A
B
C
D
66
Ikoni za Lebo za Usalama
1
ONYO: Soma na uelewe Mwongozo wa Mwendeshaji kabla
ya kutumia mashine hii. Fahamu eneo na utendaji wa vidhibiti
vyote. Usiendeshe mashine hii isipokuwa ikiwa umepitia
mafunzo.
2
HATARI - HATARI YA KUKOSA NGUVU YA KUKAMATA
ARDHI, KUTELEZA, KUENDESHA NA UDHIBITI KWENYE
MTEREMKO: Ikiwa mashine itasimama kwenda mbele au
itaanza kuteleza kwenye mteremko, simamisha visu na
uendeshe polepole kutoka kwenye mteremko.
3
HATARI: HATARI YA MOTO: Weka kifaa bila nyasi, majani na
oili nyingi kupita kiasi. Usiongeze mafuta wakati injini ipo moto
au inaguruma. Zima injini, ondoa ufunguo na uiruhusu ipoe kwa
angalau dakika 3 kabla ya kuongeza mafuta. Usiongeze mafuta
ukiwa ndani ya chumba, katika trela lililofunikwa, gereji au
maeneo mengine yaliyofungwa. Safisha mafuta yaliyomwagika.
Usivute sigara ukiwa unaendesha mashine hii.
4
HATARI - HATARI YA KUINAMA NA KUTELEZA: Kata nyasi
kwenda juu na chini ya miteremko si kutoka upande mmoja hadi
mwingine. Usiendeshe kwenye miteremko iliyoinama zaidi ya
digrii 10. Epuka kupiga kona ghafla na kwa kasi ukiwa kwenye
miteremko.
5
HATARI - HATARI YA KUKATWA VIUNGO VYA MWILI: Ili
uepuke majeraha kutokana na visu vinavyozunguka na sehemu
zinazotembea, weka vifaa vya usalama (vizuizi, ngao na swichi)
tayari na viwe vinafanya kazi.
6
Usikate nyasi wakati watoto au watu wengine wapo karibu.
Usiwahi kubeba watu hasa watoto hata kama visu vimezimwa.
Usikate nyasi ukirudi nyuma isipokuwa kama inahitajika.
Tazama chini na nyuma – kabla na wakati unarudi nyuma.
7
Rejelea maelezo ya kiufundi kabla ya kufanya ukarabati au
udumishaji wa kiufundi. Wakati unaiacha mashine, zima injini,
weka breki ya kuegesha kwenye eneo la kufunga na uondoe
ufunguo wa kuwasha.
8
Katia nyasi mbali na watu na watoto. Ondoa vitu ambavyo
vinaweza kurushwa na visu. Usikate nyasi bila chuti ya kutoa
nyasi kuwekwa.
9
Usikate nyasi bila chuti ya kutoa nyasi au kikamata nyasi
kuwekwa.