Descargar Imprimir esta página

Vanguard 25E300 Manual Del Operador página 45

Ocultar thumbs Ver también para 25E300:

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 20
5.
Ondoa kifaa cha kusonga au kishika cheche, iwapo kipo, na ukague kama kuna
uharibifu au uzuiaji wa kaboni. Hakikisha kwamba unasafisha au kusakinisha vipuri
kabla ya kuendesha kifaa.
6.
Ikiwa yapo, hakikisha mapezi ya kupoesha oili ni safi.
Badilisha Oili ya Injini
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la
mafuta liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto
au mlipuko.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Oili iliyotumika ni bidhaa taka na hatari na ni lazima itupwe kwa njia sahihi. Usitupe
pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha huduma
au muuzaji ili kupata zana salama za kutupa au kutumia tena.
Ondoa Oili
1.
Injini ikiwa IMEZIMWA lakini bado ina joto, tenganisha waya wa plagi ya spaki (D,
Kielelezo 10), na uiweke mbali na plagi ya spaki (E). Kwa miundo ya injini iliyo na
kinga ya joto (Kielelezo 11), tenganisha waya wa spaki ya plagi kama ifuatavyo:
a.
Fungua kichupo chekundu (A, Kielelezo 11) kwenye kiunganishaji (B).
b.
Sukuma kichupo cheusi (C, Kielelezo 11) huku ukivuta kiunganishaji (B) nje
kutoka kwenye koili (D)
2.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, B, C, Kielelezo 4).
3.
Ondoa kifuniko kimoja cha tundu la kumwaga oili (F, G, Kielelezo 13). Mwaga oili
katika kontena iliyoidhinishwa.
4.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwaga oili (F, G, Kielelezo 13).
Ongeza Oili
Hakikisha injini haijainama.
Safisha vifusi vyote kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, B, C, Kielelezo 4).
2.
Polepole ongeza oili kwenye tundu la kujazia oili ya injini (E, F, Kielelezo 5). Usijaze
oili kupita kiasi.
3.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, B, C, Kielelezo 4).
a.
Kifaa Kirefu cha Kupima Kiwango cha Oili, iwapo kipo (B, Kielelezo 4):
Hakikisha kwamba alama zinazoashiria oili kujaa zilizo kwenye kifaa cha
kupima kiwango cha oili (B) zinaangalia juu ya injini.
b.
Kifaa Kifupi cha Kupima Kiwango cha Oili au Kifuniko cha Tundu la Kujazia
Oili, iwapo kipo (C, Kielelezo 4): Funika na ukaze kifaa cha kupima kiwango
cha oili (C).
4.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, B, C, Kielelezo 4) tena.
5.
Kagua kiwango cha oili. Hakikisha kwamba kiwango sahihi cha oili kiko juu ya
alama inayoashiria kujaa (D, Kielelezo 4).
6.
Weka kifaa cha kupima kiwango cha oili tena (A, B, C, Kielelezo 4).
7.
Unganisha waya wa plagi ya spaki (D, 10) kwenye plagi ya spaki (E). Kwa miundo
ya injini iliyo na kinga ya joto (Kielelezo 11) unganisha waya wa spaki ya plagi kama
ifuatavyo:
a.
Weka kiunganishaji (B, Kielelezo 11).
b.
Funga kichupo chekundu (A, Kielelezo 11).
Kufanya Udumishaji kwenye Chujio la Hewa
ONYO 
Mvuke wa mafuta unaweza kushika moto na kulipuka kw aharaka sana. Moto au
mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Usiwashe na kuendesha injini kamwe wakati kifaa cha usafishaji hewa (iwapo
kipo) au chujio la hewa (iwapolipo) kimeondolewa.
NOTISI 
Usitumie hewa au maji yaliyoshinikizwa kusafishia chujio. Hewa iliyoshinikizwa inaweza
kuharibu chujio na vioevu vitayeyusha chujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji ili kujua mahitaji ya huduma.
