifai kuzidi mita 80.
ONYO! Nyaya-enezi zilizozidisha kiwango cha
vitumizi zinaweza kupata joto kubwa, kupinda,
na kuchomeka na kusababisha kifo au majeraha
mabaya. Vifaa vya elektroniki, pamoja na nyaya na vizibo
vya kuunganisha, havifai kuwa na hitilafu.
ILANI Unganisha vifaa vya elektroniki ikiwa kwa eneo
1
linaloonyesha ZIMA (OFF) kisha uweke kwenye WASHA
(ON) ili kuendesha.
Plagi za Volti 230 za AC
Tumia plagi (E au F) ili kuendesha Volti 230 za AC,
msururu mmoja, 50 Hz ya vitumizi vya umeme. Plagi za
16A zinafaa kulindwa kutokana na uzito kwa kutumia swichi
za kukata umeme za kusukuma ili kuweka upya (G). Plagi
ya 32A inafaa kulindwa kutokana na uzito kwa kutumia
swichi kuu ya kukata umeme (C). Swichi kuu ya kukata
umeme ikishuka, inakata umeme kwa plagi zote.
Ulinzi wa vifaa vya umeme unategemea swichi za kukata
umeme zinazoafikiana na jenereta. Badilisha swichi
ya kukata umeme na ile yenye kadirio la sifa sawia za
utendakazi.
ONYO! Volti za jenereta zinaweza kusababisha
mshtuko wa umeme au kuchomeka kunakoweza
kusababisha kifo au majeraha mbaya. Usiguze
nyaya au plagi zilizo wazi. Usitumie jenereta yenye nyaya
za umeme ambazo zimechakaa, kuchubuka, wazi au
vinginevyo zilizoharibika. Usitumie jenereta kwenye
mvua au wakati kuna unyevunyevu. Usishike jenereta au
nyaya za umeme ukiwa umesimama ndani ya maji, ukiwa
miguu mitupu ama mikono na miguu ikiwa na maji.
Usiruhusu watu ambao hawajahitimu au watoto
kuendesha au kuhudimia jenereta. Weka watoto mahali
salama mbali na jenereta.
Hatua ya 5: Kuzima Jenereta
1. Zima na uondoe vifaa vyote vinavyotumia umeme
kutoka kwenye plagi za paneli ya jenereta. Usiwahi
zima injini huku vifaa vinavyotumia umeme vikiwa
havijaondolewa na vimewaka.
2. Acha injini iendelee kuguruma bila vifaa
vibnavyotumia umeme kwa dakika moja ili kuimarisha
hali joto la ndani ya injini na jenereta.
3. Zungusha ufunguo wa kuwasha hadi eneo
linaloonyesha ZIMA (OFF) (0).
4. Zungusha vali ya mafuta hadi eneo linaloonyesha
ZIMA (OFF) (0).
1
7