Briggs & Stratton 110000 Manual Del Operario página 49

Ocultar thumbs Ver también para 110000:
Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 16
Petroli safi, freshi, yasiyo na isiyo na lead.
Kiwango cha chini cha 87 okteni/87 AKI (91 RON). Matumizi ya mwinuko wa juu,
tazama hapa chini.
Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% (gasohol) inakubalika.
Notisi
Usitumie petroli isiyoidhinishwa, kama vile E15 na E85. Usichanaganye mafuta
kwenye petroli au kurekebisha injini ili kuendesha fueli mbadala. Usitumie fueli
isiyoidhinishwa itaharibu vipengele vya injini, ambavyo havitashughulikiwa chini ya
udhamini.
Ili kulinda mfumo wa fueli kutokana na utengenezaji wa gundi, changanya kiimarishaji cha
fueli kwenye fueli. Tazama Hifadhi . Fueli zote sio sawa. Iwapo matatizo ya kuanza au
utendakazi yatatokea, badilisha mtoaji fueli au badilisha chapa. Injini hii imeidhinishwa
kuendesha kutumia petroli. Mfumo wa kudhibiti uchafuzi wa injini hii ni EM (Marekebisho
ya Injini).
Mwinuko wa Juu
Katika mwinuko wa zaidi ya futi 5,000 (mita1524), kiwango cha chini cha okteni 85 /85 AKI
(89 RON) petroli inakubaliwa.
Kwa injini iliyo na kabureta, marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika ili kudumisha
utendakazi. Oparesheni bila marekebisho unaweza kusababisha kupunguka kwa
utendakazi, matumizi ya fueli yalioongezeka, na uchafuzi ulioongezeka. Wasiliana na Mtoa
Huduma wa Briggs & Stratton Aliyeidhibishwa kwa maelezo ya marekebisho ya mwinuko
wa juu. Oparesheni wa injini katika mwinuko wa chini ya futi 2,500 (mita 762) na
marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
Kwa injini za Uinjizaji wa Fueli wa Kielektriki (EFI), hakuna marekebisho ya mwinuko wa
juu yanahitajika.
Ongeza Mafuta
Tazama Kelelezo: 7
Onyo
Fueli na mvuke wako unawaka na kulipuka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
Wakati wa kuongeza fueli
Zima injini na uruhusu injini kupoa angalau dakika 2 kabla ya kuondoa kifuniko cha
fueli.
Jaza tangi la fueli nje au katika eneo linaruhusu hewa kuingia vizuri.
Usijaze tangi la fueli kupita kiasi. Ili kuruhusu upanukaji wa fueli, usijaze kupita chini
ya shingo la tangi la fueli.
Hifadhi fueli mbali na cheche, miale iliyo wazi, taa za mwongozo, joto na vyanzo
vingine vya uwakaji.
Angalia tundu, tangi, kifuniko na kurekebisha mara kwa mara kwa nyufa na uvujaji.
Badilisha ikiwezekana.
Iwapo fueli itamwagika, subiri hadi ivukize kabla ya kuwasha injini.
1.
Safisha kifuniko cha fueli kutokana na uchafu. Ondoa kifuniko cha fueli.
2.
Jaza tangi la fueli kwa fueli (A, Kielelezo 7). Ili kuruhusu upanuzi wa fueli, usijaze
juu ya chini ya shingo la tangi la fueli (B).
3.
Sakinisha upya kifuniko cha fueli.
Washa na Simamisha Injini
Tazama Kielelezo: 8, 9, 10
Washa Injini
Onyo
Uvutaji nyuma kwa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Inaweza kupelekea mifupa kuvunjika, michubuko au kuteguka maungo.
Wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi inakuwa
gumu kuvuta na kisha uvute kwa haraka ili kuzuia kuvutwa nyuma kwa haraka.
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuwasha Injini
Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha mafuta, na kisafishaji hewa
(iwapo kipo) vimefungwa na kukazwa.
Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
Injini ikifurika, weka choki (ikiwa ipo) katika eneo la kuonyesha FUNGUA / ENDESHA
(OPEN / RUN), songeza kidhibiti injini (ikiwa kipo) hadi eneo la kuonyesha HARAKA
(FAST) na ushtue hadi injini iwake.
Onyo
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina gesi ya kaboni monoksidi,
gesi yenye sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika kadhaa. HUAWEZI kuiona,
kuinusa wala kuionja. Hata kama hauwezi kunusa mafukizo yanayotolewa, bado
unaweza kugusana na gesi ya kaboni monoksidi. Ukianza kuhisi mgonjwa,
kizunguzungu, au mchovu wakati unatumia bidhaa hii, izime na uende eneo lenye
hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda umegusana na sumu ya kaboni
monoksidi.
Tumia bidhaa hii TU nje, mbali na madirisha, milango na matundu ili kupunguza
hatari ya gesi ya kaboni monoksidi kukusanyika na uwezekano wa kuwa inasambazwa
kuelekea maeneo yenye watu.
Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa monoksidi ya kaboni vinavyotumia betri
pamoja na hifadhi ya betri kulingana na maagizo ya mtengenezaji. Ving'ora vya
moshi haviwezi kutambua gesi ya monoksidi ya kaboni.
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi, ubati,
vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi ama
kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Gesi ya kaboni monoksidi inaweza
kukusanyika kwa haraka katika maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa, hata
baada ya bidhaa hii kuzimwa.
KILA WAKATI Weka bidhaa hii upande ambao upepo unatelekea na uelekeze ekzosi
mbali na maeneo yenye watu.
Notisi
Injini hii ililetwa kutoka Briggs & Stratton bila oili. Kabla ya kuwasha injini,
hakikisha umeongeza oili kulingana na maagizo yaliyo kwenye mwongozo huu. Ukiwasha
injini bila oili, itaharibika kiasi haiwezi kukarabatiwa na hautafidiwa chini ya udhamini.
Tambua Mfumo wa Kuwasha
Kabla ya kuwasha injini, ni lazima utambue aina ya mfumo wa kuwasha ambao uko kwenye
injini yako. Injini yako itakuwa na mojawapo ya aina zifuatazo.
®
Mfumo wa ReadyStart
: Hii ina choki otomatiki inayodhibitiwa na halijoto. Haina
choki ya kudhibiti mwenyewe wala prima.
Mfumo wa Choki: Huu una choki ya kutumiwa kuwasha katika halijoto baridi. Baadhi
ya miundo itakuwa na kidhibiti cha choki tofauti huku miundo mingine itakuwa na
muunganiko wa kidhibiti cha choki na cha injini. Aina hii haina prima.
Ili kuwasha injini yako, fuata maelekezo ya aina yako ya mfumo wa kuwasha.
Kumbuka: Kifaa kinaweza kuwa na vidhibiti vya mbali. Tazama mwongozo wa kifaa kwa
utambuzi na uendeshaji wa vidhibiti vya mbali.
®
Mfumo wa ReadyStart
Kagua oili ya injini. Tazama sehemu ya Kagua Kiwango cha Oili .
1.
2.
Hakikisha vidhibiti vya uendeshaji kifaa, iwapo vipo, vimezimwa.
3.
Songeza vali ya kufungia mafuta (A, Kielelezo 8), ikiwa ipo, hadi eneo la kuonyesha
IMEFUGULIWA (OPEN).
4.
Songeza kidhibiti injini (B, Kielelezo 8), ikiwa kipo, hadi eneo la kuonyesha HARAKA
(FAST). Endesha injini kidhibiti kikiwa katika eneo la kuonyesha HARAKA (FAST).
5.
Bonyeza swichi ya kusimamisha (D, Kielelezo 9), ikiwa ipo, hadi eneo la kuonyesha
IMEWASHWA (ON).
6.
Ikiwa bidhaa ina wenzo wa kusimamisha injini (C, Kielelezo 10), shikilia wenzo wa
kusimamisha injini dhidi ya sehemu ya kushika.
7.
Kianzishaji Upya, iwapo kipo: Kwa uthabiti shikilia sehemu ya kushika ya kamba
ya kianzishaji (E, Kielelezo 8, 9). Vuta kamba ya kianzishaji polepole hadi uhisi
inakuwa gumu kuvuta, kisha uvute kwa haraka.
49

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

120000

Tabla de contenido