Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton 130000 Manual Del Operador página 42

Ocultar thumbs Ver también para 130000:

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 24
ONYO 
Mwako wa injini usiokusudiwa unaweza kusababisha mshutuko wa umeme au
moto na kupelekea kunaswa, kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha
mabaya ya ukataji wa ngozi.
Kabla ya kufanya marekebisho au ukarabati:
Tenganisha waya wa plagi ya spaki na uuweke mbali na plagi ya spaki.
Tenganisha betri katika kichwa cha hasi (injini tu zenye kianzishaji cha umeme.)
Tumia zana sahihi pekee.
Unapokagua uwepo wa cheche:
Tumia kifaa kilichoidhinishwa cha kujaribu plagi ya spaki.
Usikague cheche huku plagi ya spaki ikiwa imeondolewa.
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Ili kupata huduma ya udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo
ya kudhibiti mafukizo, wasiliana na kituo chochote kinachohitimu cha kukarabati
injini au mtoa huduma aliyehitimu wa kukarabati injini. Hata hivyo, ili kupata
huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima kazi ifanywe na muuzaji
aliyeidhinishwa na kiwanda. Rejelea Kauli za Udhibiti Mafukizo.
Ratiba ya Udumishaji
Saa 5 za Kwanza
Badilisha oili.
Mpishano wa Saa 8
Kagua kiwango cha oili ya injini.
Safisha maeneo yaliyo karibu na mafla na vidhibiti.
Safisha grili ya kuingiza hewa.
Mpishano wa Saa 50 au Kila Mwaka
Badilisha oili ya injini.
Fanyia huduma mfumo wa ekzosi.
Mpishano wa Saa 100
Fanyia huduma chujio la hewa.
Kila Mwaka
Badilisha plagi ya/za spaki.
Fanyia huduma chujio la hewa
Fanyia huduma mfumo wa kupoesha
1
Safisha mara nyingi zaidi katika mazingira ya vumbi au wakati kuna vipengee vingi
hewani
Rekebisha Kasi ya Injini
NOTISI 
Mtengenezaji wa kifaa hubainisha kasi ya juu zaidi ya injini kama ilivyosakinishwa
kwenye kifaa. Usizidishe kasi hii. Iwapo huna uhakika kasi ya juu zaidi ya kifaa hiki
ni ipi, au kasi ya injini iilivyopangwa tangu kiwandani, wasiliana na Muuzaji Huduma
Aliyeidhinishwa wa Briggs & Stratton ili kupata usaidizi. Kwa oparesheni salama na
sahihi ya kifaa hiki, kasi ya injini inapaswa tu kurekebishwa na mtaalamu wa huduma
aliyehitimu.
Rekebisha Kabureta
Marekebisho madogo ya kabureta yanaweza kuhitajika ili kufidia kwa tofauti zilizopo
katika mafuta, hali ya joto, mwinuko au mzigo.
1.
Sogeza kidhibiti injini (A, Kielelezo 10) hadi kwenye eneo linaloonyesha
MGURUMO.
2.
Rekekebisha rpm ya kasi ya mgurumo: Geuza vali ya mchanganyiko wa
mgurumo (B, Kielelezo 10) kuelekea upande wa kulia (KULIA) mpaka injini
ianze kuguruma kwa kutetemeka. Geuza vali ya mchanganyiko wa mgurumo
(B) kuelekea upande wa kushoto (KUSHOTO) mpaka injini ianze kuguruma
kwa kutetemeka. Kisha, geuza vali ya mchanganyiko wa mgurumo (B) kati ya
upande wa KUSHOTO na KULIA. Kagua RPM ya mgurumo na urekebishe iwapo
inahitajika.
Kufanyia Huduma Plagi ya Spaki
Kagua pengo la plagi ya spaki (A, Kielelezo  11) ukitumia pamba ya waya (B). Ikiwa
inahitajika, rekebisha pengo la plagi ya spaki.  Sakinisha na ukaze plagi ya spaki kwa
kiwango sahihi. Ili kupata maelezo maalum ya pengo na kukaza, rejelea sehemu ya
Maelezo.
42
1
.
1
.
KUMBUKA: Katika baadhi ya maeneo, kulingana na sheria za eneo husika ni
lazima kutumia plagi ya spaki ya kifaa kisichopitisha nishati ili kupunguza ishara
za kugurumisha. Ikiwa plagi ya spaki ya kifaa kisichopitisha nishati iliwekwa na
mtenegenezaji wa kifaa hicho, tu,ia aina sawa unapobadilisha.
