Descargar Imprimir esta página

Victa SPX2342F Manual Del Operador página 71

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 19
Washa Injini.
Onyo
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na
kulipuka ka haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya
ya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuwasha Injini
• Hakikisha kwamba plagi ya spaki, mafla, kifuniko cha
mafuta, na kisafishaji hewa (iwapo kipo) vimefungwa
na kukazwa.
• Usishtue injini wakati plagi ya spaki imeondolewa.
• Injini ikifurika, weka choki (ikiwa ipo) katika eneo la
kuonyesha FUNGUA / ENDESHA (OPEN / RUN),
sogeza kidhibiti injini (ikiwa kipo) hadi eneo la
kuonyesha HARAKA (FAST) na ushtue hadi injini
iwake.
Onyo
Injini hutoa moshi wa sumu ya kaboni monoksidi, usio na
harafu, wala rangi.
Kupumua kaboni monoksidi kunaweza kusababisha
kichefuchefu, kuzirai au kifo.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya
ya kuchomeka au kifo.
• Washa na uendeshe injini nje ya chumba.
• Usiwashe wala kuendesha injini ndani ya eneo
lililofunikwa, hata kama milango na madirisha yako
wazi.
1. Kague kiwango cha oili (rejelea Kagua na Uongeze Oili
ya Injini).
2. Hakikisha vidhibiti vya uendeshaji kifaa vimezimwa.
3. Kalia kiti na uinue JUU wenzo wa kurekebisha kiti ili
kufunga kiti katika nafasi yake.
4. Weka breki za kuegesha. Sukuma pedali ya breki, vuta
JUU kidhibiti cha breki ya kuegesha, na uachilie pedali ya
breki.
5. Zima swichi ya PTO kwa kusukuma NDANI.
6. Weka kidhibiti injini/choki katika eneo linaloonyesha
HARAKA (FAST).
7. Ingiza ufunguo ndani ya swichi ya kuwasha na
uuzungushe hadi eneo linaloonyesha WASHA/ANZISHA
(ON/START).
8. Baada ya injini kuwaka, songeza kidhibiti injini/choki hadi
kasi nusu. Pasha injini joto kwa kuiendesha kwa angaa
sekunde 30.
9. Weka kidhibiti injini/choki katika eneo linaloonyesha
HARAKA (FAST),
Katika tukio la dharura injini inaweza kusimamishwa kwa
urahisi kwa kuzungusha swichi ya kuwashia hadi eneo
linaloonyesha SIMAMA (STOP). Ili kuzima injini kwa njia ya
kawaida fuata utaratibu uliotolewa katika Kusimamisha Trekta
na Injini.
Kumbuka: Injini ikikosa kuwaka baada ya kujaribu mara
kadhaa, wasiliana na muuzaji aliyeidhinishwa.
Kusimamisha Trekta na Injini
Onyo
Mafuta na mvuke wake yanaweza kuwaka moto na kulipuka
kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya
ya kuchomeka au kifo.
• Ujaribu kutoruhusu hewa kuingia kwenye kabureta ili
kusimamisha injini.
1. Achilia pedali za kasi ya ardhini (A, Kielelezo 7) hadi
kwenye eneo la linalonyesha GIA HURU (NEUTRAL).
2. Ukiwa ungali kwenye nyasi, zima swichi ya PTO (B),
kisha usubiri sehemu zote zinazozunguka zisimame.
3. Sogeza kidhibiti Injini ( C) (au kidhibiti injini/choki) hadi
eneo linaloonyesha POLEPOLE (SLOW) na uzungushe
ufunguo wa kuwasha (D) hadi eneo linaloonyesha ZIMA
(OFF).
4. Ondoa ufunguo.
5. Weka breki ya kuegesha (E). Sukuma pedali ya breki
(F), vuta JUU kidhibiti cha breki ya kuegesha, na uachilie
pedali ya breki.
Katika tukio la dharura injini inaweza kusimamishwa kwa
urahisi kwa kuzungusha swichi ya kuwashia hadi SIMAMA
(STOP).
Uendeshaji Trekta
1. Kalia kiti na urekebishe kiti ili uweze kufikia vidhibiti vyote
vizuri. Tazama Vipengele na Vidhibiti. 
2. Weka kidhibiti breki ya kuegesha:
a. Sukuma chini pedali ya breki kabisa. 
b. Vuta JUU kwenye breki ya kuegesha. 
c. Achilia pedali ya breki. 
3. Hakikisha swichi ya PTO imezimwa. 
4. Washa injini. Tazama Washa Injini. 
5. Ondoa breki ya kuegesha:
a. Sukuma CHINI pedali ya breki kabisa. 
b. Sukuma NDANI kwenye udhibiti wa breki ya
kuegesha. 
c. Achilia pedali ya breki. 
6. Sukuma chini pedali ya kudhibiti kasi ili uende mbele.
Achilia pedali hii ili usimame.
Kumbuka: Unavyosukuma pedali zaidi ndivyo trekta
itakwenda haraka zaidi. 
71

Publicidad

loading

Este manual también es adecuado para:

2691498