Udumishaji
Ratiba ya Udumishaji
Fuata mpishano wa saa au kalenda, yoyote ile
inayotangulia. Huduma ya mara kwa mara zaidi
inahitajika wakati unapoendesha kwenye hali mbaya
zaidi. Mita ya saa (A) inaonyesha na kurekodi saa
ambazo jenereta yako imeguruma (hadi 9,999.9).
Saa 5 za Kwanza
• Badilisha oili ya injini
Kila Baada ya Saa 25 au Kila Mwaka
• Safisha chujio la hewa la injini
Kila Baada ya Saa 50 au Kila Mwaka
• Badilisha oili ya injini
Kila Mwaka
• Badilisha chujio la hewa la injini
• Hudumia vali ya mafuta
• Hudumia plagi ya spaki
• Kagua mafla na kishika cheche
• Safisha mfumo wa kupoesha
Fanya huduma mara nyingi zaidi katika hali chafu au zenye vumbi.
Mapendekezo Jumla
Udumishaji wa mara kwa mara utaboresha utendakazi
na kuongezea maisha ya jenereta ya nje. Mwone
Muuzaji Huduma Yeyote Aliyeidhinishwa wa Briggs &
Stratton ili kufanyiwa udumishaji na huduma. Uwekaji
sehemu na kazi kubwa ya ukarabati ni lazima zifanywe
na wafanyikazi wenye mafunzo maalum.
Huduma na marekebisho yote yanafaa kufanywa
angalau mara moja kila msimu. Plagi mpya za spaki na
chujio safi la hewa zinahakikisha mchanganyiko mzuri
wa hewa na mafuta ili kusaidia injini yako kuendeshwa
vyema na pia kudumu kwa muda mrefu zaidi. Fuata
mahitaji katika Ratiba ya Udumishaji.
ONYO! Ili kuhakikisha usalama wa mashine,
tumia tu sehemu asilia kutoka kwa mtengenezaji
au kuidhinishwa na mtengenezaji. Ukiwa na
maswali kuhusu kubadilisha vijenzi kwenye jenereta
yako, tafadhali tutembelee kwenye tovuti yetu
BRIGGSandSTRATTON.COM.
TAHADHARI Kasi za juu au chini zaidi kupita kasi
zinaweza kusababisha majeraha madogo.
Usichokore springi ya gavana, viungo au sehemu
nyingine ili kubadilisha kasi. Usifanye mabadiliko kwenye
jenereta kwa njia yoyote ile.
8
Kielelezo
1
1
1
1
1
Uhifadhi
Ikiwa unahifadhi kifaa hiki kwa zaidi ya siku 30, tumia
miongozo ifuatayo ili kukiandaa kwa uhifadhi.
Maagizo ya Uhifadhi wa Muda Mrefu
Mafuta yanaweza kuharibika yakihifadhiwa kwa zaidi ya
siku 30. Mafuta yaliyoharibika yanaweza kusababisha
mabaki ya asidi na gundi kutengenezeka kwenye mfumo
wa mafuta au kwenye sehemu muhimu za kabureta. Ili
uweke mafuta yakiwa sawa, tumia Briggs & Stratton®
Advanced Formula Fuel Treatment & Stabilizer,
inayopatikana mahali popote ambapo sehemu halisi za
huduma zinauzwa.
Hakuna haja ya kumwaga petroli kutoka kwenye injini
ikiwa kiimarishaji mafuta kimeongezwa kulingana
na maagizo. Washa injini ikiwa nje kwa dakika 2
kuzungusha kiimarishaji katika mfumo wote wa mafuta
kabla ya kukiweka.
Ikiwa petroli kwenye injini haijatibiwa kwa kiimarishaji
mafuta, ni lazima imwagwe kwenye kontena
iliyoidhinishwa. Endesha injini ikiwa nje hadi isimame
kutokana na ukosefu wa mafuta. Matumizi ya kiimarishaji
mafuta kwenye kontena ya uhifadhi yanapendekezwa ili
kudumisha usafi.
ONYO! Mafuta na mivuke yake
yanaweza kuwaka moto na kulipuka na
kusababisha kuchomeka, moto au
mlipuko na kupelekea kifo au majeraha mabaya.
Unapohifadhi mafuta au kifaa chenye mafuta kwenye
tangi, hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia
maji, vifaa vya kukausha nguo au vitu vingine ambavyo
vina taa za moto au vyanzo vya mwako kwa sababu
vinaweza kuwasha moto kwenye mivuke ya mafuta.
Unapomwaga mafuta, zima injini na uwache injini ipoe
kwa angalau dakika 2 kabla ya kuondoa kifuniko cha
mafuta. Legeza kifuniko hicho polepole ili kutoa shinikizo
kwenye tangi. Mwanga mafuta ukiwa nje ya nyumba.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi,
joto, na vyanzo vingine vya mwako. Kagua tundu, tangi,
kifuniko kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha kama
itahitajika.
Vidokezo Vingine vya Kuhifadhi
1. Safisha jenereta kama ilivyoainishwa kwa Kusafisha.
2. Weka chaja ndani ya eneo la kuchajia betri na plagi ya
volti 230 za AC.
ILANI Chaja haitachaji betri wakati inatumika kwa muda
mrefu zaidi.
ONYO! Fifuniko vya uhifadhi vinaweza
kusababisha moto na hatimaye kifo au majeraha
mabaya. Usiweke kifuniko cha hifadhi juu ya
jenereta iliyo moto.Wacha vifaa vipoe kwa muda wa
kutosha kabla ya kuweka kifuniko juu yake.
BRIGGSandSTRATTON.COM