Briggs & Stratton BPW4000 Manual Del Usuario página 199

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 60
Ili Kubadilisha Ncha za Mnyunyizo:
1. Rudisha nyuma sehemu ya pembeni iliyo kwenye
mwunganisho-chapu na uvute ncha ya sasa ya mnyunyizo
hadi kuzima. Hifadhi ncha za mnyunyizo kwenye mashimo
yaliyowekwa kwenye trei ya nyongeza.
2. Teua ncha pendelewa ya mnyunyizo:
kwa kusuuza kwa makini, teua ncha ya minyunyizo
nyeupe ya 40 (A) au ya kijani (B) ya 25°.
Kwa kusuuza kwa jumla, teua ncha ya mnyunyizo (C) ya
njano ya 15°
Kwa kusuuza kwa kiwango cha juu zaidi, teua ncha ya
mnyunyizo (D) nyekundu ya 0°
Ili kutumia sabuni, teua ncha ya mnyunyizo (E) nyeusi ya
sabuni.
3. Vuta nyuma sehemu ya pembeni, chomeka ncha mpya ya
mnyunyizo na uwachilie sehemu hiyo ya pembeni. Weka
vyema ncha ya mnyunyizo na uhakikishe kwamba iko
salama.
Vidokezo vya Matumizi
• Kwa usafishaji kamilifu, hakikisha kwamba ncha ya
mnyunyizo iko umbali wa sentimita 20 hadi sentimita 61
(nchi 8 hadi 24) mbali na sehemu ya usafishaji.
• Ukisongeza ncha ya mnyunyizo karibu sana, haswa kwa
kutumia ncha ya mnyunyizo ya presha ya juu unaweza
kuharibu sehemu inayosafishwa.
• USISONGEE karibu sana umbali ulio karibu zaidi sentimita
15 (nchi 6) wakati unaposafisha magurudumu.
Matumizi ya Sabuni
ONYO! Kemikali zinaweza kusababisha kuungua
kunakosababisha kifo au majeraha mabaya. USITUMIE
kiolevu kinachotokana na magadi soda katika kioshaji cha
presha. Tumia TU kioshaji kwa presha na sabuni/vioshaji salama.
Fuata maelekezo ya utengenezaji.
1. Weka neva ya kuvuta sabuni kwenye mkebe ule wa sabuni.
2. Weka ncha ya nyeusi ya mnyunyizo wa sabuni.
ARIFA Sabuni haiwezi kutumiwa kwenye ncha za mnyunyizo
zilizo na presha ya juu (Nyeupe, Njano, Nyekundu).
3. Tumia sabuni katika sakafu kavu, ukianzia katika sehemu ya
chini zaidi inayofaa kuoshwa, kwa kutumia miguso mirefu,
pamoja na ile ya kujirudia.
4. Ruhusu sabuni kuweza "kuroweka" kulingana na maelekezo
ya utengenezaji wa sabuni kabla ya kuosha na kusuuza.
ARIFA Piga maji mfumo wa kuvuta sabuni baada ya kila
matumizi kwa kuweka neva kwenye ndoo ya maji safi, kisha
kuwasha kioshaji kwa presha kwa kutumia ncha nyeusi ya
mnyunyizo kwa dakika 1-2.
Kusuuza kwa kutumia Kioshaji kwa Presha
Mchoro
3
1. Ondoa ncha nyeusi ya mnyunyizo wa sabuni kutoka kwenye
kirefusho cha pua.
2. Teua na uweke ncha ya presha ya juu ya mnyunyizo.
ONYO! Kule kurudi nyuma kwa sehemu ya mbele ya
mnyunyizo (43 N) kunaweza kufanya kuanguka na
kusababisha kifo au majeraha mabaya. Tumia kioshaji kwa
presha kutoka kwenye sehemu dhabiti. Kuwa makini sana kama
lazima utumie kioshaji kwa presha kutoka kwenye ngazi, viunzi,
au mahali popote pengine kama hapo. Shikilia kwa nguvu
sehemu ile ya mbele ya mnyunyizo kwa mikono yote miwili wakati
unapotumia mnyunyizo wa presha ya juu ili kuepuka jeraha
wakati ambapo sehemu ya mbele ya mnyunyizo itakaporuka
nyuma.
