Briggs & Stratton 120000 Manual Del Operador página 46

Ocultar thumbs Ver también para 120000:
Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 19
Ongeza Oili
Hakikisha injini inadumisha mizani.
Safisha vifusi vyote kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5). Futa oili kwenye kifaa
cha kupima kiwango cha oili ukitumia kitambaa safi.
2.
Polepole weka oili kwenye tundu la kujazia oili ya injini (C, Kielelezo 5). Usijaze
kupita kiasi.  Subiri dakika moja, na kisha ukague kiwango cha oili.
3.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
4.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili
kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 5) kwenye kifaa cha kupima
kiwango cha oili.
5.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 5).
6.
Unganisha waya wa plagi ya spaki kwenye plagi ya/za spaki. Tazama sehemu
ya Kuondoa Oili.
Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa
ONYO 
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Usiwashe na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa (iwapo
kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) kimeondolewa.
NOTISI 
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa iliyoshinikizwa inaweza
kuharibu chujio na vioevu vitayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji ili kujua mahitaji ya huduma.
Miundo tofauti itatumia vichujio vya sifongo au karatasi. Baadhi ya miundo pia iinaweza
kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa
tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako
na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Povu la Hewa
1.
Legeza au uondoe vifaa vya kufunga (A, Kielelezo 14), iwapo vipo.
2.
Fungua au uondoe kifuniko (B, Kielelezo 14).
3.
Kwa uangalifu ondoa elementi ya povu (C, Kielelezo 14) kutoka kwenye sehemu ya
chini ya chujio la hewa.
4.
Osha elementi ya povu (C, Kielelezo 14) kwenye sabuni oevu na maji. Finya
elementi ya povu ukitumia mikono yako ndani ya kitambaa kavu mpaka ikauke.
5.
Tumbukiza elementi ya povu (C, Kielelezo 14) ndani ya oili safi ya injini. Ili kuondoa
oili ya injini isiyohitajika kwenye elementi ya povu, ifinye ukitumia mikono yako
ndani ya kitambaa kavu.
6.
Sakinisha elementi ya povu (C, Kielelezo 14) kwenye sehemu ya chini ya chujio la
hewa.
7.
Funga au weka kifuniko (B, Kielelezo 14) na ufunge vizuri ukitumia bizimu.
Hakikisha kwamba umekaza vizuri.
Chujio la Hewa la Karatasi
1.
Legeza au uondoe bizimu, iwapo zipo, (A, Kielelezo 15, 16).
2.
Fungua au uondoe kifuniko (B, Kielelezo 15, 16).
3.
Kwa makini ondoa kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 15, 16) na chujio (C)
kutoka kwenye eneo la chini la chujio la hewa (F).
4.
Ondoa kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 15, 16), ikiwa kipo, kwenye chujio (C).
5.
Ili kuondoa uchafu usiotakikana kwa utaratibu gongesha chujio (D, Kielelezo 15, 16)
kwenye eneo gumu. Ikiwa chujio ni chafu sana, badilisha kwa chujio jipya.
6.
Osha kisafishaji cha mwazo (D, Kielelezo 15, 16), ikiwa kipo, kwenye sabuni
oevu na maji. Hakikisha kisafishaji cha mwanzo kimekauke kabisa. Usiongeze oili
kwenye kisafishaji cha mwanzo.
7.
Weka pamoja kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 15, 16) kilichokauka, ikiwa kipo,
