Briggs & Stratton 030722-00 Manual Del Usuario página 52

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 18
Briggs & Stratton inatoa hakikisho kwamba, wakati wa kipindi cha hakikisho kilichobainishwa hapa chini, itafanyia ukarabati au kubadilisha, bila malipo, sehemu
yoyote ambayo ina matatizo katika nyenzo au ufanyakazi au yote mawili. Gharama za usafirishaji bidhaa zilizowasilishwa ili kufanyiwa ukarabati au kubadilishwa chini
ya hakikisho hili ni lazima zigharimiwe na mnunuzi. Hakikisho hili linatumika na liko chini ya vipindi vya muda na masharti yaliyoelezwa hapa chini. Ili kupata huduma
ya hakikisho, tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa katika ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM. Ni lazima mnunuzi awasiliane na
Muuzaji HudumaAliyeidhinishwa, na kisha apeleke bidhaa kwa Muuzaji Huduma huyo Aliyeidhinishwaili kufanyiwa ukaguzi na majaribio.
Hakuna hakikisho lingine la haraka. Hakikisho zilizoashiriwa, ikiwa ni pamoja na lile wa uuzaji na uzima kwa ajili ya dhumuni fulani, zina kipimo cha
kipindi cha hakikisho kilichoorodheshwa hapa chini, au kwa kiasi kilichoruhusiwa na sheria. Dhima ya uharibifu wa kimatukio au unaotokana na jambo
jingine haijajumuishwa kwa kiasi kinachoruhusiwa na sheria. Baadhi ya majimbo au nchi haziruhusu vipindi vya hakikisho kuwekewa vipimo, na baadhi ya
majimbo au nchi haziruhusu kutojumuishwa au kipimo cha uharibifu wa kimatukio au unaotokana na jambo jingine, kwa hivyo kipimo na kutojumuishwa huku huenda
hakukuhusu wewe. Hakikisho hili linakupa haki maalum za kisheria na pia huenda ukawa una haki nyingine ambazo zinatofautiana kutoka jimbo moja hadi jingine au
nchi moja hadi nyingine.**
▲ Baada ya miezi 24, hakikisho linasimamia sehemu pekee.
* Inahusu tu injini za Briggs & Stratton pekee. Hakikisho la kusimamia injini zisizo za Briggs & Stratton linatolewa na mtengenezaji wa injini hizo. Vipengee vinavyohusiana
na utoaji mafukizo vinasimamiwa na Kauli ya Hakikisho la Utoaji Mafukizo.
** Nchini Australia - Bidhaa zetu huja na hakikisho ambazo haziwezi kutojumuishwa chini ya Sheria ya Mtumiaji ya Australia. Una haki ya kubadilishiwa au kurudishiwa
pesa kwa hitilafu kuu au fidia kwa uharibifu au hasara nyingine yoyote ya siku za usoni. Pia una haki ya bidhaa kufanyiwa ukarabati au kubadilishwa endapo bidhaa
hazitakuwa za ubora unaokubaliwa na hitilafu haimaanishi kuharibika kwa njia kubwa. Ili kupata huduma ya hakikisho, tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu
zaidi nawe kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM, au kwa kupiga simu kwa nambari 1300 274 447, au kwa kutuma barua pepe
kwa salesenquiries@briggsandstratton.com. au, au utume barua kwa Briggs & Stratton Australia PtyLtd, 1 Moorebank Avenue, Moorebank, NSW, Australia, 2170.
Kipindi cha hakikisho kinaanzia tarehe ya ununuzi wamtumiaji wa kwanza wa rejareja au wa kibiashara. "Matumizi ya kibinafsi" inamaanisha matumizi ya kibinafsi ya
nyumbani ya mtumiaji wa rejareja. "Matumizi ya kibiashara" inamaanisha matumizi mengine yote, yakijumuisha matumizi kwa madhumuni ya kibiashara, ya kuzalisha
mapato au ya kukodisha. Mara tu bidhaa inapopitia matumizi ya kibiashara, baada ya hapo itazingatiwa kuwa bidhaa ya matumizi ya kibiashara kwa ajili ya hakikisho hili.
Ili kuhakikisha hakikisho inasimamia kikamilifu na kwa muda unaofaa, sajili bidhaa yako kwenye tovuti iliyoonyeshwa hapa juu au kwenye www.onlineproductregistration.
com.
