Ondoa Oili
1.
Injini ikiwa imezimwa lakini bado ina joto, tenganisha waya ya plagi ya spaki (D,
Kielelezo 18) na ukiweke mbali na plagi ya spaki (E).
2.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 19).
3.
Injini ina tundu mbili za kumwaga oili. Ondoa kifuniko kimoja cha tundu la
kumwaga oili (F, H, Kielelezo 20). Mwaga oili katika kontena iliyoidhinishwa.
4.
Baada ya oili kumwagwa, weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwaga oili (F,
H, Kielelezo 20).
Ongeza Oili
• Hakikisha injini inadumisha mizani.
• Safisha eneo la kujazia oili kutokana na vifusi vyovyote.
• Tazama Maelezo sehemu ya kiwango cha oili.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 19) na upanguse ukitumia
kitambaa safi.
2.
Injini ina matundu mengi ya kujazia oili. Polepole weka oili kwenye tundu
la kujazia oili ya injini (C, G, Kielelezo 20). Usijaze kupita kiasi. Baada ya
kuongeza oili, subiri dakika moja na kisha ukague kiwango cha oili.
3.
Sakinisha kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 19).
4.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha
oili ni kuwa juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 19) kweny kifaa cha
kupimia kiwango cha mafuta.
5.
Weka tena kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 19).
6.
Unganisha waya ya plagi ya spaki (D, Kielelezo 18) kwenye plagi ya spaki (E).
Badilisha Oili katika Kifaa cha
Upunguzaji
Kifaa cha Upunguzaji Gia kwa Uwiano wa 6:1
Tazama Kielelezo: 21
Iwapo injini yako imewekwa kifaa cha upunguzaji gia kwa uwiano wa 6:1, ifanyie
huduma kama ifuatavyo:
1.
Ondoa kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 21) na kifuniko cha eno la
kiwango cha oili (B).
2.
Ondoa kifuniko cha tundu la kumwagia oili (C, Kielelezo 21) na umwage oili
kwenye kontena inayofaa.
3.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwagia oili (C, Kielelezo 21).
4.
Ili kujaza, mwaga polepole oili ya kulainisha gia (tazama sehemu ya Maelezo)
kwenye tundu la kujazia oili (D, Kielelezo 21). Endelea kumwaga hadi oili ifurike
kwenye shimo la kiwango cha oili (E).
5.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kiwango cha oili (B, Kielelezo 21).
6.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 21).
Kumbuka: Kifuniko cha tundu la kujazia oili (A, Kielelezo 21) kina shimo ndogo la
kupitishia hewa (F) na ni lazima kiwekwe upande wa juu wa kifuniko cha gia kama
ilivyoonyeshwa.
Kifaa cha Upunguzaji Gia kwa Uwiano wa 2:1
Tazama Kielelezo: 22
Ikiwa injini ina kifaa cha upunguzaji nyororo kwa uwiano wa 2:1 (G, Kielelezo 22), basi
hauhitaji kubadilisha oili. Oili katika injini pia inalainisha lifaa cha upunguzaji nyororo.
Kifaa cha Upunguzaji Klachi Oevu kwa Uwiano wa 2:1
Tazama Kielelezo: 23
Iwapo injini yako imewekwa kifaa cha upunguzaji klachi oevu kwa uwiano wa 2:1, ifanyie
huduma kama ifuatavyo:
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 23).
2.
Ondoa kifuniko cha tundu la kumwagia oili (B, Kielelezo 23) na umwage oili
kwenye kontena inayofaa.
3.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwagia oili (B, Kielelezo 23).
4.
Ili kujaza, mwaga polepole oili ya kulainisha gia (tazama sehemu ya Maelezo )
kwenye tundu la kujazia oili (C, Kielelezo 23).
5.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 23).
6.
Ondoa kifaa cha kupima oili (A, Kielelezo 23) na ukague kiwango cha oili. Kiwango
sahihi cha oili ni kuwa juu ya alama inayoashiria oili imejaa (D) kwenye kifaa cha
kupima kiwango cha oili.
7.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 23).
Dumisha Chujio la Hewa
Tazama Kielelezo: 24
Onyo
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
• Usiwashe washa na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa
(iwapo kipo) au chujio la hewa (iwapo lipo) vimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa ili kusafishia chujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu chujio na maji yatayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji ili kujua mahitaji ya huduma.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza sehemu za kufunga (C, Kielelezo 24).
2.
Ondoa kifuniko (A, Kielelezo 24).
3.
Ondoa chujio (B, Kielelezo 24).
4.
Ili kulegeza uchafu, gonga gonga chujio kwa utaratibu (B, Kielelezo 24) kwenye
sehemu ngumu. Ikiwa chujio ni chafu kupita kiasi, badilisha kwa chujio mpya.
5.
Weka chujio (B, Kielelezo 24) .
6.
Weka kifuniko (A, Kielelezo 24) na ukaze sehemu za kukazia (C). Hakikisha
sehemu za kukazia zimekazwa kabisa.
Fanyia huduma Mfumo wa Mfuta
Tazama Kielelezo: 25
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto haraka sana na kulipuka.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au
kifo.
• Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
• Kagua tundu za mafuta, tangi, kifuniko kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha
kama itahitajika.
• Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha mafuta , mimina mafuta kutoka kwa
tangi ya mafuta au au funga vali ya kuzuia mafuta.
• Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo yatavukiza kabla ya kuwasha
injini.
• Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa kwa namna sawa na
sehemu asili.
Chujio Msingi la Mafuta, iwapo lipo
1.
Ondoa kifuniko cha mafuta (A, Kielelezo 25).
2.
Ondoa chujio msingi la mafuta (B, Kielelezo 25).
3.
Iwapo chujio msingi la mafuta ni chafu, lisafishe au ulibadilishe. Ukibadilisha chujio
msingi la mafuta, hakikisha umetumia chujio msingi la mafuta ambalo si ghushi.
Shughulikia Mfumo wa Kupoesha
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa
moto zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi, n.k., unaweza
kushika moto.
• Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
• Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
Notisi
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa fueli.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa na hewa. Uchafu unaweza kuzuia mtiririko wa hewa na
kusababisha injini kuchemka kupita kiasi, na kusababisha utendakazi mbaya na
kupunguza maisha ya injini.
51