Onyo
Cheche zisizokusudiwa zinaweza kusababisha moto au
mrusho wa umeme.
Uwashaji usiokusudiwa unaweza kusababisha kunaswa,
kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha makali ya
ukataji wa ngozi.
Kabla ya kutekeleza marekebisho au ukarabati:
• Tenganisha waya wa plagi ya spaki na uuweke mbali
na plagi ya spaki.
• Tenganisha betri katika kichwa hasi (negative) (injini tu
zenye kianzishi cha umeme).
• Tumia zana sahihi tu.
• Usihitilafiane na springi ya kidhibiti, viungo, au viungo
vingine ili kuongeza kasi ya injini.
• Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawa
na ziwekwe katika eneo sawa kama sehemu asilia.
Sehemu nyingine huenda zisifanye kazi kwa njia sawa,
zinaweza kuharibu kifaa na inaweza kusababisha
majeraha.
• Usigonge gurudumu la kuongeza kasi ya injini kwa
nyundo au kifaa kigumu kwa sababu gurudumu la
kuongeza kasi ya injini linaweza kuvunjika wakati wa
kuendesha.
Ratiba ya Udumishaji
KIFAA NA KIKATA NYASI
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
Kagua Mfumo wa Usalama wa Intaloki.
Ondoa vitu visivyotakikana kwenye kifaa, deki ya mashine ya kukatia nyasi,
na eneo la injini.
Kila Baada ya Saa 25 au Kila Mwaka
Safisha kipoeshaji oili ya ubadilishaji gia.
Kagua kiwango cha oili ya ubadilishaji gia.
Kagua hewa kwenye tairi.
Kagua muda wa kusimama wa visu vya mashine ya kukatia nyasi.
Kagua kifaa na mashine ya kukatia nyasi kama kuna sehemu zilizolegea.
Kagua kiwango cha oili kwenye akseli ya mbele.
Baada ya Saa 50 au Kila Mwaka
Kusafisha Betri na Kebo.
Kagua breki za trekta.
Kila Baada ya Saa 250 au Kila Mwaka
Badilisha oili ya ubadilishaji gia na chujio.
Kagua breki za trekta.
Kila Msimu wa Vuli na Masika
Kagua oili ya kisanduku cha gia cha deki ya mashine ya kukatia nyasi.
Mtembelee Muuzaji Kila Mwaka
Kulainisha trekta na mashine ya kukatia nyasi.
Ukaguzi wa visu vya mashine ya kukatia nyasi.***
* Yoyote ile inayotangulia.
** Miundo ya 4WD pekee.
*
**
*
*
*** Kagua visu vya mashine ya kukatia nyasi mara nyingi
zaidi katika maeneo yenye udongo wa kichanga au hali za
vumbi kali.
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
Kagua kiwango cha oili ya injini.
Safisha maeneo yaliyo karibu na mafla na vidhibiti.
Kila Baada ya Saa 100 au Kila mwaka
Badilisha plagi za spaki.
Badilisha oili ya injini.
Badilisha chujio la mafuta, iwapo lipo.
Fanyia huduma chujio la hewa.
Safisha kisafishaji cha mwanzo (iwapo kipo).
Fanyia huduma mfumo wa ekzosi.
Kila baada ya Saa 250
Kagua uwazi wa vali. Rekebisha kama itahitajika.
Kila baada ya Saa 400 au Kila mwaka
Badilisha chujio la hewa.
Badilisha chujio la mafuta.
Fanyia huduma mfumo wa kupoesha.
Safisha fini za oili.
Ukaguzi wa Hewa kwenye Tairi
Ili kuhakikisha nguvu sahihi ya kukamata ardhi na tendakazi
bora wa kukata nyasi, hakikisha shinikizo la hewa kwenye
tairi ni 12-14 psi (0.82-0.96 bar). Rejelea Ukaguzi wa Hewa
kwenye Tairi katika Ratiba ya Udumishaji. Pia, tazama
Shinikizo la Hewa kwenye Tairi katika sehemu ya Maelezo.
Kumbuka: Shinikizo la Hewa kwenye Tairi linaweza
kutofautiana kidogo na "Shinikizo la Juu Zaidi" lililoonyeshwa
kwenye upande wa matairi.
Safisha Betri na Kebo
Onyo
Wakati wa kuondoa au kuweka kebo za betri, tengenisha
kebo hasi (negative) KWANZA na kisha iunganishe tena
ikiwa ya MWISHO. Ikikosa kufanyika kwa mpangilio huu,
kichwa chanya (positive) kinaweza kupata shoti kwenye
fremu na zana.
1. Tenganisha kebo na betri, kebo hasi (-) kwanza.
2. Ondoa mkanda wa kushikilia betri na betri.
3. Safisha chumba cha betri ukitumia mchanganyiko wa
magadi ya kuumulia na maji.
4. Safisha vichwa vya betri na ncha za kebo na brashi
yenye waya mpaka zing'ae.
5. Funga tena betri kwenye chumba cha betri upya, na
ukaze na mkanda wa kushikilia betri.
6. Weka kebo za betri tena, kebo chanya (+) kwanza (A, B,
Kielelezo 10).
INJINI
73