Briggs & Stratton 073052-00 WP2RS Manual De Instrucciones página 101

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 20
ILANI HATARI YA GESI YA SUMU. Ekzosi ya injni
huwa na monksidi ya kaboni, gesi ya sumu
inayoweza kukuua ndani ya dakika chache.
HUWEZI kuona, kuinusa, au kuionja. Hata kama
hunusi moshi wa kezosi, bado unaweza kuwa
hatarini mwa gezi ya monoksidi ya kaboni. Ukianza kuhisi
mgonjwa, kisuzi, au mnyonge wakati unatumia bidhaa hii,
nenda mahali penye hewa safi MARA MOJA. Mtembelee
daktari. Waweza pata sumu ya kabon monoksidi.
• Tumia mtambo huu nje PEKEE na mbali na madirisha,
milango na matundu ili kupunguza hatari ya gesi
ya kaboni monoksidi kukusanya na kusababisha
uwezekano wa kuvutwa kwenye sehemu za makazi.
• Simika kamsa ya kaboni monoksidi inayotumia betri
au kamsa ya kaboni monoksidi ya plagi na betri ya
ziada kuambatana na maelekezo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya
monoksidi ya kaboni.
• USIENDESHE mtambo huu ndani ya nyumba, gereji,
vyumba ya chini ya ardhi, ubati, vibanda, au majengo
mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha kwa hewa.
Monoksidi ya kaboni inaweza kukusanyika haraka
katika maeneo haya na ibakie kwa saa kadhaa, hata
baada ya kifaa hiki kuzimwa.
• WAKATI wote weka kifaa hiki kunakoelekea upepo na
kuelekeza ekzosi kinyume cha sehemu za makazi.
ILANI Matumizi ya mtambo huu wa pampu yanaweza
kusababisha vidimbwi na sakafu terezi ambazo
huenda zikasababisha kuanguka kunakoweza
kuleta kifo ama majeraha mabaya.
• Endesha mtambo juu ya sakafu iliyo dhabiti.
• Eneo linapaswa kuwa na miteremko ya kutosha na
mifereji ya maji taka ili kupunguza uwezekano wa
kuanguka kutokana na sakafu telezi.
ILANI Kurudi kwa kamba ya kiasha mtambo (kunywea
haraka) kwaweza kuvuta mkono kuuelekekeza
kwenye mashine kwa kasi kuliko unavyoweza
kuachilia ambako kunaweza sababisha kuvunjika
kwa mkono, kuvunjika mifupa, kupata miparuzo
ama kuteguka na kusababisha majeraha mabaya.
• Wakati unapowasha injini, vuta kamba polepole mpaka
pale ambapo utaweza kuhisi upinzani na kisha uvute kwa
haraka ili kuepuka kukataa kuwashwa kwa mtambo.
• Weka mikono na mwili mbali na pampu ya kumwaga.
• Hifadhi bomba la kumwaga kuzuia kugongwa.
ILANI Stata na sehemu zingine zinazozunguka zaweza
kunasa mkono, nywele, nguo ama vivalio vingine
na kusababisha majeraha mabaya.
• USIDHUBUTU kuweka mikono au sehemu zingine za mili
katika pampu inayonguruma ama katika mabomba.
• USIWAHI kuendesha kioshaji kwa presha bila ya sehemu
za kukifunika au vifuniko.
• USIVALIE mavazi yaliyolegea, johari au kitu chochote
kilicholegea kinachoweza kukamatwa kwenye kiwashi au
sehemu nyingine zinazozunguka.
• Funga nywele ndefu na uondoe johari.
ILANI Mtambo huu umeundwa ili kupiga maji ambayo si
ya kunywewa na binadamu.
ILANI Matumizi mabaya ya mtambo huu yanaweza
kuuharibu na kufupisha maisha yake.
• Kama unayo maswali kuhusu matumizi yaliyonuiwa,
mwulize mwuzaji au wasiliana na kituo cha huduma
kinachofaa.
• Hakikisha kuwa chumba cha pampu kimejazwa maji kabla
ya kungurumisha mtambo. Usiendeshe mtambo huu bila
ya kujaza maji ya msukumo.
• Tumia bomba lisilojikunja upande wa kufyonza wa pampu.
• Tumia mtambo huu kwa matumizi yaliyokusudiwa pekee.
• Kuvuta maji ya bahari, vileo au vinywaji, asidi, michakato
ya kemikali, ama kioevu kingine kinachodumisha kutu
vyaweza kuharibu mtambo
• Hakikisha hakuna kiunganishi chochote kinavuja hewa.
• USIKINGE bomba la kufyonza wala la kumwaga kwa njia
yoyote.
• USIENDESHE mtambo bila kapu la kuchujia katika
upande wa kufyonza.
• USIZIDISHE kiwango cha kilele cha kufyonza (soma
Maelekezo). Tumia kilele cha kufyonza kilicho kifupi
iwezekanavyo.
• USIRUHUSU magari kukanyaga mabomba. Iwapo
utatumia bomba kuvuka barabara, tumia vipande vya
mbao katika kila upande wa bomba kuruhusu magari
kupita bila kukinga wala kubonyeza bomba.
• Hifadhi pampu kuhakikisha "halitembei" wala kuyumba,
hasa kama liko karibu ya mtaro ama pembe ya bonde.
Mtambo huenda ukatumbukia.
• Weka mtambo mbali na ukingo wa mto ama bahari
kuhakikisha ukingo hauporomoki.
• USITUNDIKE vitu vyovyote katika mianya ya kupumua.
• USIWAHI kutumia mashine haya yakiwa na sehemu
zilizovunjika au zinazokosekana, au bila ya sehemu yake
inayoyafunika au vifuniko.
• USIPUUZE kifaa chochote cha usalama katika mashine
haya.
• USIVURUTE mtambo kwa kutumia mabomba - tumia
shikio.
• USIWARURHUSU watu wasiohitimu ama watoto
kuendesha mtambo wala kuukarabati.
• Angalia kuvuja katika mfumo wa mafuta ama kuzorota,
hasa bomba lililochibuka ama kuchafuka, mabano
yaliyolegea ama kutoka, mtungi au kifuniko vilivyoharibika.
Rekebisha makosa yote kabla ya kuendesha mtambo.
• Mtambo huu umeundwa kutumiwa pamoja na vipuri
vilivyoidhinishwa kutoka kwa Briggs & Stratton Power
Products pekee. Iwapo mtambo huu utatumia vipuri
ambavyo HAVIAMBATANI na mapendekezo, mtumizi
atachukua majukumu yote ya hatari na gharama.
5

Publicidad

Tabla de contenido

Solución de problemas

loading

Este manual también es adecuado para:

073051-00 wp3rs

Tabla de contenido