Hifadhi risiti yako ya ushahidi wa ununuzi. Ukikosa kutoa ushahidi wa tarehe ya kwanza ya ununuzi wakati huduma ya hakikisho inapoombwa, tarehe ya utengenezaji wa
bidhaa itatumiwa kung'amua kipindi cha hakikisho. Usajili wa bidhaa hauhitajiki ili kupata huduma ya hakikisho kwa bidhaa za Briggs & Stratton.
Huduma ya hakikisho inapatikana tu kupitia Wauzaji Huduma Walioidhinishwa wa Briggs & Stratton. Hakikisho hili linasimamia tu kasoro kwenye nyenzo au ufanyikazi.
Halisimamii hasara iliyosababishwa na matumizi yasiyofaa au mabaya, udumishaji au urekebishaji mbaya, kuchakaa na kuchanika kwa kawaida, au mafuta yaliyoharibika
au ambayo hayajaidhinishwa.
Matumizi Yasiyofaa na Mabaya - Matumizi sahihi na yanayokusudiwa bidhaa hii yameelezwa katika Mwongozo wa Mwendeshaji. Kutumia bidhaa kwa njia ambayo
haijaelezwa katika Mwongozo wa Mwendeshaji au kutumia bidhaa baada ya kuharibika hakutasimamiwa na hakikisho hili. Hakikisho pia halitasimamia chochote ikiwa pia
nambari ya utambulisho iliyo kwenye bidhaa imeondolewa au bidhaa imehitilafiwa au kubadilishwa kwa njia yoyote, au ikiwa bidhaa ina dalili ya matumizi mabaya kama
vile uharibifu wa kugongwa au uharibifu wa maji/kemikali.
Udumishaji au Ukarabati Usiofaa - Bidhaa hii ni lazima idumishwe kulingana na taratibu naratiba zilizotolewa katika Mwongozo wa Mwendeshaji, na kufanyiwa
huduma au ukarabati kwa kutumia sehemu halisi za Briggs & Stratton au za ubora sawia. Uharibifu unaosababishwa na ukosefu wa udumishaji au matumizi ya sehemu
zisizo halisi hausimamiwi na hakikisho.
Kuchakaa na Kuchanika kwa Kawaida - Kama tu mitambo mingi, kifaa chako kinaweza kuchakaa na kuchanika hata kinapodumishwa ipasavyo. Hakikisho hili
halisimamii ukarabati wakati matumizi ya kawaida yamemaliza kabisa muda wa sehemu ya kifaa au kifaa kizima. Vipengee vya udumishaji na kuchakaa kama vile chujio,
mikanda, visu vya kukatia, na pedi za breki (isipokuwa pedi za breki ya injini) havijasimamiwa na hakikisho hili kwa ajili ya hali yake ya kuchakaa vyenyewe, isipokuwa
chanzo kiwe ni kwa ajili ya kasoro kwenye nyenzo au ufanyakazi.
Mafuta Yaliyoharibika au Hayajaidhinishwa - Ili kufanya kazi vizuri, bidhaa hii inahitaji mafuta safi ambayo yanaambatana na vigezo vilivyobainishwa kwenye
Mwongozo wa Mwendeshaji. Uharibifu wa Injini au vifaa unaosababishwa na mafuta yaliyoharibika au matumizi ya mafuta ambayo hayajaidhinishwa (kama vile
mchanganyiko wa ethanol za E15 au E85) haujasimamiwa na hakikisho hili.
Mambo ambayo Hayasimamiwi - Hakikisho hili halijumuishi uharibifu kutokana na ajali, matumizi mabaya, marekebisho, kuhitilafiana, ufanyaji huduma mbaya,
kugandisha au kuzorota kutokana na kemikali. Viambatanishi au vikorokoro ambavyo havikupakiwa asili na bidhaa hii pia havisimamiwi. Hakuna hakikisho kwenye vifaa
vinavyotumiwa kwa nishati msingi badala ya nishati ya matumizi au kwenye kifaa kinachotumika katika shughuli za kuokoa maisha. Hakikisho hili halijumuishi vifaa au
injini zilizotumika, zilizowekwa upya, zilizotumika hapo awali, au za maonyesho. Hakikisho hili pia halisimamii matendo kwa nguvu za Mungu na nguvu nyingine zinazozidi
udhibiti wa mtengenezaji.
10
SERA YA HAKIKISHO LA BIDHAA ZA BRIGGS & STRATTON
HAKIKISHO LENYE KIPIMO
KIPINDI CHA HAKIKISHO
Kipengee
Matumizi ya Kibinafsi
Kifaa
Miezi 36 ▲
Injini*
Miezi 24
Betri (ikiwa ipo)
Miezi 3
KUHUSU HAKIKISHO LAKO
Matumizi ya Kibiashara
Miezi 12
Miezi 12
Hamna
BRIGGSandSTRATTON.COM
80011056_SW Rev A

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

8500ea

Tabla de contenido