Yaliyomo:
Maelezo Jumla.................................................................... 64
Usalama wa Mwendeshaji..................................................64
Vipengele na Vidhibiti........................................................ 67
Uendeshaji........................................................................... 68
Udumishaji........................................................................... 72
Uhifadhi................................................................................ 75
Kutatua Matatizo................................................................. 77
Maelezo................................................................................ 78
Maelezo Jumla
Ili kupata maelezo zaidi, rejelea Mwongozo wa Mawasiliano
wa Mteja umejumuishwa na kifaa.
Picha zilizo katika hati hii ni za mfano tu. Huenda
kifaa chako kikaonekana kuwa tofauti na picha
zilizoonyeshwa. KUSHOTO na KULIA zinarejelewa kulingana
na mahali pa kuendeshea.
Utumizi wa sehemu ya Muhimu na Kumbusho katika
maandishi inaonyesha ufafanuzi, mambo ya kipekee, au
mbadala za taratibu.
Tafsiri zote za lugha za hati hii zimetokana na faili asili ya
Kiingereza.
Tumia tena mifuko yote, oili na betri zilizotumika kulingana na
kanuni husika za serikali.
Usalama wa Mwendeshaji
Hifadhi maagizo haya kwa ajili ya marejeleo ya siku
zijazo. Mwongozo huu una maelezo ya usalama ili
kukufahamisha kuhusu hatari zinazohusiana na bidhaa hii na
jinsi ya kuziepuka hatari hizo. Pia mwongozo una maagizo
muhimu ambayo ni lazima yafuatwe wakati wa utayarishaji,
uendeshaji, na udumishaji wa kwanza kabisa wa bidhaa hii.
Kifaa hiki kimeundwa na kusudiwa kutumiwa kukata nyasi
iliyotuzwa vyema na hakijakusudiwa kwa madhumuni
mengine yoyote.
Ni muhimu usome na kuelewa maagizohaya kabla ya kujaribu
kuanzisha au kuendesha kifaa hiki.
Hakikisha kwamba una ufahamu wa kina kuhusu vidhibiti na
utumizi mzuri wa bidhaa.
Jua jinsi ya kusimamisha kifaa na kuzima vidhibiti kwa
haraka.
64
Mwongozo wa Utambulisho wa
Mwinamo
Namna ya kupima mwinuko wa eneo tambarare le nyasi
ulio na simu maizi au zana ya kitafuta pembe:
Onyo
Usiendeshe kwenye miteremko iliyoinama zaidi ya digrii 10.
1. Tumia pembezo iliyonyoka na iliyo na urefu wa angalau
fiti mbili (2) (A, Kielelezo 1). Kipande cha chuma cha 2x4
au kilichonyoka hufanya kazi vyema.
2. Zana za kitafuta pembe.
a. Tumia simu yako maizi: Simu nyingi maizi (B,
Kielelezo 1) zina zana ya kupima mwinamo (kitafuta
penbe) ambayo imewekwa chini ya programu ya dira
(programu). Au, tafutiza duka la programu tumizi kwa
kupata programu tumizi za kipima mwinuko.
b. Tumia zana za kutafuta pembe: Zana za kutafuta
pembe (C na D, Kielelezo 1) zinapatikana madukani
au mtandaoni (pia inajulikana kama "inclinometer",
"protractor", "angle meter", au "angle gauge"). Aina
ya kubonyeza (C) au aina ya dijitali (D) inafanya
kazi, huenda nyingine zikakosa kufanya kazi. Soma
na ufuate maagizo yanayoandamana na kifaa cha
kutafuta pembe.
3. Weka upande ulionyoka ulio na urefu wa fiti mbili (2)
kwenye sehemu iliyoinama zaidi ya mteremko. Weka bodi
kwenye sehemu ya juu na chini ya mteremko.
4. Ipange simu maizi au zana ya kitafuta pembe kwenye
pembezo iliyonyoka na uisome pembe katika digrii. Huu
ndio mwinuko wa eneo lako la nyasi.
Kumbuka: Mwongozo wa kutambua mteremko wa karatasi ya
geji umejumuishwa katika pakiti ya maandishi ya bidhaa yako
na pia inaweza kupakuliwa kwenye tovuti ya mtengenezaji.
Alama za Usalama na Maana Yake
Alama
Maelezo ya usalama kuhusu hatari zinazoweza
kusababisha jeraha la kibinafsi.
Soma na uelewe Mwongozo wa Mwendeshaji kabla ya
kuendesha kifaa na kukifanyia huduma.
Soma na uelewe Mwongozo wa Mwendeshaji kabla ya
kufanyia kifaa huduma.
Maana