Kufanyia Huduma Mfumo wa Mafukizo
ONYO 
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Vitu vinavyoweza kuwaka moto, kama vile majani, nyasi, brashi, vinaweza kushika
moto.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Ondoa uchafu kwenye mafla na injini.
Ni ukiukaji wa Kanuni za Rasilimali za Umma za California, Sehemu ya 4442, kutumia
au kuendesha injini katika eneo linalozungukwa na msitu, lililozungukwa na brashi, au
lililo na nyasi isipokuwa mfumo wa ekzosi una kishika spaki, kama ilivyobainishwa katika
sehemu ya 4442, kilichodumishwa katika hali fanisi ya kufanya kazi. Mamlaka nyingine
za majimbo au serikali ya kitaifa huenda zikawa na sheria sawia; Rejelea Kanuni za
Serikali ya KItaifa ya 36 CFR Sehemu ya 261.52. Wasiliana na mtengenezaji asilia wa
kifaa, muuzaji rejareja, au muuzaji ili kupata kishika spaki kilichobuniwa kwa ajili ya
mfumo wa ekzosi uliowekwa kwenye injini hii.
Ondoa vifuzi vilivyokusanyika kutoka kwenye mafla na eneo la silinda. Kagua mafla
kama ina nyufa, ubabuzi, au uharibifu mwingine. Ondoa kifaa cha kusonga au kishika
cheche, iwapo kipo, na ukague kama kuna uharibifu au uzuiaji wa kaboni. Iwapo
uharibifu utapatikana, sakinisha sehemu za ubadilishaji kabla ya kuendesha kifaa.
ONYO 
Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa na ziwekwe katika eneo sawa
kama sehemu asilia. Sehemu nyingine huenda zinaweza kuharibu kifaa au kusababisha
majeraha.
Badilisha Oili ya Injini
ONYO 
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka au kifo.
Wakati wa uendeshaji, injini na mafla zinakuwa moto. Ukigusa injini moto,
unaweza kuchomeka.
Ukimwaga oili kutoka kwenye tundu la juu la kujazia oili, ni lazima tangi la
mafuta liwe tupu. Ikiwa si tupu, mafuta yanaweza kuvuja na kusababisha moto
au mlipuko.
Kabla ya kugusa injini au mafla, zima injini na usubiri dakika mbili (2). Hakikisha
kwamba injini na mafla ni salama kugusa.
Oili iliyotumika ni bidhaa taka na hatari na ni lazima itupwe kwa njia sahihi. Usitupe
pamoja na taka ya nyumbani. Wasiliana na mamlaka yako ya ndani, kituo cha huduma
au muuzaji ili kupata zana salama za kutupa au kutumia tena.
Ondoa Oili
1.
Injini ikiwa IMEZIMWA lakini bado ina joto, tenganisha waya wa plagi ya spaki (D,
Kielelezo 12), na uihifadhi mbali na plagi ya spaki (E).
2.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 13).
3.
Ondoa kifuniko cha tundu la kumwaga oili (F, Kielelezo 13). Mwaga oili katika
kontena iliyoidhinishwa.
4.
Weka na ukaze kifuniko cha tundu la kumwaga oili (F, Kielelezo 13).
Ongeza Oili
Hakikisha injini inadumisha mizani.
Safisha vifusi vyote kutoka kwenye eneo la kujazia oili.
Rejelea sehemu ya Vipimo ili kujua kiwango cha oili.
1.
Ondoa kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 14). Futa oili kwenye kifaa
cha kupima kiwango cha oili ukitumia kitambaa safi.
2.
Polepole ongeza oili kwenye tundu la kujazia oili ya injini (C, Kielelezo 14) Usijaze
kupita kiasi.  Subiri dakika moja, na kisha ukague kiwango cha oili.
3.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 14).
4.
Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili. Kiwango sahihi cha oili
kiko juu ya alama inayoashiria kujaa (B, Kielelezo 14) kwenye kifaa cha kupima
kiwango cha oili.
5.
Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A, Kielelezo 14).
6.
Unganisha waya wa plagi ya spaki kwenye plagi ya/za spaki. Tazama sehemu ya
Kuondoa Oili.

Publicidad

loading

Este manual también es adecuado para:

250000