Muundo: 25V000
Pengo la Hewa
Mwanya wa Vali ya Kuingiza Hewa
Mwanya wa Vali ya Ekzosi
Nguvu ya injini utapungua kwa 3.5% kwa kila futi 1,000 (mita 300) juu ya mwinuko
wa bahari na 1% kwa kila 10° F (5.6° C) juu ya 77° F (25° C). Injini itaendesha kwa
kuridhisha katika pembe ya hadi 30°. Rejelea mwongozo wa mwendeshaji ili kufahamu
viwango salama vinavyoruhusiwa kwenye miteremko.
Sehemu za Udumishaji - Muundo: 25V000
Sehemu za Udumishaji
Chujio la Hewa la Karatasi (Kielelezo 20)
Plagi ya Spaki ya Kifaa Kisichopitisha Nishati
Kifaa cha Kutega Plagi ya Spaki
Kifaa cha kujaribu Spaki
Tunapendekeza kuwa umwone Mtoa Huduma yeyote wa Briggs & Stratton
Aliyeidhinishwa kwa udumishaji na huduma zote za injini na sehemu za injini.
Ukadiriaji wa Nishati: Ukadiriaji wa pato la nishati kwa kila modeli ya injini ya petroli
imewekwa alama kwa kuzingatia SAE (Jumuiya ya Wahandisi wa Magari) msimbo
J1940 Nishati ya Injini Ndogo & Utaratibu wa Ukadiriaji wa Toku, na umekadiriwa
kwa kuzingatia SAE J1995. Thamani ya toku inafikia 2600 RPM kwa injini hizi kwa
"rpm" iliyowekwa kwenye lebo na 3060 RPM kwa vingine vote; thamani ya nishati ya
chaja inafikia 3600 RPM. Vizingo vya mapato ya nishati vinaweza kutazamwa katika
www.BRIGGSandSTRATTON.COM. Thamani halisi ya nishati inachukuliwa kwa eneo la
injini la kutolea injini na kisafishaji wa injini iliyosakinishwa ambapo thamani ya mapato
ya injini yanakusanywa bila viambatisho hivi. Mapato halisi ya nishati ya injini yatakuwa
juu kuliko nishati ya injini na yanaathiriwa na, miongoni mwa mambo mengine, hali
iliyoko ya kuendesha na utofauti wa injini hadi nyingine. Kwa kuwa mpangilio mpana
wa bidhaa ambayo injini imewekwa, injini ya petroli inaweza kuwa na mapato ya nishati
iliyokadiriwa wakati inatumika katika kifaa fulani cha nishati. Tofauti hii inatokana na
sababu mbalimbali zikijumuisha, lakini zisizokithi kwa, vijenzi mbalimbali vua injini
(kisafishaji cha hewa, eneo la injini la kutolea moshi, pampu ya fueli n.k.), upungufu wa
utekelezaji, hali zilizoko za kuendesha (hali joto, unyevunyevu, mwinuko), na utofauti wa
injini hadi injini. Kutokana na upungufu wa utengenezaji na viwango, Briggs & Stratton
inaweza kubadilisha injini na nishati iliyokadiriwa juu kwa injini hii.
Udhamini
Hakikisho la Injini ya Briggs & Stratton
Kuanzia Januari 2019
Hakikisho lenye Kipimo
Briggs & Stratton inatoa hakikisho kwamba, wakati wa kipindi cha hakikisho
kilichobainishwa hapa chini, itafanyia ukarabati au kubadilisha, bila malipo, sehemu
yoyote ambayo ina matatizo katika nyenzo au ufanyakazi au yote mawili. Gharama
za usafirishaji bidhaa zilizowasilishwa ili kufanyiwa ukarabati au kubadilishwa chini ya
hakikisho hili ni lazima zigharimiwe na mnunuzi. Hakikisho hili linatumika na liko chini ya
vipindi vya muda na masharti yaliyoelezwa hapa chini. Ili kupata huduma ya hakikisho,
tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe kwenye ramani yetu ya
kutafuta wauzaji kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM. Ni lazima mnunuzi awasiliane
na Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa, na kisha apeleke bidhaa kwa Muuzaji Huduma
huyo Aliyeidhinishwa ili kufanyiwa ukaguzi na majaribio.
