Briggs & Stratton WP2-60 Manual Del Usuario página 207

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 60
1. Hakikisha mtambo wa kupiga maji uko katika sakafu
tambarare.
2. Safisha eneo lililo karibu na kifuniko cha tangi la
mafuta, ondoa kifuniko.
3. Polepole ongeza mafuta ya kawaida yasiyo na risasi
(A) ili kutia mafuta kwenye tangi (B). Kuwa makini ili
usijaze kupita kiasi. Ili kuruhusu upanuzi wa mafuta,
usijaze zaidi ya chini mwa shingo ya tangi la mafuta.
4. Rudisha kifuniko cha tangi la mafuta na huruhusu
mafuta yoyote yaliyomwagika kuyeyuka kabla ya
kuwasha injini.
Mwinuko wa Juu
Katika sehemu za milimani zilizo juu ya mita 1524 (futi
5,000), kiwango kidogo cha mafuta ya okteni 85 / 85
AKI (89 RON) yanakubalika. Ili uendelee kuzingatia
utoaji moshi, marekebisho ya mwinuko wa juu
yanahitajika. Uendeshaji bila marekebisho haya unaweza
kusababisha kupunguka kwa utendakazi, matumizi
ya fueli yalioongezeka, na uchafuzi ulioongezeka.
Tazama Mwuzaji Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton
kwa sehemu za mlimani kwa minajili ya taarifa ya
marekebisho haya. Uendeshaji wa injini katika sehemu
za milimani zilizo chini ya mita 762 (futi 2,500) pamoja na
mkoba wa sehemu za milima ya juu haipendekezwi.
Kusanya na Uunganishe Mabomba
Utahitaji kifaa kifuatacho ili kufunga mabomba katika
pampu ya maji:
• kizungusha nati cha milimita 10
Unganisha Bomba la Kunyonya Katika Pampu
Tumia bomba linalopatikana kwa maduka. Bomba la
kufyonza sharti lidhibitiwe na ukuta usiobonyea ama kifaa
kilichosokotwa. USITUMIE bomba ambalo kipenyo chake
cha ndani ni kidogo kuliko kipenyo cha pampu cha kufyonza.
1. Telezesha sijafu-mwiba juu ya bomba-mwiba.
Pachika kikuku cha mpira mwishoni mwa sijafu-
mwiba. Kielelezo
2. Funga sijafu-mwiba katika mfumo wa pampu kwa
kusokota kwa mzunguko wa saa hadi mfumo wa
sijafu-mwiba umakazika kimakinifu. Kielelezo
3. Telezesha bano la bomba juu ya mwisho wa bomba.
Telezesha bomba la kufyonza juu ya sijafu-mwiba.
Kaza bano la bomba kimakinifu ukitumia kizingusha
nati cha kiwangogezi cha milimita 10. Kielelezo
Unganisha bomba la kufyonza kwa kikapu cha
kuchujia Kielelezo
10
Telezesha bano la bomba juu ya bomba. Ambatanisha
mwisho wazi wa bomba la kufyonza kwa kichujio cha
bomba la sijafu-mwiba. Kaza bano la bomba kimakilifu
ukitumia kizingusha nati cha kiwangogezi cha milimita 10.
Unganisha Bomba La Kumwaga (Hiari)
Ikihitajika, tumia bomba linalopatikana madukani.
USITUMIE bomba ambalo kipenyo chake cha ndani ni
kidogo kuliko kipenyo cha pampu cha kufyonza.
1. Telezesha sijafu-mwiba juu ya bomba-mwiba. Pachika
kikuku cha mpira mwishoni mwa sijafu-mwiba.
2. Funga sijafu-mwiba katika mfumo wa pampu kwa
kusokota kwa mzunguko wa saa hadi mfumo wa
sijafu-mwiba ukazike kimakinifu. Kielelezo
3. Telezesha bano la bomba juu ya bomba la kumwaga.
Telezesha bomba la kumwaga juu ya sijafu-mwiba.
Kaza bano la bomba kimakinifu ukitumia kizingusha
nati cha kiwangogezi cha milimita 10. Kielelezo
7
Uendeshaji
Mahali Pa Kuweka Pampu Ya Maji Kielelezo
