Briggs & Stratton BPW4000 Manual Del Usuario página 197

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 60
Operesheni
Mafuta
Mapendekezo ya Mafuta Mchoro 5
Tunapendekeza matumizi ya mafuta Yaliyoidhinishwa ya
Udhamini wa Briggs & Stratton kwa utendakazi bora zaidi. Mafuta
mengine ya ubora wa juu ya kitakasaji yanakubalika endapo
yameainishwa kuwa ya huduma ya SF, SG, SH, SJ au juu zaidi.
USITUMIE nyongeza maalum.
Hali ya joto ya nje ya nyumba huamua mnato na uzito wa mafuta
hayo katika injini husika. Tumia mchoro huu ili kuteua mnato na uzito
zaidi wa kipimo cha hali joto ya nje ya nyumba ambayo inatarajiwa.
* Chini ya 4°C (40°F) matumizi ya SAE 30 yatasababisha
matatizo katika kuwasha mashine.
** Juu ya 27°C (80°F) matumizi ya 10W30 yanaweza kusababsha
matumizi yaliyoongezeka ya mafuta. Angalia kiwango cha
mafuta mara nyingi zaidi.
Ukaguzi/Kuongeza Mafuta ya Injini Mchoro 6
Kiwango cha mafuta kinafaa kukaguliwa kabla ya kila matumizi au
angaa kila baada ya saa 8 za operesheni. Hakikisha kiwango cha
mafuta kinatosha na hakipungui.
1. Hakikisha kioshaji kwa presha kiko kwenye sehemu ambayo
haijainuka.
2. Safisha eneo linalozungukia mahali pa kutilia mafuta (oil),
ondoa kifuniko cha mafuta (oil)/kijiti kirefu kinachokuwa
ndani na ukisafishe. Chomeka kijiti hicho, USIkizungushie
ndani. Ondoa na ukague kiwango cha mafuta (oil).
3. Dhibitisha mafuta (oil) yako kwenye alama ya KUJAA (A)
kwenye kijiti hicho.
4. Kama itahitajika, tia mafuta (oil) polepole kupitia kwenye
sehemu hiyo ya kujazia mafuta (oil) hadi kufikia kwenye
alama ya KUJAA kwenye kijiti hicho husika. Sita ili kuruhusu
mafuta (oil) kutulia. USIjaze kupindukia.
5. Sawazisha na ukaze kifuniko cha mafuta.
ARIFA USIJARIBU kuanzisha au kuwasha injini kabla
haijahudumiwa kikamilifu kwa mafuta yaliyopendekezwa. Hii
inaweza kusababisha kushindikana kwa injini.
TAHADHARI Epuka mtagusano wa ngozi wa muda mrefu au
wa mara kwa mara na mafuta ya gari yaliyotumiwa. Mafuta ya
gari yaliyotumiwa yamegunduliwa kusababisha saratani ya ngozi
katika wanyama fulani kule maabarani. Safisha kikamilifu sehemu
zilizomwagikiwa kwa sabuni na maji.
WEKA MBALI NA WATOTO. USICHAFUE. HIFADHI
RASILIMALI. RUDISHA MAFUTA YALIYOTUMIWA
KWENYE VITUO VINAVYOYAKUSANYA.
Ongeza Mafuta Mchoro
Lazima mafuta yatimize mahitaji haya:
• Mafuta safi, matulifu, yasiyokuwa na risasi.
• Kiwango cha chini zaidi cha okteni/87 AKI (91 RON) 87.
Kwenye sehemu za milimani tumia, tazama Sehemu za
Milimani.
• Mafuta yaliyo na hadhi ethanoli 10% (gasohol) inakubalika.
ARIFA Matumizi ya mafuta ambayo hayajaidhinishwa yanaweza
kuharibu jenereta na kuharibu udhamini wa mashine haya.
USITUMIE mafuta ambayo hayajaidhinishwa kama vile E15 na
E85. USICHANGANYE mafuta (oil) kwenye mafuta (gasoline) au
kubadilisha injini ili iweze kuendeshwa kwa kutumia mafuta mbadala.
Ili kulinda mfumo wa mafuta dhidi ya uundaji wa gamu changanya
kidhibiti cha mafuta wakati unapokuwa ukiongeza mafuta kwenye
mashine yako. Tazama Uhifadhi. Mafuta yote si sawa. Kama
utapitia hali yenye matatizo ya kuanza au utendakazi wa mashine
haya baada ya kutumia mafuta, basi badilisha mhudumu wako
wa mafuta au badilisha nembo za mafuta. Injini hii imeidhinishjwa
katika kufanya kazi kwa kutumia mafuta (gasoline). Mfumo wa
udhibiti wa utoaji moshi wa injini hii ni EM (Marekebisho ya Injini).
