Briggs & Stratton Vanguard 290000 Manual Del Operario página 51

Ocultar thumbs Ver también para Vanguard 290000:
Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 15
Safisha eneo la kujaza mafuta kutokana na uchafu wowote.
Tazama Vipimo katika eneo la kiwango cha mafuta.
1.
Ondoa kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 9) na upanguse kwa
kitambaa safi.
2.
Polepole weka mafuta kwenye eneo la kuweka mafuta la injini (C, Kielelezo 9).
Usijaze kupita kiasi. Baada ya kuongeza mafuta, subiri dakika moja na kisha angalia
kiwango cha mafuta.
3.
Sakinisha na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 9).
4.
Ondoa kifaa cha kupima mafuta na ukague kiwango cha mafuta. Kiwango sahihi cha
mafuta kiko juu ya kiashiria kilichojaa (B, Kielelezo 9) kwenye kifaa cha kuangalia
kiwango cha mafuta.
5.
Sakinisha upya na ukaze kifaa cha kuangalia kiwango cha mafuta (A, Kielelezo 9).
6.
Unganisha waya ya kuziba cheche kwenye kuziba cheche (E), (D, Kielelezo 8).
Shughulikia Kichuja Hewa
Tazama Kielelezo: 11
Onyo
Fueli na mvuke wake unawaka na kulipuka hara sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha kuchomeka vikali au kifo.
Kamwe usiwashe na kuendesha wakati uunganishaji wa kisafisha hewa (iwapo kipo)
au kichuja hewa (iwapo kipo) kimeondolewa.
Notisi
Usitumie hewa au majimaji yaliyoshinikizwa kusafisha kichujio. Hewa
iliyoshinikizwa inaweza kuharibu kichujio na majimaji yatayeyusha kichujio.
Tazama Ratiba ya Udumishaji wa mahitaji ya huduma.
Modeli mbalimbali aidha zinatumia povu au kichujio cha karatasi. Baadhi ya modeli pia
zinaweza kuwa na kisafishaji cha mwanzo cha hiari ambacho kinaweza kusafishwa na
kutumiwa tena. Linganisha mifano kwenye mwongozo na aina iliyosakinishwa kwenye
injini yako na ushughulikie kama ifuatavyo.
1.
Fungua bizimu (A, Kielelezo 11) na uondoe kifuniko (B).
2.
Ondoa kifuniko cha (C, Kielelezo 11) na kishikiliaji (D).
3.
Ili kuzuia uchafu kuanguka kwenye kabureta, kwa makini ondoa elementi ya povu
(C, Kielelezo 11) kwenye sehemu ya chini ya kichuja hewa (D).
4.
Ondoa kichujio cha hewa (E, Kielelezo 11).
5.
Ili kulegeza uchafu, kwa utaratibu gonga kichujio katika eneo gumu. Iwapo kichujio
ni kichafu kupita kiasi, badilisha na kichujio kipya.
6.
Ondoa kisafishaji cha mwanzo (F, Kielelezo 11), iwapo kipo, kutoka kwenye kichujio
cha hewa (E).
7.
Osha kisafishaji cha mwanzo (F, Kielelezo 11), iwapo kipo, kwenye sabuni oevu na
maji. Ruhusu kisafishaji cha mwanzo kukauka kabisa. Usiweke mafuta kwenye
kisafishaji cha mwanzo.
8.
Sakinisha kisafishaji cha mwanzo kilichokauka (F, Kielelezo 11), ikiwa kipo, kwenye
kichujio cha hewa (E).
9.
Sakinisha kichujio cha hewa (E, Kielelezo 11) na kuweka salama kwa kishikiliaji (D)
na mkanda (C).
10.
Sakinisha jalada (B, Kielelezo 11) na ulinde kwa bizimu(s) (A).
Fanyia huduma Mfumo wa Mafuta
Tazama Kielelezo: 12
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya ya kuchomeka au kifo.
Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi, joto, na vyanzo vingine
vya mwako.
Kagua njia za mafuta, tangi, kifuniko na sehemu nyingine mara kwa mara ili uone
kama kuna nyufa na uvujaji. Badilisha kama itahitajika.
Kabla ya kusafisha au kubadilisha kichujio cha mafuta, mimina mafuta kutoka kwa
tangi ya mafuta au ufunge vali ya kuzuia mafuta.
Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo yatavukiza kabla ya kuwasha injini.
Sehemu za ubadilishaji lazima ziwe sawa na zilizosakinishwa kwa namna sawa na
sehemu asili.
Kichujio cha Mafuta, iwapo kipo
1.
Kabla ya kubadilisha kichujio cha mafuta (A, Kielelezo 12), iwapo kipo, mimina mafuta
kutoka kwa tangi la mafutai au funga vali ya kuzuia mafuta . La sivyo, mafuta
yanaweza kuvuja na kusababisha moto au mlipuko.
2.
Tumia koleo kubana vichupo (B, Kielelezo 12) kwenye vibanio (C), ) kisha telezesha
vibanio kutoka kwenye kichujio cha fueli (A). Zungusha na uvute njia za mfuta (D)
kutoka kwenye kichujio cha mafuta.
3.
Kagua njia za mfuta (D, Kielelezo 12)ili uone kamakuna nyufa au uvujaji. Badilisha
kama itahitajika.
4.
Badilisha kichujio cha mafuta (A, Kielelezo 12) kwa kichujio halisi cha kubadilisha
sehemu.
5.
Linda njia za mfuta (D, Kielelezo 12) kwa vibanio (C) kama inavyoonyeshwa.
Shughulikia Mfumo wa Kupoesha
Onyo
Injini inayoendesha inazalisha joto. Sehemu za injini, hususan mafla, huwa moto
zaidi.
Kuchomeka vikali kunaweza kusababishwa unapogusana nazo.
Uchafu unaoweza kuwaka, kama vile majani, nyasi, brashi, n.k., unaweza kushika
moto.
Ruhusu mafla, silinda na mapezi ya injini kupoa kabla ya kugusa.
Ondoa uchafu uliokusanyika kutoka kwenye eneo la mafla na eneo la silinda.
Notisi
Usitumie maji kusafisha injini. Maji yanaweza kuchafua mfumo wa fueli. Tumia
brashi au kitambaa kilichokauka kusafisha injini.
Hii ni injini inayopoeshwa na hewa. Uchafu unaweza kuzuia mtiririko wa hewa na
kusababisha injini kuchemka kupita kiasi, na kusababisha utendakazi mbaya na kupunguza
maisha ya injini.
1.
Tumia brashi au kitambaa kilichokauka kuondoa uchafu kutoka kwenye grili ya
kuingiza hewa.
2.
Weka uhusiano, springi na vidhibiti safi.
3.
Weka ene lililo karibu na nyuma ya mafla, iwapo ipo, huru kutokana na uchafu wowote
unaoweza kuwaka.
4.
Hakikisha mapezi ya kupoesha mafuta, iwapo yapo, yako huru kutokana na uchafu.
Baada ya kipindi cha muda, uchafu unaweza kukusanyika kwenye mapezi ya kupoesha
silinda na kusababisha injini kuwa moto kushinda kiasi. Uchafu huu hauwezi kuondolewa
bila kutokusanyika kwa kiasi fulani kwa injini. Ruhusu Mtoa Huduma wa Briggs & Stratton
Aliyeidhinishwa kukagua na kusafisha mfumo wa kupoesha hewa kama ilivyopendekezwa
kwenye Ratiba ya Udumishaji.
Hifadhi
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuhifadhi Mafuta Au Kifaa Kilicho na Mafuta Kwenye Tangi
Hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji, au vitu vingine ambavyo vina
taa za moto au vyanzo vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha moto kwenye
mvuke wa mafuta.
Mfumo wa Mafuta
Tazama Kielelezo: 13
Hifadhi kiwango cha injini (mkao wa kawaida wa kuendesha). Jaza tangi la mafuta (A,
Kielelezo 13) kwa mafuta. Ili kuruhusu uvukizi wa mafuta, usijaze kupita chini ya shingo
ya tangi la mafuta (B).
Mafuta yanaweza kuharibika yakihifadhiwa kwa zaidi ya siku 30. Mafuta yaliyoharibika
yanasababisha mabaki ya asidi na gundi kukusanyika katika mfumo wa mafuta au kwenye
sehemu muhimu za kabureta. Ili kuhifadhi usafi wa mafuta , tumia Briggs & Stratton
51

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Este manual también es adecuado para:

Vanguard 300000Vanguard 350000Vanguard 380000

Tabla de contenido