Descargar Imprimir esta página

Victa SPX2342F Manual Del Operador página 72

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 19
7. Ili kusimamisha trekta, achilia pedali za kudhibiti
kasi, uweke breki ya kuegesha, na uzime injini.
Tazama Simamisha Trekta na Injini. 
Kukata Nyasi
Hatari
Mashine ina uwezo wa kuikata mikono na miguu, na
kurusha vitu. Kukosa kuzingatia maagizo ya usalama
kunaweza kusababisha kifo au majeraha mabaya.
• Endesha mashine tu wakati wa mchana au ukitumia taa
yenye mwangaza mzuri.
• Epuka mashimo, matope, matuta, mawe, au hatari
nyingine fiche.
Maeneo ambayo si tambarare yanaweza kufanya
mashine kubingirika au kumfanya mwendeshaji
kupoteza mizani au kuanguka.
• Usielekeze vitu vinavyotolewa kuelekea kwa mtu
yeyote. Epuka kuelekeza kwenye ukuta au kizuizi, vitu
vinavyotolewa, kwani vinaweza kumrudia mwendeshaji
kifaa.
• Simamisha visu unapovuka sehemu zenye
changarawe.
• Usiache mashine ikiwa peke yake. Kila wakati egesha
mahali tambarare, zima kiambatisho, weka breki ya
kuegesha, zima injini, na uondoe funguo.
1. Weka breki ya kuegesha (B, Kielelezo 8).
2. Hakikisha swichi ya PTO (C) imezimwa.
3. Washa injini (rejelea Washa Injini).
4. Weka udhbiti wa throtoli (D) hadi katika mkao wa
HARAKA.
5. Washa swichi ya PTO ili kuwasha visu vya kukata nyasi.
6. Tumia Wenzo wa Urefu wa Kukata (A) kuweka urefu wa
kukata katika kiwango unachotaka.
7. Toa breki ya kuegesha, kisha uanze kukata nyasi.
8. Ukimaliza kukata nyasi, zima PTO.
9. ZIMA injini (rejelea Kusimamisha Trekta na Injini).
Onyo
Injini itazima ikiwa pedali ya kasi ya ardhini ya kurudi
nyuma itasukumwa wakati PTO imewashwa na RMO
haijawezeshwa. Mwendeshaji anapaswa kila wakati kuzima
PTO kabla ya kuendesha kwenye barabara, vinjia, au eneo
lolote ambalo linaweza kutumiwa na magari mengine.
Kupoteza nguvu kwa ghafla kunaweza kusababisha hatari.
Chaguo la Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma
(RMO)
72
Hatari
Kukata nyasi ukirudi nyuma kunaweza kuwa hatari kwa
waliosimama kando. Ajali za kuhuzunisha zinaweza
kutokea ikiwa mwendeshaji hayuko makini kwa kuwepo
kwa watoto. Mara nyingi watoto huvutiwa na mashine hiyo
na shughuli ya ukataji nyasi. Usiwahi kudhania kwamba
watoto watasalia pale ulipowaona mara ya mwisho.
• Weka watoto mbali na eneo linalokatwa nyasi na chini
ya uangalizi mkubwa wa mtu mzima anayewajibika.
• Usiwahi kubeba watu, hasa watoto, hata kama kisu(vi)
vimezimwa. Watoto wanaweza kuanguka na kujeruhiwa
vibaya sana au kuhitilafiana na uendeshaji salama
wa mashine. Watoto ambao wamewahi kubebwa na
kifaa hapo awali huenda wakatokea ghafla katika eneo
linalokatwa nyasi wakitaka kubebwa tena na wagongwe
au kusukumwa na mashine hiyo
• Usikate nyasi ukirudi nyuma isipokuwa kama
inahitajika. Kila wakati tazama chini na nyuma kabla na
wakati wa kurudi nyuma.
• Mashine ikikata nyasi ikirudi nyuma bila kuwezesha
Chaguo la Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma, mtembelee
muuzaji aliyeidhinishwa mara moja.
Chaguo la Kukata Nyasi Ukirudi Nyuma (RMO)
linamwezesha mwendeshaji kukata nyasi akirudi nyuma.
Ili kuliwezesha:
1. Washa swichi ya PTO (B, Kielelezo 9).
2. Zungusha ufunguo wa Chaguo la Kukata Nyasi Ukirudi
Nyuma (RMO) (A) hadi eneo linaloonyesha WASHA
(ON).
3. Taa ya L.E.D. itawaka.
4. Mwendeshaji anaweza kukata nyasi akirudi nyuma.
Kumbuka: Ufunguo unapaswa kuondolewa ili kuzuia ufikiaji
wa RMO.
Udumishaji

Publicidad

loading

Este manual también es adecuado para:

2691498