7
ONYO! Mafuta na mvuke wake vyote vinaweza
kuwaka moto na kulipuka na hivyo basi kusababisha
kuungua, moto au milipuko inayoweza kusababisha
kifo au majeraha mabaya. Zima injini ya kioshaji kwa presha na
ukiwache kitulie kwa angaa dakika 2 kabla ya kuondoa kifuniko cha
tangi la mafuta. Legeza kifuniko hicho polepole ili kutoa presha
kwenye tangi. Jaza tangi la mafuta ukiwa nje ya nyumba.
USIZIDISHE mafuta kwenye tangi la mafuta. Ruhusu nafasi kwa
upanuzi wa mafuta. Kama mafuta yatamwagika, subiri mpaka pale
ambapo yatakapoyeyuka kabla ya kuwasha injini. Hakikisha
kwamba mafuta yako mbali na cheche za moto, miali ya moto, taa
zilizo mbele ya mashine, joto, na vianzio vingine vya kuwasha.
Angalia viwango vya mafuta, tangi, kifuniko na vinginevyo mara
kwa mara ili kujua kama kuna nyufa au uvujaji wowote. Sawazisha
kama itahitajika. USIWASHE sigara wala moshi.
1. Safisha eneo lililo karibu na kifuniko cha tangi la mafuta,
ondoa kifuniko.
2. Polepole ongeza mafuta ya kawaida yasiyo na risasi (A)
ili kutia mafuta kwenye tangi (B). Kuwa makini ili yasifurike.
Ruhusu karibu nafasi ya tangi ipatayo sentimita 4 (1.5") (C)
ya tangi kwa minajili ya kupanuka kwa mafuta.
3. Rudisha kifuniko cha tangi la mafuta na huruhusu mafuta
yoyote yaliyomwagika kuyeyuka kabla ya kuwasha injini.
Sehemu ya Milimani
Katika sehemu za milimani zilizo juu ya 1524 m (5,000 ft.),
kiwango kidogo cha mafuta ya okteni 85 / 85 AKI (89 RON)
yanakubalika. Ili kubakia kuwa na ukubalifu wa utoaji moshi,
marekebisho ya sehemu za milimani yanahitajia. Operesheni
bila ya marekebisho haya itasababisha utendakazi uliopungua,
matumizi ya mafuta yaliyoongezeka, na utoaji moshi
ulioongezeka. Tazama Mwuzaji Aliyeidhinishwa wa Briggs
& Stratton kwa sehemu za mlimani kwa minajili ya taarifa
marekebisho haya. Operesheni ya injini katika sehemu za
milimani zilizo chini ya mita 762 m (2,500 ft.) pamoja na mkoba
wa sehemu za milima ya juu haipendekezwi.
Mahali pa Kioshaji kwa Presha Mchoro
Uwekaji Sumu wa Carbon Monoxide
ONYO! Kitolea moshi cha injini kinayo Carbon Monoxide,
gesi yenye sumu inayoweza kuua kwa dakika chache.
HUWEZI kuinusa, kuiona, au hata kuiramba. Hata kama
huwezi kunusia moshi unaotolewa, bado unaweza kukumbana na
gesi ya Carbon Monoxide. Tumia bidhaa hii nje ya nyumba
PEKEE mbali na madirisha, milango matundu ya kupitishia hewa
ili kupunguza hatari ya Carbon Monoxide dhidi ya kukusanyika na
kuwa na uwezo wa kuvutwa kuelekea kwenye nafasi zile
nyingine. Weka ving'ora vya Carbon Monoxide vinavyoendeshwa
betri au ving'ora vya Carbon Monoxide vya kuchomekwa vilivyo
na chelezo cha betri kulingana na maelekezo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kugudua gesi ya Carbon Monoxide.
USITUMIE bidhaa hii ndani ya nyumba, gareji, vyumba vya chini
kwa chini, nafasi za kutambalia, vibada vya kuifadhia vitu, au
sehemu nyingine zilizofunikwa-kiasi ata kama unatumia feni au
unaifungua milango na madirisha kwa minajili ya kupitisha hewa.
Carbon monoxide inaweza kushinikiza kwenye nafasi hizi na
kubakia hapo kwa saa kadhaa, ata baada ya bidhaa hii kuzimwa.
SIKU ZOTE weka bidhaa hii mahali ambapo upepo unavuma
ukielekea na uelekeze kitolea moshi cha injini mbali na nafasi hizi
tumika. Ukianza kuhisi mgonjwa, kisuzi, au mnyonge wakati
unatumia bidhaa hii, nenda mahali penye hewa safi MARA
MOJA. Mwone daktari. Huenda unaweza kuwa umepumua sumu
ya Carbon Monoxide.
Hatari ya Uondoaji wa Moto
ONYO! Joto/gesi zinazotolewa zinaweza kusababisha
kuwashwa kwa moto, vibanda au uharibifu wa tangi ya
mafuta na hivyo basi kusabaisha moto, na kuishia kuleta
vifo au majeraha mabaya. Hakikisha kwamba uko mbali na pande
zote za kioshaji kwa presha kwa angaa mita 1.5 (5 ft.) pamoja na
sehemu ile ya juu.
8
5 5

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido