L
Choki
M
Pedali za Kasi ya Ardhini
N
Ubadilishaji Urefu wa Kukatia wa Mashine ya
Kikatia Nyasi
O
Wenzo wa Kutoa Gia
P
Tangi la Mafuta
R
Pedali ya Breki
S
Wenzo wa Kurekebisha Kiti (ikiwa upo)
Uendeshaji
Eneo la Kuendeshea
1. Jifahamishe na eneo ambapo unapanga kuendeshea
mashine ya kukatia nyasi.
2. Hakikisha kwamba eneo hili halina vifusi au vitu
visivyotakikana ambavyo vinaweza kurushwa na visu.
Hatari
Mashine hii ina uwezo wa kurusha vitu vinavyoweza
kuwajeruhi waliosimama kando au kusababisha uharibifu
kwenye majengo.
• Usiendeshe mashine bila kifaa kizima cha kukamata
nyasi, kifaa cha kutoa nyasi, au vifaa vingine vya
usalama vikiwepo na vikifanya kazi vizuri. Kagua mara
nyingi kama kuna dalili za kuchakaa na ubadilishe
kama inahitajika.
• Ondoa vitu vyovyote vilivyo kwenye eneo la
kuendeshea ambavyo vinaweza kurushwa au
kuhitilafiana na utendakazi wa mashine.
3. Peleka kifaa cha kukatia nyasi nje, kabla ya kuwasha
injini.
68
Onyo
Injini hutoa moshi wa sumu ya kaboni monoksidi, usio na
harafu, wala rangi. Kupumua kaboni monoksidi kunaweza
kusababisha kuhisi kutapika, kuzirai au kifo.
4. Kumbuka miteremko na maeneo yote yaliyoshuka ghafla.
Hatari
Kuendesha kwenye miteremko, au karibu na maji, au
maeneo yaliyoshuka ghafla kunaweza kusababisha
kupoteza udhibiti na kubingirika.
• Kata nyasi kwenda juu na chini ya miteremko, sio
kutoka upande mmoja hadi mwingine.
• Punguza kasi na uwe makini zaidi kwenye miteremko.
• Usiendeshe kwenye miteremko ya zaidi ya digrii 10,
ambayo ni mwinuko wa futi 3.5 kwenye umbali wa futi
20.
• Kaa umbali wa sawia na ya mashine mbili za kukatia
nyasi na eneo lenye maji, kuta, au maeneo yaliyoshuka
ghafla.
• Epuka kukata nyasi zilizo na majimaji au unyevunyevu.
• Usiendeshe mashine katika hali yoyote ambapo nguvu
ya magurudumu kukamata chini, uendeshaji au ustawi
hauaminiki. Magururdumu yanaweza kuteleza hata
kama magurudumu yamesimamishwa.
• Epuka kuanza au kusimama kwenye mteremko.
• Usifanye mabadiliko ya ghafla katika kasi au
mwelekeo.
• Piga kona polepole na kwa utaratibu.
• Kuwa mwangalifu unapoendesha mashine nyenye vifaa
vya kukamata nyasi au viambatisho vingine. Vinaweza
kuathiri ustawi wa mashine hii.
• Fuata mapendekezo ya mtengenezaji kuhusu vipimo
vya uzito wa vifaa vilivyokokotwa na kukokota katika
miteremko. Tazama Vifaa Vinavyokokotwa.
5. Hakikisha kwamba eneo la kuendeshea halina watu
waliosimama kando, hasa watoto.