Briggs & Stratton WP2-60 Manual Del Usuario página 209

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 60
Udumishaji
Ratiba ya Udumishaji
Fuata vipindi vya kila saa au kalenda, vyovyote vile
vinavyokuja mbele. Huduma ya mara kwa mara zaidi
inahitajika wakati unapoendesha kwenye hali mbaya
zaidi.
Saa 5 za kwanza
Badilisha mafuta
Kila baada ya saa 8 au kila siku
Kagua kiwango cha oili
Safisha chembechembe
Kila masaa 25 au kila siku
Safisha chujio la hewa
Safisha kisafishaji cha mwanzo, iwapo kipo
Baada ya masaa 50 kila mwaka
Badilisha oili *
Ng'arisha na kukagua kishika cheche
Kila Mwaka
Badilisha plagi ua kuwasha
Badilisha chujio la hewa *
Safisha mfumo wa kiyoyozi *
Safisha ongezeko la tope ndani ya pampu
*Karabati mapema kama unatumia katika semu chafu ama ya vumbi.
Mapendekezo ya Jumla
Ukarabati wa mara kwa mara utaboresha utendakazi na
kurefusha maisha ya pampu ya maji. Tembelea muuzaji
yeyote wa Briggs & Stratton kwa huduma.
Usakinishaji na kazi kubwa ya ukarabati sharti zifanywe
na wafanyikazi wenye mafunzo maalum.
Udhamini wa pampu ya maji haujumlishi vitu ambavyo
vimetumiwa vibaya au kupuuzwa na anayevitumia.
Kupokea thamani kamili ya udhamini, mwendeshaji
lazima adumishe pampu ya maji kwa mujibu wa
maelekezo katika mwongozo huu.
ONYO Kuhakikisha usalama wa mtambo, tumia tu
vipuri vya asili kutoka kwa mtengenezaji wa kifaa ama
vilivyoidhinishwa na mtengenezaji wa kifaa. Ukiwa na
maswali yoyote kuhusu ubadilishaji wa vipuri katika
mtambo wako, tutembelee kwa tovuti yetu katika
BRIGGSandSTRATTON.COM.
Uhifadhi
Iwapo utauhifadhi mtambo huu kwa siku 30, bila ya
kuufanyiza kazi, tumia mwongozo ufuatao ili kuuandaa
kwa uhifadhi.
Linda Mfumo wa Mafuta
Mafuta yanaweza kuharibika yakihifadhiwa kwa zaidi ya
siku 30. Fueli iliyoharibika inaweza kusababisha mabaki
ya asidi na gundi kutengenezeka kwenye mfumo wa fueli
au kwenye sehemu muhimu za kabureta.
Hakuna haja ya kumwaga petroli kutoka kwenye injini
iwapo kiimarishaji cha fueli kimeongezwa kuzingatia
maelekezo. Washia mtambo nje kwa dakika 2 ili
kusambaza kidhibiti katika mfumo wa kuhifadhi mafuta.
Iwapo petroli kwenye injini haijatibiwa kwa kiimarishaji cha
fueli, lazima imwagwe kwenye kantena iliyoidhinishwa.
Acha mtambo ugurumie nje hadi uzime kwa ukosefu wa
mafuta. Matumizi ya kiimarishaji cha fueli kwenye kontena
iliyohifadhiwa yanapendekezwa ili kuimarisha usafi.
ONYO Mafuta na mivuke yake zina hatari ya
kuwaka na kulipuka na zaweza
kusababisha kuchomeka, moto ama
mlipuko unaoweza kusababisha maafa
au majeraha mabaya.
WAKATI WA KUHIFADHI MAFUTA AU KIFAA
KILICHO NA MAFUTA KWENYE TANGI
• Hifadhi mbali na tanuu, stova, hita za kuchemshia
maji, au vitu vingine ambavyo vina taa za moto au
vyanzo vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha
mivuke ya mafuta.
UNAPOTOA MAFUTA KWA MTAMBO
• ZIMA pampu ya maji na uiwache itulie kwa angalau
dakika 2 kabla ya kuondoa kifuniko cha tangi la
mafuta. Legeza kifuniko hicho polepole ili kutoa
presha kwenye tangi.
• Jaza tangi la mafuta ukiwa nje ya nyumba.
• Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za
gesi, joto, na vyanzo vingine vya mwako.
• USIWASHE sigara wala usivute sigara.
Vidokezo Vingine vya Kuhifadhi
1. USIHIFADHI mafuta kutoka kwenye msimu mmoja
hadi mwingine isipokuwa tu kama yametiwa dawa
kama ilivyofafanuliwa katika Linda Mfumo wa
Mafuta.
2. Hifadhi mtambo huu katika sehemu iliyo safi, kavu
na kuufunika na kifaa kizuri kisicho na unyevu.
ONYO Vifuniko vya kuhifadhi vyaweza kuwasha
moto na kusababisha kifo ama majeraha
mabaya.
• USIWEKE kifuniko ya uhifadhi juu ya kioshaji kwa
presha chenye joto.
• Hakikisha kwamba mitambo hii imepoa kwa muda
unaotosha kabla ya kuweka kifuniko kwenye mitambo
hii.
9

Publicidad

Tabla de contenido

Solución de problemas

loading

Este manual también es adecuado para:

Wp3-65Wp2-35073010-01073011-01073035-00

Tabla de contenido