Hakuna hakikisho lingine la haraka. Hakikisho zilizoashiriwa, ikiwa ni pamoja na
lile wa uuzaji na uzima kwa ajili ya dhumuni fulani, zina kipimo cha kipindi cha
hakikisho kilichoorodheshwa hapa chini, au kwa kiasi kilichoruhusiwa na sheria.
Dhima ya uharibifu wa kimatukio au unaotokana na jambo jingine haijajumuishwa kwa
kiasi kinachoruhusiwa na sheria. Baadhi ya majimbo au nchi haziruhusu vipindi vya
hakikisho kuwekewa vipimo, na baadhi ya majimbo au nchi haziruhusu kutojumuishwa
au kipimo cha uharibifu wa kimatukio au unaotokana na jambo jingine, kwa hivyo
kipimo na kutojumuishwa huku huenda hakukuhusu wewe. Udhamini huu hupeana haki
maalum za kisheria na pia unaweza kuwa na haki zingine ambazo zinatofautiana kutoka
kwenye jimbo hadi jingine na nchi hadi nyingine
Masharti Wastani ya Udhamini
Vanguard®; Msururu wa Kibiashara
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 36
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 36
Msururu wa XR
50
.010 - .014 inchi (,25
- ,35 milimita)
.004 - .006 inchi (,10
- ,15 milimita)
.006 - .008 inchi (,15
- ,20 milimita)
Nambari ya Sehemu
84002310
597383
19576, 5402
19368
4
.
1, 2, 3
3
Masharti Wastani ya Udhamini
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 24
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 24
Injini Nyingine Zote Zenye Mkono wa Kalibu ya Chuma ya Dura-Bore™
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 24
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 12
Injini Nyingine Zote
Matumizi ya Kibinafsi - Miezi 24
Matumizi ya Kibiashara - Miezi 3
1
Haya ni masharti yetu wastani ya hakikisho, lakini mara kwa mara huenda
kukawa na vipengele vya ziada vinavyosimamiwa na hakikisho ambavyo
havikusimamiwa wakati wa uchapishaji. Ili kupata orodha ya masharti ya sasa
ya hakikisho la injini yako, nenda kwenye BRIGGSandSTRATTON.com au
uwasiliane na Muuzaji Huduma wako Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton.
2
Hakuna hakikisho kwa injini za vifaa vilivyotumiwa kutoa nishati badala ya kifaa
kinachofaa; jenereta ya akiba kwa madhumuni ya kibiashara, magari ya kubebea
mizigo yanayozidi 25 MPH, au injini zinazotumiwa katika mashindano ya mbio au
kwenye viwanja vya kibiashara au vya kukodishwa.
3
Vanguard iliyowekwa kwenye jenereta ya akiba: miezi 24 kwa matumizi ya
kibinafsi, hakuna hakikisho kwa matumizi ya kibinafsi. Msururu wa Kibiashara ulio
na tarehe ya kutengenezwa ya kabla ya Julai 2017, miezi 24 kwa matumizi ya
kibinafsi, miezi 24 kwa matumizi ya kibiashara.
4
Nchini Australia - Bidhaa zetu huja na hakikisho ambalo haziwezi kutojumuishwa
chini ya Sheria ya Mtumiaji ya Australia. Una haki ya kubadilishiwa au kurudishiwa
pesa kwa hitilafu kuu au fidia kwa uharibifu au hasara nyingine yoyote ya siku za
usoni. Pia una haki ya bidhaa kufanyiwa ukarabati au kubadilishwa endapo bidhaa
hazitakuwa za ubora unaokubaliwa na hitilafu haimaanishi kuharibika kwa njia
kubwa. Ili kupata huduma ya hakikisho, tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa
aliye karibu zaidi nawe kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye
BRIGGSandSTRATTON.COM, au kwa kupiga simu kwa nambari 1300 274 447,
au kwa kutuma barua pepe kwa salesenquiries@briggsandstratton.com.au, au
kutuma barua kwa Briggs & Stratton Australia Pty Ltd, 1 Moorebank Avenue,
Moorebank, NSW, Australia, 2170.
