Hatua 2: Mafuta
Mapendekezo ya Mafuta Kielelezo
Tunapendekeza matumizi ya mafuta Yaliyoidhinishwa
ya Udhamini wa Briggs & Stratton kwa utendakazi bora
zaidi. Mafuta mengine ya ubora wa juu ya kitakasaji
yanakubalika endapo yameainishwa kuwa ya huduma ya
SF, SG, SH, SJ au juu zaidi. Usitumie viongezi spesheli.
Hali ya joto ya nje ya nyumba huamua mnato na uzito wa
mafuta hayo katika injini husika. Tumia chati kuchagua
mnato bora kwa ajili ya joto la nje linalotarajiwa.
* Chini ya 4°C (40°F) matumizi ya SAE 30 itasababisha ugumu
wakati wa kuwasha.
** Zaidi ya 27°C (80°F) matumizi ya 10W30 yanaweza
kusababisha kuongezeka kwa matumizi ya mafuta. Angalia
kiwango cha mafuta mara nyingi zaidi.
Kuangalia/Kuongeza Mafuta ya Injini Kielelezo
Kiwango cha mafuta kinafaa kukaguliwa kabla ya kila
matumizi au angaa kila baada ya saa 8 za operesheni.
Hakikisha kiwango cha mafuta kinatosha na hakipungui.
1. Hakikisha kuwa jenereta iko juu ya sehemu tambarare
2. Safisha sehemu ya kuwekea mafuta (1,H) na
uondoe kizibo/pima
3. Thibitisha kuwa mafuta yako alama kamili (3,A) kwa
kijiti cha kupimia
4. Kama itahitajika, tia mafuta taratibu kupitia kwenye
sehemu hiyo ya kujazia mafuta hadi kufikia kwenye
alama ya KUJAA kwenye kijiti hicho husika. Usijaze
kupita kiasi.
5. Badilisha na ukaze kifuniko cha sehemu ya kujazia
mafuta/kujiti cha kupimia.
NOTISI Usijaribu kuzungusha au kuwasha injini kabla
ijahudumiwa vizuri na mafuta yaliyopendekezwa. Hii
inaweza kuharibu injini.
TAHADHARI Epuka mgusano wa ngozi wa mara
kwa mara au wa muda mrefu na mafuta ya gari
yaliyotumika na mafuta. Mafuta ya gari
yaliliyotumika yameonekana kusababisha saratani ya
ngozi katika baadhi ya wanyama wa maabara. Safisha
kwa kina maeneo yaliyo na jeraha au wazi kwa sabuni na
maji.
WEKA MBALI KUTOKA KWA WATOTO.
USICHAFUE. LINDA RASILIMALI. RUDISHA
MAFUTA YALIYOTUMIKA KWA VITUO VYA
KUKUSANYA.
Ongeza Mafuta Kielelezo
Lazima mafuta yatimize viwango hivi:
• Safi gasolini ambayo haina madini ya ledi na yenye
kiwango cha oktane kisichopungua 87/87 AKI (91
RON).
• Gasolini yenye kiwango cha hadi 10%cha ethanoli
inakubalika
NOTISI Usichanganye mafuta kwenye petroli
au kubadilisha injini ili iweze kuendeshwa kwa
kutumia mafuta tofauti. Usitumie mafuta ambayo
hayajaidhinishwa kama vile E15 na E85. ARIFA Matumizi
ya mafuta ambayo hayajaidhinishwa yanaweza kuharibu
jenereta na kuharibu udhamini wa mashine haya.
Angalia Mwinuko wa Juu kwa mita 1524 (futi 5000) na juu.
2
1 3
4
ONYO! Mafuta na mivuke yake
yanaweza kuwaka na kulipuka hivyo
yanaweza kuchoma, washa moto au
mlipuko na kusababisha kifo au majeraha makubwa.
Usiongeze mafuta wakati jenereta inatumika. Zimisha
injini na uwache ipoe angalau kwa dakika 2 kabla ya
kuondoa kizibo cha mafuta. Jaza tenki ya mafuta nje.
Usimwage mafuta. Weka mafuta mbali na cheche, moto
ulio wazi, taa ya kujaribia, joto, na vyanzo vingine vya
moto. Angalia mistari ya mafuta, tenki,kofia na sehemu
za kuunganisha mara nyingi kwa nyufa au mtiririko.
Badilisha kama itahitajika. Usiwashe wala kuvuta sigara.
Usimwage maji kwenye jenereta ili kuzimia moto. Tumia
tu kizima moto kilichotengenezwa kuzimia kioevu
kishikacho moto kirahisi na mifumo ya kiumeme kama
kizima moto cha unga. Fuata maagizo yaliyotolewa na
mtengenezaji wa kizima moto kabla ya matumizi.
Jenereta hii haipaswi kutumiwa katika mazingira
yashikayo moto kirahisi.
1. Taratibu ondoa kizibo cha mafuta ili kupunguza
shinikizo kwa tenki.
2. Taratibu ongeza mafuta yasiyo na madini ya ledi (A)
ili kujaza tenki (B). Kuwa mwangalifu usijaze hadi
juu ya ukingo (C). Hii inawacha nafasi ya kutosha
kwa ajili ya upanuzi wa mafuta.
3. Weka kifuniko cha mafuta na uwache mafuta yote
yaliomwagika yayeyuke kabla uwashe injini.
Mwinuko wa Juu
Kwa mwinuko wa zaidi ya mita 1524 (futi 5000)
mafuta yenye kiwango cha chini cha oktane cha 85
kinakubalika/85 AKI (89 RON). Ili kubakia na uzalishaji
unao kubalika, marekebisho ya sehemu za mwinuko
marekebisho yanahitajia. Operesheni bila marekebisho
haya yatasababisha upungufu kwa utekelezaji,
kuongezeka kwa matumizi ya mafuta, na kuongezeka kwa
uzalishaji wa uchafu.
Sema na muuzaji wa Briggs & Stratton aliyeidhinishwa
kwa maelezo zaidi kuhusu marekebisho ya miinuko ya
juu. Operesheni ya injini katika sehemu za milimani zilizo
chini ya mita 762 m (futi 2500) pamoja na mkoba wa
sehemu za milima ya juu haipendekezwi.
Kusafirisha
Unaposafirisha kifaa kwa gari au trela,zungusha valvu
ya kufunga mafuta hadi sehemu ya OFF (0) Usiweke
injini au mitambo katika hali ambayo itasababisha mafuta
kumwagika.
Kusafisha
Kila siku au kabla ya kutumia, anagalia karibu na chini
ya jenereta kwa ishara ya uvujaji wa mafuta. Safisha
uchafu wowote ambao umekusanyika. Weka sehemu
inayozunguka kifaa cha kunyamazisha eksozi huru
kutokana na uchafu.
• Tumia brashi laini ili kulegeza uchafu an mafuta
ambayo yamekauka.
• Tumia kitambaa baridi kupanguza ili kusafisha
sehemu za nje
NOTISI Usiingize kifaa chochote kwenye mashimo ya
kufanya injini kuwa baridi.
5