Descargar Imprimir esta página

Briggs & Stratton 130000 Manual Del Operador página 44

Ocultar thumbs Ver también para 130000:

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 24
3
®
Vanguard
iliyowekwa kwenye jenereta ya akiba: miezi 24 kwa matumizi ya kibinafsi,
hakuna hakikisho kwa matumizi ya kibiashara. Msururu wa Kibiashara ulio na tarehe
ya kutengenezwa ya kabla ya Julai 2017, miezi 24 kwa matumizi ya kibinafsi, miezi 24
kwa matumizi ya kibiashara.
*
Nchini Australia - Bidhaa zetu huja na waranti ambazo haziwezi kutojumuishwa chini
ya Sheria ya Mtumiaji ya Australia. Una haki ya kubadilishiwa au kurudishiwa pesa
kwa hitilafu kuu au fidia kwa uharibifu au hasara nyingine yoyote ya siku za usoni. Pia
una haki ya bidhaa kufanyiwa ukarabati au kubadilishwa endapo bidhaa hazitakuwa
za ubora unaokubaliwa na hitilafu haimaanishi kuharibika kwa njia kubwa. Ili kupata
huduma ya waranti, tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe
kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM,
au kwa kupiga simu kwa nambari 1300 274 447, au kwa kutuma barua pepe kwa
salesenquiries@briggsandstratton.com.au, au kutuma barua kwa Briggs & Stratton
Australia Pty Ltd, 1 Moorebank Avenue, Moorebank, NSW, Australia, 2170.
Kipindi cha waranti huanzia tarehe ya ununuzi ya mtumiaji wa kwanza kununua dukani
rejareja au mtumiaji wa mwisho wa kibiashara, na inaendelea kwa kipindi cha muda
kilichobainishwa katika jedwali lililo hapa juu. "Matumizi ya kibinafsi" inamaanisha
matumizi ya kibinafsi ya nyumbani ya mtumiaji wa rejareja. "Matumizi ya kibiashara"
inamaanisha matumizi mengine yote, yakijumuisha matumizi kwa madhumuni ya
kibiashara, ya kuzalisha mapato au ya kukodisha. Pindi tu injini inapopitia matumizi ya
kibiashara, baada ya hapo itazingatiwa kuwa injini ya matumizi ya kibiashara kwa ajili
ya hakikisho hili.
Usajili wa bidhaa hauhitajiki ili kupata huduma ya waranti ya bidhaa za Briggs &
Stratton. Hifadhi risiti yako ya ushahidi wa ununuzi. Ukikosa kutoa ushahidi wa
tarehe ya kwanza ya ununuzi wakati huduma ya waranti inapoombwa, tarehe ya
utengenezaji wa bidhaa itatumiwa kubaini kipindi cha waranti.
Kuhusu Hakikisho Lako
Hakikisho hili lenye kipimo linasimamia tu nyenzo zinazohusiana na injini na/au
utendakazi, na sio kubadilishiwa au kurudishiwa pesa ulizonunua kifaa ambacho kina
injini husika. Udumishaji, uimarishaji, marekebisho ya mara kwa mara au kuchakaa
na kuchanika kwa kawaida hazijasimamiwa na hakikisho hili. Vile vile, hakikisho
halitumiki ikiwa injini imehitilafiwa au kubadilishwa au ikiwa nambari tambulishi ya
injini imeharibiwa ua kuondolewa. Hakikisho hili halisimamii uharibifu kwenye injini au
matatizo ya utendakazi wa injini yanayosababishwa na:
1.
Matumizi ya sehemu ambazo siBriggs & Stratton
2.
Kuendesha injini zilizo na oili isiyotosha, chafu, au ya ubora usio sahihi;
3.
Matumizi ya mafuta machafu au yaliyoharibika, petroli yaliyotengenezwa kwa zaidi
ya 10% ya ethanoli, au matumizi ya mafuta kama vile petroli iliyoevuka au gesi
asili kwenye injini ambazo hazijaundwa/kutengenezwa tangu mwanzo na Briggs &
Stratton kuendeshwa kwa mafuta kama hayo;
4.
Uchafu ulioingia kwenye injini kwa sababu ya udumishaji kwa kutumia kisafishaji
hewa kisichofaa au ufunganishaji mbaya;
5.
Kugonga kitu kwa visu vya kukata vya mashine ya kukatia nyasi, adapta, impela
au vifaa vingine vya shafti kombo ambavyo vimelegea au havijawekwa ifaavyo au
ukazaji wa v-belt kupita kiasi;
6.
Sehemu au vifaa vinavyohusiana kama vile klachi, gia, vidhibiti vya kifaa, nk.,
ambavyo havijatolewa na Briggs & Stratton;
7.
Joto kupita kiasi kutokana na vipande vya nyasi, uchafu na vifusi, au viota vya
panya vinavyoziba au kufunika vifaa vya kupoesha au eneo la gurudumu la
kuongeza kasi, au kuendesha injini bila uingizaji hewa wa kutosha;
8.
Mtetemo kupita kiasi kwa ajili ya kasi kupita kiasi, uwekaji injini ikilegea, visua
kukata au impele ambazo zimelegea au havijasawazishwa, au uunganishaji
vibaya wa vipengele vya vifaa kwenye shafti kombo;
9.
Matumizi mabaya, ukosefu wa udumishaji wa mara kwa mara, usafirishaji,
ushughulikiaji, au uwekaji injini vibaya.
Huduma ya hakikisho inapatikana tu kupitia Wauzaji Huduma Walioidhinishwa wa
Briggs & Stratton. Tafuta Muuzaji Huduma Aliyeidhinishwa aliye karibu zaidi nawe
kwenye ramani yetu ya kutafuta wauzaji kwenye BRIGGSandSTRATTON.COM au
kwa kupiga simu kwa nambari  1-800-444-7774 (nchini Marekani).
80012121 (Rekebisho C)
44

Publicidad

loading

Este manual también es adecuado para:

250000