Kwa utendaji bora zaidi, weka pampu juu ya sakafu
tambarare, laini karibu iwezekanavyo na mahali pa
kufyonza. Dhibiti pampu ya maji kuzuia kuanguka.
Usitumie mabomba ambayo ni marefu kupita kiasi.
ONYO Joto la ekzosi/mivuke laweza kuwasha
maunzi ya kuwaka, majenzi ama kuharibu
tangi la mafuta, na kusababisha kifo au
majeraha mabaya.
• Hakikisha kwamba uko mbali na pande zote za
kioshaji kwa presha kwa angalau mita 1.5 (5 ft.)
pamoja na sehemu ile ya juu.
Sumu Ya Kaboni Monoksidi
ONYO HATARI YA GESI YA SUMU. Eksozi ya injini
ina monoksidi ya kaboni, gesi ya sumu
ambayo inaweza kukuua wewe kwa dakika
chache. HUWEZI kuiona, kuinusa wala kuionja.
Hata kama huwezi kunusa mafukizo
yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi ya monoksidi
ya kaboni. Ukianza kuhisi mgonjwa, kisunzi, au mnyonge
wakati unatumia bidhaa hii, nenda mahali penye hewa
safi MARA MOJA. Mwone Daktari. Huenda ukawa
umeathiriwa na sumu ya monoksidi ya kaboni.
• Endesha kifaa hiki nje PEKEE mbali na madirisha,
milango na matundu ili kupunguza hatari ya gesi ya
monoksidi ya kaboni kukusanyika na kuenda maeneo
yenye watu.
• Weka ving'ora vya betri vya monoksidi ya kaboni
au weka ving'ora vya betri vya monoksidi ya kaboni
kulingana na maelekezo ya mtengenezaji. Ving'ora vya
moshi haviwezi kutambua gesi ya monoksidi ya kaboni.
• USIENDESHE kifaa hiki ndani ya nyumba, gereji,
sehemu ya nyumba iliyo chini ya ardhi, mahali
pa kutambaa, vibanda, au maeneo mengine
yaliyofunikwa kiasi hata kama unatumia feni au
milango na madirisha yamefunguliwa kwa uingizaji
hewa. Monoksidi ya kaboni inaweza kukusanyika
haraka katika maeneo haya na ibakie kwa saa
kadhaa, hata baada ya kifaa hiki kuzimwa.
8
• Weka kifaa hiki upande upepo unatoka WAKATI WOTE
na ulenge ekzosi mbali na maeneo yenye watu.
"Kichwa" ni nini? Kielelezo
Kichwa kinarejelea urefu wa safu ya maji ambayo
9
yanaweza kutolewa kwa utekelezaji wa pampu.
Kichwa cha Kufyonza (A) ni umbali wa wima katikati
ya pampu na uso wa maji upande wa mvuto wa bomba.
Yaweza pia kuitwa "mwinuo wa ufyonzaji". Shinikizo
la anga la mpigo 1 (14.5 psi) katika usawa wa bahari
huweka wakifu wa uinuaji kwa kichwa cha kufyonza chini
ya takriban Mita 8 (26 ft) kwa pampu yoyote.
Kilele cha Kumwaga (B) ni umbali wa wima baina ya
sehemu ya kipenyo cha pampu cha kumwagia na sehemu
ya kumwaga, ambayo ni ubapa wa kioevu kama pampu
imetumbukizwa au inapiga maji hadi kina cha tangi.
Jinsi kina cha kusukuma maji juu kinapoongezeka, utoaji
wa maji unapungua. Urefu, aina, na kimo cha mabomba
ya kufyonza na kumwaga vyaweza pia kuathiri kwa
ukubwa jinsi utoaji wa maji utakuwa.
Ni muhimu kwa uendeshaji wa ufyonzaji uwe ndio mfupi
11
katika harakati nzima ya kupiga maji. Hili litapunguza
muda wa kumwaga maji katika pampu na kuboresha
utendakazi kwa kuongeza kina cha kupiga maji.
TazamaVipimo Maalum kwa kiwango cha juu cha
12
hesabu ya kilele.
13
16
7

Publicidad

Tabla de contenido

Solución de problemas

loading

Este manual también es adecuado para:

Wp3-65Wp2-35073010-01073011-01073035-00

Tabla de contenido