Briggs & Stratton 130000 Manual Del Operario página 45

Ocultar thumbs Ver también para 130000:
Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 15
2.
Ondoa kiziba cha kutoa mafuta (F, Kielelezo 13). Weka mafuta kwenye kontena
iliyoidhinishwa.
Kumbuka: Viziba cheche mbalimbali vya kutoa mafuta (G, Kielelezo 13) vinatumika.
3.
Baada ya mafuta kutolewa, sakinisha na ukaze kiziba cha kutoa mafuta (F,
Kielelezo 13).
Ongeza Mafuta
• Hakikisha kuwa mtambo uko katika kiwango.
• Safisha eneo la kujaza mafuta kutokana na uchafu wowote.
• Tazama Vipimo katika eneo la kiwango cha mafuta.
Kifaa Kifupi cha Kuangalia Mafuta, iwapo kipo
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 13) na upanguse
kwa kitambaa safi.
2.
Polepole weka mafuta kwenye eneo la kuweka mafuta la injini (C, Kielelezo 13).
Jaza hadi sehemu ya kufurika.
Sakinisha kifaa cha kupima mafuta (A, Kielelezo 13). Usigeuze au kukaza.
3.
Ondoa na uangalie kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha mafuta kiko juu ya
kiashiria kilichojaa (B) kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta.
4.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo
13).
5.
Unganisha waya wa kuziba cheche (D, Kielezo 12) kwenye kuziba cheche (E).
Kifaa kipana cha kuangalia mafuta, iwapo kipo
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 14) na upanguse
kwa kitambaa safi.
2.
Polepole weka mafuta kwenye eneo la kuweka mafuta la injini (C, Kielelezo 14).
Usijaze kupita kiasi. Baada ya kuongeza mafuta, subiri dakika moja (1) na kisha
angalia kiwango cha mafuta.
3.
Sakinisha na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 14).
4.
Ondoa na uangalie kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha mafuta kiko juu ya
kiashiria kilichojaa kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (B, Kielelezo
14) kwenye kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta.
5.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo
14).
6.
Unganisha waya wa kuziba cheche (D, Kielezo 12) kwenye kuziba cheche (E).
Shughulikia Kichuja Hewa
Tazama Kelelezo: 15, 16, 17
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
• Kamwe usiwashe na kuendesha wakati uunganishaji wa kisafisha hewa (iwapo
kipo) au kichuja hewa (iwapo kipo) kimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au majimaji yaliyoshinikizwa kusafisha kichujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu kichujio na majimaji yatayeyusha kichujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji wa mahitaji ya huduma.
Modeli mbalimbali aidha zinatumia povu au kichujio cha karatasi. Baadhi ya modeli pia
zina kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa tena.
Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako na
ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza bizimu (A, Kielelezo 15).
2.
Ondoa kifuniko (B, Kielelezo 15).
3.
Ondoa bizimu (E, Kielelezo 15).
4.
Ili kuzuia uchafu kutokana na kuanguka ndani kabureta, kwa umakini ondoa
kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 15) na kichujio cha (C) kutoka katika eneo la
kuchujia hewa (F).
5.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio katika eneo gumu, (C, Kielelezo
15) Iwapo kichujio ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
6.
Ondoa kichujio cha mwanzo kutoka kwenye kichujio (C), (D, Kielelezo 15).
7.
Osha kisafishaji cha mwazo kwenye sabuni oevu na maji, (D, Kielelezo 15).
Ruhusu kisafishaji cha mwanzo kukauka kabisa. Usiweke mafuta kwenye
kisafishaji cha mwanzo.
8.
Kusanya kisafishaji cha mwanzo kilichokauka kwenye kichujio (C), (D, Kielelezo
15).
9.
Sakinisha kichujio (C, Kielezo 15) na kisafishaji (D) cha mwanzo katika eneo la
kichujio cha hewa (F) na kwenye kitufe (G). Hakikisha kichujio kimeunganishwa
sahihi kwenye eneo la kichujio cha hewa na kulinda kwa bizimu (E).
10.
Sakinisha jalada (B, Kielelezo 15) na ulinde kwa bizimu(s) (A). Hakikisha bizimu
imekazwa.
Kichujio cha Povu ya Hewa
1.
Legeza bizimu (D, Kielelezo 16) inayoshikilia kifuniko (A).
2.
Ondoa kifuniko (D, Kielelezo 16), kishikiliaji (C), na kichujio (B).
3.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio (B, Kielelezo 16) kwenye eneo
gumu. Iwapo kichujio ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
4.
Sakinisha kishikiliaji (C, Kielelezo 16) kwenye kichujio (B).
5.
Weka jalada (A, Kielelezo 16) na ulinde kwa bizimu (D). Hakikisha bizimu
imekazwa.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza bizimu (D, Kielelezo 17).
2.
Ondoa kifuniko (A, Kielelezo 17).
3.
Ondoa kisafisha awali (C, Kielelezo 17), iwapo kipo, na kichujio (B).
4.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio (B, Kielelezo 17) kwenye eneo
gumu. Iwapo kichujio ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
5.
Osha kisafishaji cha mwanzo (C, Kielelezo 17), iwapo kipo, kwenye sabuni oevu
na maji. Ruhusu kisafishaji cha mwanzo kukauka kabisa. Usiweke mafuta
kwenye kisafishaji cha mwanzo.
6.
Weka kisafishaji kavu cha awali (C, Kielelezo 17), wapo kipo, na kichujio (B) .
7.
Weka jalada (A, Kielelezo 17) na ulinde kwa bizimu (D). Hakikisha bizimu
imekazwa.
Badilisha Mafuta ya Kupunguza Gia
Tazama Kelelezo: 18, 19
Upunguzaji Gia wa 6:1 (Kielelezo 18)
Iwapo injini yako imewekwa kitengo cha upunguzaji gia wa 6:1, ihudumie kama
ifuatavyo:
1.
Ondoa plagi ya kujaza mafuta (A, Kielelezo 18) na plagi ya kiwango cha mafuta
(B).
2.
Ondoa plagi ya kukamua mafuta (C, Kielelezo 18) na ukamue mafuta kwenye
kontena inayofaa.
3.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo
18).
4.
Ili kujaza upya, mwaga polepole mafuta ya kulainisha gia (tazama sehenu ya
Vipimo kwenye shimo la kujaza mafuta (D, Kielelezo 18). Endelea kumwaga hadi
mafuta yafurike kwenye shimo la kiwango cha mafuta (E).
5.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo
18).
6.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo
18).
Kumbuka: Plagi ya kujaza mafuta (A, Kielelezo 18) ina shimo la tundu (F) na lazima
isakinishwe upande wa juu wa kifuniko gia kama ilivyoonyeshwa.
Upunguzaji Gia wa 2:1 (Kielelezo 19)
Kitengo cha upunguzaji gia wa 2:1 (G, Kielelezo 19) hakihitaji kubadilishwa mafuta.
Shughulikia Mfumo wa Fueli
Tazama Kielelezo: 20, 21
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
• Hifadhi fueli mbali na cheche, miale iliyo wazi, taa za mwongozo, heat na vyanzo
vingine vya uwakaji.
• Angalia tundu, tangi, kifuniko na kurekebisha mara kwa mara kwa nyufa na uvujaji.
Badilisha ikiwezekana.
• Kabla ya kusafisha ua kubadilisha kichujio cha fueli, ondoa fueli au funga vali ya
kufunga fueli.
45

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido