Briggs & Stratton 073052-00 WP2RS Manual De Instrucciones página 105

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 20
Ukarabati
Ratiba Ya Ukarabati
Fuata vipimo vya kila saa au kalenda, vyovyote vile
vinavyokuja mbele. Huduma ya mara kwa mara zaidi
inahitajika wakati unapoendesha kwenye hali mbaya zaidi.
Masaa 5 ya kwanza
Badilisha oili
Kila masaa 8 kutwa
Mafuta Hayaingii
•Safisha chembechembe
Kila masaa 25 kutwa
Safisha chujio la hewa
Safisha kisafishaji kama kipo kwa mtambo
Baada ya masaa 50 kila mwaka *
Badilisha oili *
Ng'arisha na kukagua kishika cheche
Kwa Mwaka
Badilisha kizibo cha cheche
Badilisha chujio la hewa *
Safisha mfumo wa kiyoyozi *
Safisha ongezeko la tope ndani ya pampu
*Karabati mapema kama unatumia katika semu chafu ama ya vumbi.
Mapendekezo ya Jumla
Ukarabati wa mara kwa mara utaboresha utendakazi
na kurefusha maisha kwa kioshaji kwa presha.
Tazama wauzaji wengine wa Utoaji Huduma hii
Walioidhinishwa wa Briggs & Stratton kwa kupata
huduma.
Usakinishaji na kazi kubwa ya ukarabati sharti
zifanywe na watu waliohitimu.
Udhamini wa kioshaji kwa presha haujumlishi vitu,
ambavyo vimetumiwa vibaya au kupuuzwa na
anayevitumia. Kupokea thamani kamili ya udhamini,
opareta lazima kudumisha pampu ya maji kwa mujibu
wa maelekezo katika mwongozo huu.
ILANI Kuhakikisha usalama wa mtambo, tumia tu
vipuri vya asili kutoka kwa mtengenezaji wa kifaa ama
vilivyoidhinishwa na mtengenezaji wa kifaa. Ukiwa na
maswali yoyote kuhusu ubadilishaji wa vipuri katika
mtambo wako, tutembelee kwa tovuti yetu katika:
BRIGGSandSTRATTON.COM.
Uhifadhi
Iwapo utauweka mtambo huu kwa siku 30 bila ya
kuufanyiza kazi, tumia maelekezo yafuatayo kwa jinsi
ya uhifadhi.
Linda Mfumo wa Mafuta
Mafuta inaweza kuoza wakati imehifadhiwa kwa zaidi
ya siku 30. Mafuta yaliyooza husababisha asidi na
fizi kukusanyika katika mfumo wa mafuta au kwenye
sehemu muhimu za kabureta.
Hakuna haja ya kumwaga petroli kutoka injini kama
kiimarishaji cha mafuta ni kinaongezwa kwa mujibu
wa maelekezo. Washia mtambo nje kwa dakika 2 ili
kusambaza kidhibiti katika mfumo wa kuhifadhi mafuta.
Kama petroli katika injini haijawahi kutibiwa na
kiimarishaji cha mafuta, ni lazima imwagwe katika
kontena iliyoidhinishwa.
Acha mtambo ugurumie nje hadi uzime kwa ukosefu
wa mafuta. Matumizi ya kisawazishaji cha mafuta
katika kontena la kuhifadhia kunapendekezwa ili
kudumisha ubora wake.
ILANIMafuta na mivuke yake zina hatari ya kuwaka
na kulipuka na zaweza kusababisha
kuchomeka, moto ama mlipuko
unaoweza kusababisha maafa au
majeraha mabaya.
UNAPOHIFADHI MAFUTA AMA MTAMBO UKIWA NA
MAFUTA
• Hifadhi mbali na tanuu, stova, hita za kuchemshia maji,
au vitu vingine ambavyo vina taa za moto au vyanzo vya
mwako kwa sababu vinaweza kuwasha mivuke ya mafuta.
UNAPOTOA MAFUTA KWA MTAMBO
• ZIMA pampu ya mafuta na kuacha ipunguze joto kwa
dakika mbili kabla ya kutoa kifuniko. Legeza kifuniko
taratibu ili kupunguza shinikizo katika tanki.
• Jaza tangi la mafuta ukiwa nje ya nyumba.
• Hakikisha kwamba mafuta yako mbali na cheche za
moto, miali ya moto, taa zilizo mbele ya mashine, joto, na
vianzio vingine vya kuwasha.
• USIWASHE sigara wala moshi.
Vidokezo Vingine vya Kuhifadhi
1. USIHIFADHI mafuta kutoka kwenye msimu mmoja hadi
mwingine isipokuwa tu kama yametiwa dawa kama
ilivyofafanuliwa katika Linda Mfumo wa Mafuta.
2. Hifadhi mtambo huu katika sehemu iliyo safi, kavu na
kuufunika na kifaa kizuri kisicho na unyevu.
ILANI Vifuniko vya kuhifadhi vyaweza kuwasha moto
na kusababisha kifo ama majeraha mabaya.
• USIWEKE kifuniko ya uhifadhi juu ya kioshaji kwa presha
chenye joto.
• Hakikisha kwamba mitambo hii imepoa kwa muda
unaotosha kabla ya kuweka kifuniko kwenye mitambo hii.
9

Publicidad

Tabla de contenido

Solución de problemas

loading

Este manual también es adecuado para:

073051-00 wp3rs

Tabla de contenido