3. Ongeza (punguza) presha ya mnyunyizo kwa kuzungusha
kishikio cha kudhibiti presha (A) kuanzia mkono wa kulia
hadi kushoto (tofauti na kuanzia kushoto hadi kulia).
Tumia presha ya chini zaidi kuviosha vitu kama vile gari
au mashua. Tumia presha ya juu zaidi kuondoa rangi na
kuondoa mafuta yasiofaa kwenye maegesho.
4. Tumia mnyunyizo wa presha ya juu katika eneo ndogo na
ukague sehemu hiyo endapo imeharibika. Kama haijaribika,
endelea kusuuza.
5. Anzia sehemu ya juu inayofaa kusuuzwa, ukija chini
kwa miguso ile ya kujirudia kama ulivyofanya wakati wa
usafishaji.
Mfumo Otomatiki wa Kupoza
(Punguzo la Kijoto(
Kupitisha maji kwenye pampu kunaweza kufikia halijoto ya juu ya
51°C (125°F) kama unaendesha kioshaji kwa presha kwa dakika
3-5 bila ya kubonyeza triga kwenye sehemu hiyo ya mbele.
Mfumo huo unahusisha pampu ya kupoza kwa kumwaga maji
yenye joto kwenye sakafu.
Kusitisha Kioshaji kwa Presha
1. Achilia triga ya sehemu ya mbele ya mnyunyizo na uiache
injini kwenda hivyo tu kwa dakika mbili.
2. Songeza throto hadi mkao wa (
wa (
) SITISHA.
3. Zima mafuta na kuyaweka kwenye mkao wa (
4. SIKU ZOTE elekeza sehemu ya mbele ya mnyunyizo katika
upande salama, bonyeza kitufe chekundu na uifinye triga
ya sehemu ya mbele ya mnyunyizo na uiwachilie ili iweze
kuachilia presha ya juu, kila wakati unapositisha injini.
ONYO! Sehemu ya mbele ya mnyunyizo hunasa presha
ya juu ya maji, ata pale ambapo injini imesitishwa na maji
yamekatizwa, hali ambayo inaweza kusababisha majeraha
mabaya. Hakikisha kwamba mpira wa maji uliounganisha kwenye
pampu unayo presha ya juu na sehemu ya mbele ya mnyunyizo
vilevile wakati mfumo unapoongezwa presha. SIKU ZOTE
elekeza sehemu ya mbele ya mnyunyizo katika upande salama,
bonyeza kitufe chekundu na uifinye triga ya sehemu ya mbele ya
mnyunyizo ili kuachilia presha ya juu, kila wakati unapositisha
injini.
Baada ya Kila Matumizi
Maji yanafaa kubakia kwenye kitengo hicho kwa vipindi virefu vya
muda. Chembechembe au madini yanaweza kubakia kwenye
sehemu za pampu na kugandisha utenda kazi wa pampu. Fuata
taratibu hizi baada ya kila matumizi:
1. Zima chanzo cha maji, na uiwache injini ipoe.
2. Katiza mpira wa maji kutoka kwenye sehemu ya mbele ya
mtambo na sehemu inayotoa maji kwenye pampu. Ondoa
maji kutoka kwenye mpira wa maji, sehemu ya mbele ya
mtambo na kirefusho cha pua.
3. Weka ncha za mnyunyizo na mpira wa maji kwenye trei
ya nyongeza. Weka sehemu ya mbele ya mnyunyizo na
kirefusho cha pua kwenye nyaya husika.
4. Ondoa kwenye pampu viowevu vyote kwa kukivuta kishikio
cha waya karibu mara sita.
5. Hifadhi kitengo hicho katika eneo safi, kavu.
ARIFA Kama unahifadhi kwa zaidi ya siku 30, tazama Hifadhi.
ONYO! Mafuta na mvuke wake vyote vinaweza
kuwaka moto na kulipuka na hivyo basi
kusababisha kuungua, moto au milipuko inayoweza
kusababisha kifo au majeraha mabaya. Wakati unahifadhi mafuta
au mitambo iliyo na mafuta kwenye tangi, ihifadhi mbali na tanuu,
stovu, vipashaji maji moto, vikaushaji vya nguo, au mitambo
mingineyo iliyo na taa zilizoko kwenye sehemu ya mbele au
chanzo kingine cha kuwaka kwa sababu inaweza kuwasha
mivuke ya mafuta.
) POLEPOLE kisha mkao
) ZIMA.
7 7

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido