Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton 020633-00 Manual Del Usuario página 184

Publicidad

Mwinuko wa Juu
Kwa miinuko zaidi ya mita 1,524 (futi 5,000), Kima cha petroli chini
yaa 85 octane/85 AKI (89 RON) kinakubalika. Ili ufuate sheria za
kuzalisha uchafu, marekebisho ya mwinuko wa juu unahitajika.
Operesheni bila marekebisho haya yatasababisha upungufu kwa
utekelezaji, kuongezeka kwa matumizi ya mafuta, na kuongezeka
kwa uzalishaji wa uchafu. Angalia muuzaji wa Briggs & Stratton
aliyethibitishwa kwa maelezo zaidi kuhusu marekebisho ya miinuko
ya juu. Operesheni ya injini katika mwinuko chini ya mita 762 (futi
2,500) na vifaa vya miinuko ya juu haijapendekezwa.
Eneo la Mashine inayoosha kwa kutumia
Shinikizo
Kielelezo
Sumu ya Kaboni Monoksidi
ONYO! Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya sumu
ambayo inaweza kukuua wewe kwa dakika kadhaa. HUWEZI
kuinusa, kuiona, au kuionja. Hata kama huwezi kunusa mvuke
wa eksozi, unaweza bado kuwa katika hatari ya kuipumua kaboni
monoksidi. Tumia bidhaa hii NJE PEKEE mbali na madirisha, milango
na matundu ili kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi
kukusanyika na uwezekano wa kuwa inasambazwa kuelekea maeneo
ya nje. Weka kamsa ya kaboni monoksidi inayotumia betri au ziweke
kamsa za kaboni monoksidi na betri za ziada kwa mujibu wa maelekezo
ya mtengenezaji. Kamsa za moshi haziwezi kugundua gesi ya kaboni
monoksidi. USITUMIE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, sehemu ya
nyumba iliyo chini ya ardhi, chumba kidogo sana, vibanda, au nafasi
zingine hata kama unatumia vipepeo au milango zilizofunguliwa na
madirisha za kuingizia hewa. Kaboni monoksidi inaweza kujaa haraka
katika nafasi hizi na inaweza tuwama kwa masaa, hata baada ya bidhaa
hii imezimika. DAIMA weka bidhaa hii katika mwelekeo ambao upepo
unavuma na elekeza eksozikutoka nafasi zilizojazwa. Ukianza kujisikia
mgonjwa, kizunguzungu, au dhaifu wakati unatumia bidhaa hii, tafuta
hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Unaweza kuwa na sumu ya
kaboni monoksidi.
Hatari ya Moto
ONYO! Joto ya gesi ya Eksozi/inaweza kuwasha vitu
vinavyoweza kuwaka, haribu miundo au tenki ya mafuta na
kusababisha athari ya moto, ambayo inaweza sababisha kifo
au majeraha makubwa. Weka angalau mita 1.5 (futi 5) kibali pande
zote za mashine inayoosha na shinikizo pamoja na kutoka juu.
Unganisha Mpira wa Maji na Ugavi wa Maji
kwa Pampu
Kielelezo
ILANI Kagua mpira wa maji ulio na shinikizo ya juu ili kupata
makato, mitiririko au uharibifu.
1. Vuta nyuma kwa ukosi wa mpira wa maji ulio na shinikizo ya
juu (P), weka kwenya bunduki ya kufukiza (A) na utoe ukosi.
Vuta mpira wa maji kuhakikisha kuwa iko salama.
2. Ambatanisha sehemu nyingine ya mpira wa maji kwa tundu la
kutoa maji kwenye pampu na ukaze.
3. Kagua tundu la kuingiza maji kabla ya kuunganisha mpira
wa maji wa bustani kwa tundu la kuingiza maji (H). Safisha
pazia kama ina uchafu au uibadilishe kama imeharibika.
USITUMIE mashine ya kuosha inayotumia shinikizo kama
pazia la tundu la kuingizia maji limeharibiwa.
4. Hakikisha chanzo ya maji ina uwezo wa kusambaza maji
katika kiwango cha lita zaidi ya 14.4 (galoni 3.8) kwa dakika
moja na 0.14-0.55 MPa (1.4-5.5 BAR or 20-80 PSI) katika
mashine inayoosha kwa kutumia shinikizo kwa mpira wa maji.
5. Pitisha maji katika mpira wa maji ili kutoa uchafu.
ILANI Tumia maji baridi PEKEE (chini ya 38°C (100°F)).
ILANI Kutumia kizuizi cha mtiririko wa kuja nyuma katika tundu
la kuingiza maji la pampu inaweza kusababisha uharibifu wa
pampu. LAZIMA kuwe na angalau mita 3 (futi 10) ya mpira wa
maji ambao haujazuiliwa kati ya mashine inayoosha ikitumia
shinikizo pamoja na kizuizi cha mtiririko wa kuja nyuma.
6
6
9
4
ONYO! Maji ambayo imetiririka kupitia kizuizi cha
mtiririko wa maji kuja nyuma inachukuliwa kama maji
isiyo safi kwa kunywa.
6. Unganisha mpira wa maji (isizidi mita 15 (futi 50)) kwa tundu
la kuingizia maji na ukaze.
7. WASHA maji, bonyeza kifungo nyekundu katika bunduki,
na ufinye kifyatulio ili usafishe mfumo wa hewa. Badilisha
bunduki kama kifyatulio hakitajifunga.
8. Ambatisha ugani wa bomba (B) kwa bunduki (A) na ukaze.
9. Kuvuta nyuma shingo ya pua ugani, kuingiza dawa ncha (R) na
kutolewa. Tug juu ya dawa ncha ili kuhakikisha ni mahali salama.
Washa Mashine Inayoosha Na Shinikizo
Kielelezo
4
ILANI USITUMIE pampu bila kuiunganisha na maji
yanayosambazwa kuwashwa.
1. Songeza wenzo ya transfoma ndogo ya gari (F) hadi kwa
nafasi ya FAST (
), iliyoonyeshwa kwa injini kama sungura
ONYO! Mashine ya kuwasha injini na sehemu zingine
zinazozunguka zinaweza kunasa mikono, nywele, nguo,
au vifaa na hivyo kusababisha majeraha makubwa.
USIWAHI kutumia mashine inayoosha kwa kutumia shinikizo bila
vifaa vya kukinga majeraha. USIVAE nguo zisizokushika,
mapambo au kitu chochote ambacho kinaweza kuwa hawakupata
katika mashine ya kuwasha injini au kupokezana sehemu
nyingine. Funganisha nywele ndefu na utoe mapambo.
ILANI Kabla ya kuwasha mashine inayoosha kwa kutumia
shinikizo, hakikisha umevaa miwani na mavazi za kukinga majeraha.
ONYO! Mvuke unaweza kumichia nyuma au
kutupa vitu na kusababisha majeraha makubwa.
Hakikisha umevaa miwani za usalama zilizo na
tundu (michia ya kemikali) zilizothibitishwa kuzingatia ANSI Z87.1 wakati
unatumia ama ukiwa maeneo ya kifaa hiki. Hakikisha umevaa mavazi
ya kukinga kama vile shati iliyo na mikono mirefu, longi na viatu,
ILANI Kitengo hiki kimetengenezwa na injini ya ReadyStart®
kumaanisha hakuna utayarishaji au kupunguza hewa kwa injini
unaohitajika.
2. Wakati unawasha injini, shika mpini wa nywea na uivute
polepole hadi usikie ikianza kuwa ngumu. Kisha uvute kwa
kasi ili uwashe injine.
ONYO! Kamba ya mashine ya kuwasha injini inaweza
nywea (kurudi kwa kasi) na kuvuta mkono kuelekea injini
kwa kasi kabla uiachilie na inaweza kusababisha kuvunjika
mifupa, michubuko, na kuvunja viungo hivyo kusababisha majeraha
makubwa. USIWAHI vuta kamba ya mashine ya kuwasha injini bila
kwanza kupunguza shinikizo katika mfukizo wa bunduki. Wakati wa
kuwasha injini, vuta kamba polepole mpaka usikie ugumu kisha vuta
kwa kasi ili uepuke nywea. Shikilia bunduki ya mfukizo imara kwa
mikono miwili wakati wa kutumia mfukizo wa shinikizo ya juu ili
uepuke kuumia wakati bunduki itanywea.
3. Rudisha mpini wa nywea polepole. USIIRUHUSU kamba
kunywea kwa mashine ya kuwasha injini.
4. Baada ya kila jaribio la kuwasha, wakati injini imekataa
kuanza, elekeza bunduki ya mfukizo katika mwelekeo
salama, bonyeza kitufe nyekundu na ufinye kifyatulio kwa
bunduki ya mfukizo ili utoe shinikizo ilio juu.
ILANI Daima weka wenzo ya transfoma ndogo ya gari kwa nafasi ya
FAST (
) wakati unatumia mashine inayoosha kwa kutumia shinikizo.
ONYO! Mkondo wa maji ulio na shinikizo ya juu ambayo
kifaa hii inazalisha inaweza kukata ngozi na nyama, hivo
kusababisha majeraha makubwa na kukatwa kwa kiungo
cha mwili. Kama umekatwa na maji, mwone daktari mara moja.
USIITIBU kama jeraha la kawaida. USIWAHI lenga bunduki ya
mfukizo kwa watu, wanyama, au mimea. USIIFICHE bunduki ya
mfukizo katika nafasi ilio wazi. USIIWACHE bunduki ya mfukizo
bila kuifuatilia wakati mashine inatumika. USIWAHI kuitumia
bunduki ya mfukizo ambayo haina kinga ya kifyatulio au mlinzi wa
kifyatulio na inafanya kazi. USIWAHI unganisha mpira wa maji ulio
na shinikizo ya juu kwa ugani wa bomba.
BRIGGSandSTRATTON.COM
BRIGGSandSTRATTON.COM

Publicidad

loading

Este manual también es adecuado para:

Bpw2500