kwenye chujio (C).
8.
Sakinisha chujio (C, Kielelezo 15, 16) na kisafishaji cha mwanzo (D) kwenye
sehemu ya chini ya chujio la hewa. Hakikisha chujio linatoshea vizuri katika sehemu
ya chini ya chujio cha hewa.
9.
Weka kifuniko (B, Kielelezo 15, 16) na ufunge vizuri ukitumia bizimu (A). Hakikisha
sehemu za kufunga zimekazwa kabisa.
46
Kufanyia Huduma Mfumo wa Mafuta
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
Chujio la Mafuta, iwapo lipo
1.
Kabla ya kubadilisha chujio la mafuta (A, Kielelezo 17), mwaga mafuta kutoka
kwenye tangi ya mafuta au funga vali ya kufunga mafuta. Ikiwa tangi la mafuta si
tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
2.
Finya vichupo (B, Kielelezo 17) kwenye vibanio (C) ukitumia koleo. Ondoa vibanio
kutoka kwenye chujio la mafuta (A).
3.
Zungusha na uvute mirija ya mafuta (D, Kielelezo 17) kutoka kwenye chujio la
mafuta.
4.
Kagua mirija ya mafuta (D, Kielelezo 17) kama kuna nyufa au uvujaji. Ikiwa
inahitajika, badilisha mirija ya mafuta.
5.
Badilisha chujio la mafuta (A, Kielelezo 17).
6.
Funga mirija ya mafuta (D, Kielelezo 17) kwa kutumia vibanio (C).
Hifadhi
Mfumo wa Mafuta
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Kuhifadhi Mafuta
Kwa sababu taa za moto au vyanzo vingine vya mwako vinaweza kusababisha
milipuko, hifadhi mafuta au kifaa mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji,
au vifaa vingine ambavyo vina taa za moto.
KUMBUKA: Miundo mingine ina tangi la mafuta la uhifadhi wima ambao unaruhusu
injini kuinama kwa ajili ya udumishaji au uhifadhi (C, Kielelezo 18). Usihifadhi ikiwa wima
wakati tangi la mafuta limejaa kupita kiwango cha alama ya kiwango cha mafuta (D),
iwapo ipo. Kwa maagizo zaidi, rejelea mwongozo wa kifaa.
Weka injini bila kuinama (mkao wa kawaida wa kuendesha). Jaza tangi la mafuta (A,
Kielelezo 6) kwa mafuta. Ili kuruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze kuzidi shingo ya tangi la
mafuta (B).
Mafuta yanaweza kuganda yanapohifadhiwa kwenye kontena ya uhifadhi kwa zaidi ya
siku 30. Inapendekezwa kutumia kiimarishaji mafuta bila alkoholi na tiba ya ethanoli
kwenye kontena ya kuhifadhi mafuta. Hii inafanya mafuta kukaa yakiwa safi na
kupunguza matatizo yanayohusiana na mafuta au uchafu katika mfumo wa mafuta.
Unapojaza kontena hiyo ya mafuta kwa mafuta, ongeza kiimarishaji mafuta bila
alcoholi kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtenegenzaji. Ikiwa petroli ndani ya injini
haijatibiwa kwa kiimarishaji mafuta, ni lazima imwagwe kwenye kontena iliyoidhinishwa.
Endesha injini hadi mafuta yaishe.
Oili ya Injini
Wakati injini bado ina joto, badilisha oili ya injini. Rejelea sehemu ya Kubadilisha Oili
ya Injini.
Kutatua Matatizo
Usaidizi
Ili kupata usaidizi, wasiliana na muuzaji wa karibu au nenda
kwenyeBRIGGSandSTRATTON.COM au piga simu kwa nambari 1-800-444-7774
(nchini Marekani).
Maelezo na Sehemu za Udumishaji
Vipimo Maalum
120000, 123P00,
Unyonyaji Mafuta
11.58 ci (190 cc)
Shimo
2.688 in (68,28 mm)
Mpigo
2.040 in (51,82 mm)
Kiwango cha Oili
18 - 20 oz (,54 - ,59 L)
Miundo:
Modeli: 140000
125P00
13.60 ci (223 cc)
2.913 in (74 mm)
2.040 in (51,82 mm)
18 - 20 oz (,54 - ,59 L)
BRIGGSandSTRATTON.COM

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

140000

Tabla de contenido