Ondoa Oili
1.
Injini ikiwa imezimwa lakini ina joto, tenganisha waya wa plagi ya spaki (D,
Kielelezo 12) na uiweke mbali na plagi ya/za spaki (E).
2.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 13).
3.
Ondoa kifuniko cha tundu la kumwaga oili (F, Kielelezo 14). Mwaga oili katika
kontena iliyoidhinishwa.
KUMBUKA: Mojawapo wa vifuniko vya matundu ya kumwaga oili kinaweza kuwa
kwenye injini.
4.
Baada ya oili kumwagwa, weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwaga oili (F,
Kielelezo 14).
5.
Wakati unamwaga oili kutoka kwenye mrija wa kujazia oili wa upande wa juu (C,
Kielelezo 15), weka upande wa injini ulio na plagi ya spaki (E) ukiwa umeangalia
juu. Mwaga oili katika kontena iliyoidhinishwa.
ONYO
Unapomwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la mafuta
liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kupelekea moto au mlipuko.
Endesha injini hadi isimame kwa kukosa mafuta.
Badilisha Chujio la Oili, iwapo lipo
1.
Mwaga oili kutoka kwenye injini. Rejelea sehemu ya Kuondoa Oili.
2.
Ondoa chujio la oili (G, Kielelezo 16) na ulitupe vizuri.
3.
Kabla ya kuweka chujio jipya la oili, lainisha kiasi gasketi ya chujio la oili
ukitumia oili safi.
4.
Weka chujio la oili ukitumia mkono hadi gasketi iguse adapta ya chujio la oili, kisha
ukaze chujio la oili kwa mizunguko ya 1/2 hadi 3/4.
5.
Ongeza oili. Rejelea sehemu ya Kuongeza Oili.
6.
Washa na uendeshe injini. Injini inapochemka, kagua kama kuna uvujaji wa oili.
7.
Zima injini. Hakikisha kwamba kiwango cha oili kiko juu ya alama inayoashiria
kujaa kwenye kifaa cha kupima kiwango cha oili. Rejelea Kukagua na Kuongeza
Oili.
Ongeza Oili
•
Hakikisha injini inadumisha mizani.
•
Safisha vifusi vyote kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
•
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 6). Futa oili kwenye kifaa
cha kupima kiwango cha oili ukitumia kitambaa safi.
2.
Polepole weka oili kwenye tundu la kujazia oili ya injini (C, Kielelezo 6). Usijaze
kupita kiasi. Subiri dakika moja, na kisha ukague kiwango cha oili.
3.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 6).
4.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili
kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 6) kwenye kifaa cha kupima
kiwango cha oili.
5.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 6).
6.
Unganisha waya wa plagi ya spaki kwenye plagi ya/za spaki. Tazama sehemu
ya Kuondoa Oili.
Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa
ONYO
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
•
Usiwashe na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa (iwapo
kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) kimeondolewa.
NOTISI
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa iliyoshinikizwa inaweza
kuharibu chujio na vioevu vitayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji ili kujua mahitaji ya huduma.
Miundo tofauti itatumia vichujio vya sifongo au karatasi. Baadhi ya miundo pia iinaweza
kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa
tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako
na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Povu la Hewa
1.
Legeza au uondoe vifaa vya kufunga (A, Kielelezo 17), iwapo vipo.
2.
Fungua au uondoe kifuniko (B, Kielelezo 17).
3.
Kwa uangalifu ondoa elementi ya povu (C, Kielelezo 17) kutoka kwenye sehemu ya
chini ya chujio la hewa.
4.
Osha elementi ya povu (C, Kielelezo 17) kwenye sabuni oevu na maji. Finya
elementi ya povu ukitumia mikono yako ndani ya kitambaa kavu ili ikauke.
5.
Tumbukiza elementi ya povu (C, Kielelezo 17) ndani ya oili safi ya injini. Ili kuondoa
oili ya injini isiyohitajika kwenye elementi ya povu, ifinye ukitumia mikono yako
ndani ya kitambaa kavu.
6.
Sakinisha elementi ya povu (C, Kielelezo 17) kwenye sehemu ya chini ya chujio la
hewa.
7.
Funga au weka kifuniko (B, Kielelezo 17) na ufunge vizuri ukitumia
bizimu. Hakikisha kwamba umekaza vizuri.
Chujio la Hewa la Karatasi
1.
Legeza au uondoe vifaa vya kufunga, iwapo zipo, (A, Kielelezo 18).
2.
Fungua au uondoe kifuniko (B, Kielelezo 18).
3.
Ili kuzia uchafu unaoanguka kwenye kabureta, kwa makini ondoa kishajishai cha
mwanzo (D, Kielelezo 18) na chujio (C) kutoka kwenye eneo la chini la chujio la
hewa.
4.
Ondoa kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 18), ikiwa kipo, kwenye chujio (C).
5.
Ili kulegeza vifusi, gongesha chujio (C, Kielelezo 18) kwa utaratibu kwenye eneo
gumu. Ikiwa chujio ni chafu sana, badilisha kwa chujio jipya.
6.
Osha kisafishaji cha mwazo (D, Kielelezo 18), ikiwa kipo, kwenye sabuni oevu na
maji. Acha kisafishaji cha mwanzo kikauke kabisa. Usiongeze oili kwenye kisafishaji
cha mwanzo.
7.
Weka pamoja kisafishaji cha mwanzo (D, Kielelezo 18) kilichokauka, ikiwa kipo,
kwenye chujio (C).
8.
Sakinisha chujio (C, Kielelezo 18) na kisafishaji (D) la mwanzo kwenye sehemu ya
chini ya chujio la hewa. Hakikisha chujio linatoshea vizuri katika sehemu ya chini ya
chujio cha hewa.
9.
Funga au sakinisha kifuniko (B, Kielelezo 18) na ufunge vizuri ukitumia bizimu (A).
Hakikisha kwamba sehemu za kukazia zimekazwa kabisa.
Kufanyia Huduma Mfumo wa Mafuta
ONYO
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
•
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
•
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
•
Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha mafuta, mwaga mafuta kutoka
kwa tangi ya mafuta au funga vali ya kufungia mafuta.
•
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
•
Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo
sawa kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zinaweza kuharibu kifaa au
kusababisha majeraha.
Chujio la Mafuta, iwapo lipo
1.
Kabla ya kusafisha au kubadilisha chujio la mafuta (A, Kielelezo 19), mwaga mafuta
kutoka kwenye tangi ya mafuta au funga vali ya kufunga mafuta. Ikiwa tangi la
mafuta si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
2.
Tumia koleo kufinya vichupo (B, Kielelezo 19) kwenye vibanio (C), kisha ondoa
vibanio kutoka kwenye chujio la mafuta (A). Zungusha na uvute njia za mfuta (D)
kutoka kwenye kichujio cha mafuta.
3.
Kagua mirija ya mafuta (D, Kielelezo 19) kama kuna nyufa au uvujaji. Badilisha
kama itahitajika.
4.
Badilisha chujio la mafuta (A, Kielelezo 19) kwa chujio asili la kifaa.
5.
Funga mirija ya mafuta (D, Kielelezo 19) kwa kutumia vibanio (C).
Kufanyia Huduma Mfumo wa Kupoesha
ONYO
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Uchafu unaoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi na brashi, vinaweza
kushika moto.
•
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
•
Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
53