Iwapo injini yako imewekwa kitengo cha upunguzaji gia wa 6:1, ihudumie kama
ifuatavyo:
1.
Ondoa plagi ya kujaza mafuta (A, Kielelezo 9) na plagi ya kiwango cha mafuta (B).
2.
Ondoa plagi ya kukamua mafuta (C, Kielelezo 9) na ukamue mafuta kwenye
kontena inayofaa.
3.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 9).
4.
Ili kujaza upya, mwaga polepole mafuta ya kulainisha gia (tazama sehenu ya
Vipimo kwenye shimo la kujaza mafuta (D, Kielelezo 9). Endelea kumwaga hadi
mafuta yafurike kwenye shimo la kiwango cha mafuta (E).
5.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 9).
6.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 9).
Kumbuka: Plagi ya kujaza mafuta (A, Kielelezo 9) ina shimo la tundu (F) na lazima
isakinishwe upande wa juu wa kifuniko gia kama ilivyoonyeshwa.
Upunguzaji Gia wa 2:1 (Kielelezo 10)
Kitengo cha upunguzaji gia wa 2:1 (G, Kielelezo 10) hakihitaji kubadilishwa mafuta.
Shughulikia Kichuja Hewa
Tazama Kelelezo: 11, 12
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
• Kamwe usiwashe na kuendesha wakati uunganishaji wa kisafisha hewa (iwapo
kipo) au kichuja hewa (iwapo kipo) kimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au majimaji yaliyoshinikizwa kusafisha kichujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu kichujio na majimaji yatayeyusha kichujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji wa mahitaji ya huduma.
Modeli mbalimbali aidha zinatumia povu au kichujio cha karatasi. Baadhi ya modeli pia
zinaweza kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na
kutumiwa tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye
injini yako na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Povu ya Hewa
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 11).
2.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 11).
3.
Ondoa mkanda (D, Kielelezo 11) na kisafishaji (E).
4.
Ili kuzuia uchafu kutokana na kuanguka kwenye kabureta, kwa makini ondoa
elementi ya povu kwenye sehemu ya chini ya kichuja hewa, (C, Kielelezo 11).
5.
Ondoa kichujio cha mwanzo kutoka kwenye kichujio (C), (F, Kielelezo 11).
6.
Safisha elementi ya povu kwenye sabuni oevu na maji (C, Kielelezo 11). Finyiza ili
kukausha elementi ya povu kwenye kitambaa safi.
7.
Koleza elementi ya povu kwa mafuta safi ya injini (C, Kielelezo 11). Ili kuondoa
mafuta ya ziada ya injini, finyiza elementi ya povu kwenye kitambaa safi.
8.
Ingiza kifuniko egemezi (F, Kielelezo 11) kwenye elementi ya povu (C).
9.
Sakinisha elementi ya povu (C, Kielezo 11) katika eneo la kichujio cha hewa (G)
na kwenye kitufe (H). Hakikisha kichujio kimeunganishwa sahihi kwenye eneo la
kichujio cha hewa na kulinda kwa bizimu (E).
10.
Sakinisha kifuko na ukilinde kwa bizimu (A), (B, Kielelezo 11). Hakikisha bizimu
imekazwa.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 12).
2.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 12).
3.
Ondoa bizimu (E, Kielelezo 12).
4.
Ili kuzuia uchafu kutokana na kuanguka ndani kabureta, kwa umakini ondoa
kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 12) na kichujio cha (C) kutoka katika eneo la
kuchujia hewa (F).
5.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio katika eneo gumu, (C, Kielelezo
12) Iwapo kichujio ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
6.
Ondoa kichujio cha mwanzo kutoka kwenye kichujio (C), (D, Kielelezo 12).
7.
Osha kisafishaji cha mwazo kwenye sabuni oevu na maji, (D, Kielelezo 12).
Ruhusu kisafishaji cha mwanzo kukauka kabisa. Usiweke mafuta kwenye
kisafishaji cha mwanzo.
42
8.
Kusanya kisafishaji cha mwanzo kilichokauka kwenye kichujio (C), (D, Kielelezo
12).
9.
Sakinisha kichujio (C, Kielezo 12) na kisafishaji (D) cha mwanzo katika eneo la
kichujio cha hewa (F) na kwenye kitufe (G). Hakikisha kichujio kimeunganishwa
sahihi kwenye eneo la kichujio cha hewa na kulinda kwa bizimu (E).
10.
Sakinisha jalada (B, Kielelezo 12) na ulinde kwa bizimu(s) (A). Hakikisha bizimu
imekazwa.
Shughulikia Mfumo wa Kupoesha
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa
moto zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi, n.k., unaweza
kushika moto.
• Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
• Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
Notisi
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa fueli.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa na hewa. Uchafu unaweza kuzuia mtiririko wa hewa na
kusababisha injini kuchemka kupita kiasi, na kusababisha utendakazi mbaya na
kupunguza maisha ya injini.
1.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kuondoa uchafu kutoka kwenye grili ya
kuingiza hewa.
2.
Weka uhusiano, springi na vidhibiti safi.
3.
Weka ene lililo karibu na nyuma ya mafla, iwapo ipo, huru kutokana na uchafu
wowote unaoweza kuwaka.
4.
Hakikisha mapezi ya kupoesha mafuta, iwapo yapo, yako huru kutokana na
uchafu.
Baada ya kipindi cha muda, uchafu unaweza kukusanyika kwenye mapezi ya
kupoesha silinda na kusababisha injini kuwa moto kushinda kiasi. Uchafu huu hauwezi
kuondolewa bila kutokusanyika kwa kiasi fulani kwa injini. Ruhusu Mtoa Huduma wa
Briggs & Stratton Aliyeidhinishwa kukagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa
kama ilivyopendekezwa kwenye Ratiba ya Udumishaji.
Hifadhi
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuhifadhi Mafuta Au Kifaa Kilicho na Mafuta Kwenye Tangi
• Hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji, au vitu vingine ambavyo
vina taa za moto au vyanzo vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha moto
kwenye mvuke wa mafuta.
Mfumo wa Mafuta
Tazama Kielelezo: 13
Hifadhi kiwango cha injini (mkao wa kawaida wa kuendesha). Jaza tangi la mafuta (A,
Kilelezo 13) kwa mafuta. Ili kuruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze kupita chini ya shingo
ya tangi la mafuta (B).
Mafuta yanaweza kuharibika yanapohifadhiwa katika kontena ya uhifadhi kwa zaidi ya
siku 30. Kila mara unapojaza kontena kwa mafuta, ongeza kiimarishaji mafuta kwenye
mafuta kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji. Hii inafanya mafuta kukaa
yakiwa safi na kupunguza matatizo yanayohusiana na mafuta au uchafu katika mfumo
wa mafuta.
Si lazima umwage mafuta kutka kwenye injini wakati kiimarishaji mafuta kinapoongezwa
kama ilivyoagizwa. Kabla ya kuendesha, WASHA injini kwa dakika 2 ili kueneza mafuta
na kiimarishaji kote kwenye mfumo wa mafuta.
Ikiwa petroli ndani ya injini haijatibiwa kwa kiimarishaji mafuta, ni lazima imwagwe
kwenye kontena iliyoidhinishwa. Endesha injini hadi isimame kutokana na ukosefu wa
mafuta. Matumizi ya kiimarishaji mafuta kwenye kontena ya uhifadhi yanapendekezwa ili
kudumisha usafi.
Mafuta ya Injini
Wakati injini bado ina joto, badilisha mafuta ya injini. Tazama sehemu Kubadilisha
Mafuta ya Injini.
BRIGGSandSTRATTON.com