•
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
•
Usibadilishe na springi ya kidhibiti, viungo, au viungo vingine ili kuongeza kasi ya
injini.
•
Usigonge gurudumu la kuongeza kasi ya injini kwa nyundo au kifaa kigumu.
Inaweza kufanya gurudumu la kuongeza kasi ya injini kuvunjika wakati wa
kuendesha.
•
Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo
sawa kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zinaweza kuharibu kifaa au
kusababisha majeraha.
Unapohamisha kifaa hadi eneo nyingine
•
Hakikisha tangi la mafuta ni TUPU au vali ya kufungia ipo katika eneo la
kuonyesha IMEFUNGWA.
Wakati wa kuhifadhi mafuta au kifaa kikiwa na mafuta kwenye tangi la mafuta
•
Kwa sababu taa za moto au vyanzo vingine vya mwako vinaweza kusababisha
milipuko, hifadhi mafuta au kifaa mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji,
au vifaa vingine ambavyo vina taa za moto.
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Kuwasha injini kunasababisha mwako ambao unaweza kusababisha moto ay
mlipuko.
•
Iwapo kuna gesi asili au ya LP iliyovuja katika eneo hilo, usiwashe injini.
•
Kwa sababu mvuke unaweza kuwaka moto, usitumie firigiji zilizoshinikizwa za
kuwasha.
ONYO
HATARI YA GESI YENYE SUMU. Eksozi ya injini ina kaboni monoksidi, gesi ya
sumu ambayo inaweza kukuua kwa dakika chache. Ingawa hauwezi kunusa
mafukizo yanayotolewa, bado unaweza kuvuta gesi hatari ya monoksidi ya
kaboni. Ukihisi mgonjwa, kizunguzungu, au mchovu unapotumia bidhaa hii,
nenda kwenye eneo lenye hewa safi MARA MOJA. Mwone daktari. Huenda ukawa
umeathiriwa na sumu ya kaboni monoksidi.
•
Gesi ya kaboni monoksidi inaweza kujikusanya katika maeneno yenye watu. Ili
kupunguza hatari ya gesi ya kaboni monoksidi, tumia bidhaa hii TU nje na mbali
na madirisha, milango na matundu.
•
Sakinisha ving'ora vya kutambua uwepo wa kaboni monoksidi vinavyotumia betri
pamoja na hifadhi ya betri kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji.
Ving'ora vya moshi haviwezi kutambua gesi ya kaboni monoksidi.
•
USIENDESHEE bidhaa hii ndani ya nyumba, gereji, vyumba vya chini ya ardhi,
ubati, vibanda, au majengo mengine yaliyobanwa hata kama unatumia viyoyozi
ama kufungua milango na madirisha ili hewa safi iingie. Baada ya kuendesha
bidhaa hii, gesi ya kaboni monoksidi inaweza kukusanyika kwa haraka katika
maeneo haya na inaweza kukwama kwa saa kadhaa.
•
KILA WAKATI weka bidhaa hii upande ambao upepo unaelekea na uelekeze
ekzosi ya injini mbali na maeneo yenye watu.
ONYO
Uvutaji nyuma wa haraka wa kamba ya kianzishaji (kuvuta nyuma kwa haraka)
kutavuta mkono wako kuelekea kwenye injini haraka kuliko unavyoweza kuachilia.
Kunaweza kusababisha mifupa kuvunjika, michubuko amu maungo kuteguka.
•
Ili kuzuia kuvuta nyuma kwa haraka wakati wa kuwasha injini, vuta kamba ya
kianzishaji polepole hadi uhisi upinzani na kisha uvute haraka.
•
kabla ya kuwasha injini, ondoa vifaa vyote vya nje/mizigo yote ya injini.
•
Hakikisha kwamba vijenzi vya kifaa kilichounganishwa moja kwa moja kama
vile, lakini sio tu, bapa, mashine ya kusogeza majimaji, makapi, na proketi,
vimeambatishwe salama.
ONYO
Sehemu zinazozunguka zinaweza kunasa mikono, miguu, nywele, nguo, au
vifuasi na kupelekea kukatwa viungo au ngozi vibaya.
•
Endesha kifaa vilinzi vikiwa vimesakinishwa vizuri.
•
Weka mikono na miguu mbali na sehemu zinazozunguka.
•
Vua vipuli na uhakikishe kwamba nywele ndefu ziko mbali na sehemu
zinazozunguka.
•
Usivae nguo zilizolegea au vipengee vinavyoweza kushikwa.
ONYO
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Vitu vinavyoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi, vinaweza kushika
moto.
•
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
•
Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442, kutumia
au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa na brashi, au
lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama ilivyobainishwa katika
sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya kufanya kazi. Mamlaka nyingine
za majimbo au serikali ya kitaifa huenda zikawa na sheria sawia; Rejelea Kanuni za
Serikali ya KItaifa ya 36 CFR Sehemu ya 261.52. Wasiliana na mtengenezaji asilia wa
kifaa, muuzaji rejareja, au muuzaji ili kupata kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya
mfumo wa ekzosi uliowekwa kwenye injini hii.
ONYO
Mwako wa injini usiokusudiwa unaweza kusababisha mshutuko wa umeme au
moto na kupelekea kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha
mabaya ya ukataji wa ngozi.
Kabla ya kufanya marekebisho au ukarabati:
•
Tenganisha waya wa plagi ya spaki na uuweke mbali na plagi ya spaki.
•
Tenganisha betri katika kichwa cha hasi (injini tu zenye kianzishaji cha umeme.)
•
Tumia zana sahihi pekee.
Unapokagua uwepo wa cheche:
•
Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki.
•
Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa imeondolewa.
ONYO
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Ukinusa gesi
•
Usiwashe injini.
•
Usiwashe swichi za kiumeme.
•
Usitumie simu katika eneo hilo.
•
Ondoka kwenye eneo hilo.
•
Wasiliana na muuzaji gesi hiyo au idara ya wazima moto.
Vipengele na Vidhibiti
Vidhibiti vya Injini
Linganisha herufi zilizowekea Vielelezo 1, 2, 3, 4, 5 na vidhibiti vya injini katika orodha
ifuatayo.
A.
Nambari Tambulishi za Injini Muundo - Aina - Msimbo
B.
Plagi ya Spaki
C. Kishikio cha Kamba ya Kianzishaji
D. Tangi na Kifuniko cha Mafuta
E.
Kisafishaji Hewa
F.
Kifaa cha Kupima Oili
G. Kifuniko cha Tundu la Kumwaga Oili
H. Mafla, Kilinda Mafla (iwapo kipo), Kishika Spaki (iwapo kipo)
I.
Kidhibiti Injini (iwapo kipo)
J.
Chujio la Mafuta (iwapo lipo)
K.
Grili ya Kuingiza Hewa
L.
Vali ya Kufungia Mafuta (iwapo ipo)
M. Chujio la Oili (iwapo lipo)
N. Swichi ya Kuzima (iwapo ipo)
O. Choki (iwapo ipo)
Ishara za Kudhibiti Injini na Maana
Kasi ya Injini - HARAKA
Kasi ya Injini - POLEPOLE
49