Udumishaji
Ratiba ya Udumishaji
Fuata mpishano wa saa au kalenda, yoyote ile
inayotangulia. Huduma ya mara kwa mara zaidi
inahitajika wakati unapoendesha kwenye hali mbaya
zaidi.
Saa 5 za Kwanza
• Badilisha oili ya injini
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
• Safisha vifusi
• Kagua kiwango cha oili ya injini
Kila Baada ya Saa 25 au Kila Mwaka
• Safisha chujio la hewa la injini
Kila Baada ya Saa 50 au Kila Mwaka
• Kagua mafla na kishika cheche
Kila Baada ya Saa 100 au Kila Mwaka
• Badilisha oili ya injini
Kila Mwaka
• Badilisha chujio la hewa la injini
• Badilisha plagi ya spaki
Fanya huduma mara nyingi zaidi katika hali chafu au zenye
1
vumbi.
Tembelea muuzaji huduma aliyeidhinishwa.
2
Mapendekezo Jumla
Udumishaji wa mara kwa mara utaboresha utendakazi
na kuongezea maisha ya jenereta ya nje. Tembelea
Muuzaji Huduma yeyote Aliyeidhinishwa wa Briggs &
Stratton ili kuhudumiwa. Uwekaji sehemu na kazi kubwa
ya ukarabati ni lazima zifanywe na wafanyikazi wenye
mafunzo maalum.
Hakikisho la jenereta halisimamii vifaa vilivyotumiwa
vibaya na kutelekezwa na mwendeshaji. Ili kupokea
thamani kamili ya hakikisho, ni lazima mwendeshaji
adumishe jenereta jinsi alivyoelekezwa kwenye
mwongozo huu.
ONYO! Ili kuhakikisha usalama wa mashine,
tumia tu sehemu asilia kutoka kwa mtengenezaji
au kuidhinishwa na mtengenezaji. Ukiwa na
maswali kuhusu kubadilisha vijenzi kwenye jenereta
yako, tafadhali tutembelee kwenye tovuti yetu
BRIGGSandSTRATTON.COM.
TAHADHARI Kasi za juu au chini zaidi kupita
kasi zinaweza kusababisha majeraha madogo.
Usichokore springi ya gavana, viungo au
sehemu nyingine ili kubadilisha kasi. Usifanye mabadiliko
kwenye jenereta kwa njia yoyote ile.
EU Stage V: Viwango vya CO2
Viwango vya CO2 vya injini zilizoidhinishwa za aina
ya Briggs & Stratton vinaweza kupatikana kwenue
BriggsandStratton.com kwa kucharaza CO2 ndani ya
upau wa kutafuta.
1,2
1
1
1,2
Udumishaji Betri Kielelezo
Jenereta ina mfumo wa kuchaji betri kiotomatiki
unaochaji betri huku injini ikiguruma. Ikiwa jenereta
haitumiki mara nyingi, betri inapaswa kuunganishwa na
chaja ya trickle au kidumishaji betri (hakijajumuishwa) ili
kuiweka ikiwa imechajiwa ipasavyo.
1. Ondoa paneli kutoka mbele ya betri.
2. Tenganisha kiunganishaji cha pini mbili kutoka
kwenye betri hadi jenereta.
ILANI Usizidishe kiwango cha kuchaji cha Amp 1.5.
3. Fuata maagizo yaliyojumuishwa kwenye chaja ya
trickle au kidumishaji betri.
Udumishaji Injini
Kubadilisha Oili ya Injini Mchoro Kielelezo
TAHADHARI Epuka oili ya mota iliyotumika
kugusana na ngozi kwa muda mrefu au mara
nyingi. Oili ya mota iliyotumika imeonekana
kusababisha saratani ya ngozi katika maabara fulani za
wanyama. Safisha kwa kina maeneo yaliyoathirika
ukitumia sabuni na maji.
WEKA MBALI WA WATOTO. USICHAFUE.
TUMIA RASILIMALI VIZURI. REJESHA OILI
ILIYOTUMIKA KWENYE VITUO VYA
KUKUSANYA.
Badilisha oili wakati injini bado ina joto baada ya
kuendeshwa, kama ifuatavyo:
1. Ondoa kifuniko kwenye eneo la kujazia oili.
2. Ondoa kifuniko cha tundu la kumwaga oili (5, B) na
umwage oili yote ndani ya kontena inayofaa.
3. Rejesha kifuniko cha tundu la kumwaga oili na ukaze
vizuri. Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (5, A).
4. Ukitumia faneli ya oili, polepole weka oili
iliyopendekezwa (takriban aunzi 20 (lita 0.6)) ndani
ya tundu la kujazia oili (7). Acha ili kuruhusu oili
kutulia. Jaza hadi ifikie alama inayoonyesha imejaa
(6, A) kwenye kifaa cha kupima kiwango cha oili.
5. Pangusa kifaa cha kupima kiwango cha oili kila
mara kiwango cha oili kinapokaguliwa. Usijaze
kupita kiasi.
6. Rejesha kifaa cha kupima kiwango cha oili. Kaza
kifuniko vizuri.
7. Pangusa oili yoyote iliyomwagika.
8. Rejesha kifuniko kilicho juu ya eneo la kujazia oili.
2
5 6 7
9