Miundo tofauti itatumia vichujio vya sifongo au karatasi. Baadhi ya miundo pia iinaweza
kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na kutumiwa
tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye injini yako
na ushughulikie kama ifuatavyo.
Kichujio cha Hewa cha Karatasi
1.
Legeza sehemu za kufunga (C, Kielelezo 14).
2.
Ondoa kifuniko (A, Kielelezo 14) na chujio (B).
3.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gongesha chujio (B, Kielelezo 14) kwenye eneo
gumu. Ikiwa chujio ni chafu, badilisha kwa chujio jipya.
4.
Weka chujio (B, Kielelezo 14).
5.
Weka kifuniko (A, Kielelezo 14) na ufunge vizuri ukitumia sehemu za kufunga (C).
Hakikisha sehemu za kufunga zimekazwa kabisa.
Chujio la Hewa la Karatasi - Nyembamba
1.
Sogeza wenzo (A, Kielelezo 15) ili kufungua kifuniko (C).
2.
Sogeza sehemu za kufunga (B, Kielelezo 15) ili kuondoa kifuniko (C).
3.
Ondoa chujio (D, Kielelezo 15).
4.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gongesha chujio (D, Kielelezo 15) kwenye eneo
gumu. Ikiwa chujio ni chafu, badilisha kwa chujio jipya.
5.
Sakinisha chujio (D, Kielelezo 15).
6.
Sakinisha kifuniko (C, Kielelezo 15). Songeza wenzo (A) hadi eneo la kufunga.
KUMBUKA: Kagua jinsi kifuniko cha sifongo (E, Kielelezo 15) kilivyotoshea. Hakikisha
kwamba kifuniko cha sifongo kimeingia vizuri mahali pake (F).
Kufanyia Huduma Mfumo wa Mafuta
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Mara kwa mara kagua tundu la tangi, tangi la mafuta, kifuniko cha mafuta, na
mirija kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha sehemu zilizoharibika.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka yakauke kabla ya kuwasha injini.
Chujio la Mafuta, iwapo lipo
1.
Kabla ya kubadilisha chujio la mafuta (A, Kielelezo 16), mwaga mafuta kutoka
kwenye tangi ya mafuta au funga vali ya kufunga mafuta. Ikiwa tangi la mafuta si
tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
2.
Finya vichupo (B, Kielelezo 16) kwenye vibanio (C) ukitumia koleo. Ondoa vibanio
kutoka kwenye chujio la mafuta (A).
3.
Zungusha na uvute mirija ya mafuta (D, Kielelezo 16) kutoka kwenye chujio la
mafuta.
4.
Kagua mirija ya mafuta (D, Kielelezo 16) kama kuna nyufa au uvujaji. Ikiwa
inahitajika, badilisha mirija ya mafuta.
5.
Badilisha chujio la mafuta (A, Kielelezo 16).
6.
Funga mirija ya mafuta (D, Kielelezo 16) kwa kutumia vibanio (C).
Chujio la Mafuta, iwapo lipo
1.
Ondoa kifuniko cha mafuta (A, Kielelezo 17).
2.
Ondoa chujio la mafuta (B, Kielelezo 17).
3.
Iwapo chujio msingi la mafuta ni chafu, lisafishe au ulibadilishe. Ukibadilisha chujio
msingi la mafuta, hakikisha umetumia chujio msingi la mafuta ambalo si ghushi.
Hifadhi
Mfumo wa Mafuta
Rejelea Kielelezo: 18.
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Kuhifadhi Mafuta
Kwa sababu taa za moto au vyanzo vingine vya mwako vinaweza kusababisha
milipuko, hifadhi mafuta au kifaa mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji,
au vifaa vingine ambavyo vina taa za moto.
Weka injini bila kuinama kwa mkao wa kawaida wa kuendesha. Jaza tangi la mafuta (A,
Kielelezo 18) kwa mafuta. Ili kuruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze kuzidi shingo ya tangi
la mafuta (B).
Mafuta yanaweza kuharibika yanapohifadhiwa katika kontena ya uhifadhi kwa zaidi ya
siku 30. Inapendekezwa kutumia kiimarishaji mafuta bila alkoholi na tiba ya ethanoli
45

Publicidad

loading