Kipindi cha hakikisho kinaanzia tarehe ya ununuzi wa mtumiaji wa kwanza wa rejareja
au wa kibiashara. "Matumizi ya kibinafsi" inamaanisha matumizi ya kibinafsi ya
nyumbani ya mtumiaji wa rejareja. "Matumizi ya kibiashara" inamaanisha matumizi
mengine yote, yakijumuisha matumizi kwa madhumuni ya kibiashara, ya kuzalisha
mapato au ya kukodisha. Pindi tu injini inapopitia matumizi ya kibiashara, baada ya
hapo itazingatiwa kuwa injini ya matumizi ya kibiashara kwa ajili ya hakikisho hili.
Hifadhi risiti yako ya ushahidi wa ununuzi. Ukikosa kutoa ushahidi wa tarehe
ya kwanza ya ununuzi wakati huduma ya hakikisho inapoombwa, tarehe ya
utengenezaji wa bidhaa itatumiwa kung'amua kipindi cha hakikisho. Usajili
wa bidhaa hauhitajiki ili kupata huduma ya hakikisho kwa bidhaa za Briggs &
Stratton.
Kuhusu Hakikisho Lako
Hakikisho hili lenye kipimo linasimamia tu nyenzo zinazohusiana na injini na/au
utendakazi, na sio kubadilishiwa au kurudishiwa pesa ulizonunua kifaa ambacho kina
injini husika. Udumishaji, uimarishaji, marekebisho ya mara kwa mara au kuchakaa
na kuchanika kwa kawaida hazijasimamiwa na hakikisho hili. Vile vile, hakikisho
halitumiki ikiwa injini imehitilafiwa au kubadilishwa au ikiwa nambari tambulishi ya
injini imeharibiwa ua kuondolewa. Hakikisho hili halisimamii uharibifu kwenye injini au
matatizo ya utendakazi wa injini yanayosababishwa na:
1.
Matumizi ya sehemu ambazo si sehemu halisi za Briggs & Stratton;
2.
Kuendesha injini zilizo na oili isiyotosha, chafu, au ya ubora usio sahihi;
3.
Matumizi ya mafuta machafu au yaliyoharibika, petroli yaliyotengenezwa kwa zaidi
ya 10% ya ethanoli, au matumizi ya mafuta kama vile petroli iliyoevuka au gesi
asili kwenye injini ambazo hazijaundwa/kutengenezwa tangu mwanzo na Briggs &
Stratton kuendeshwa kwa mafuta kama hayo;
4.
Uchafu ulioingia kwenye injini kwa sababu ya udumishaji kwa kutumia kisafishaji
hewa kisichofaa au ufunganishaji mbaya;
5.
Kugonga kitu kwa visu vya kukata vya mashine ya kukatia nyasi, adapta, impela
au vifaa vingine vya shafti kombo ambavyo vimelegea au havijawekwa ifaavyo au
ukazaji wa v-belt kupita kiasi;
6.
Sehemu au vifaa vinavyohusiana kama vile klachi, gia, vidhibiti vya kifaa, nk.,
ambavyo havijatolewa na Briggs & Stratton;
7.
Joto kupita kiasi kutokana na vipande vya nyasi, uchafu na vifusi, au viota vya
panya vinavyoziba au kufunika vifaa vya kupoesha au eneo la gurudumu la
kuongeza kasi, au kuendesha injini bila uingizaji hewa wa kutosha;
8.
Mtetemo kupita kiasi kwa ajili ya kasi kupita kiasi, uwekaji injini ikilegea, visua
kukata au impele ambazo zimelegea au havijasawazishwa, au uunganishaji
vibaya wa vipengele vya vifaa kwenye shafti kombo;
9.
Matumizi mabaya, ukosefu wa udumishaji wa mara kwa mara, usafirishaji,
ushughulikiaji, au uwekaji injini vibaya.
1, 2, 3
VanguardEngines.com