Descargar Imprimir esta página

Victa SPX2342F Manual Del Operador página 75

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 19
Notisi
Plagi za spaki zina ustahimilivu tofauti kwa joto. Ni muhimu
kwamba plagi sahihi ya spaki itumiwe, la sivyo, injini
inaweza kuharibika. Badilisha plagi ya spaki kwa nyingine
ya aina sawia au ya ubora sawia. 
Safisha Plagi ya Spaki 
Safisha plagi ya spaki ukitumia brashi ya waya na kisu
kigumu. USITUMIE kikwaruzo. 
Kagua Pengo la Plagi ya Spaki 
Tumia kifaa cha kupima pengo la plagi ya spaki
(A, Kielelezo 15) wa ili ukague pengo kati ya elektrodi zote
mbili. Wakati pengo hili liko sawa, kifaa cha kupima pengo
kitajikokota kidogo unapokivuta kupitia kwenye pengo. 
Ili kurekebisha pengo la plagi ya spaki, tumia geji ya plagi ya
spaki na kwa utaratibu ukunje elektrodi iliyokunjwa. Hakikisha
kwamba haugusi katikati mwa elektrodi au kauri.  
Weka Plagi ya Spaki 
Kaza plagi ya spaki ukitumia vidole vyako, na kisha, ikaze
ukitumia spana kama inavyoonyeshwa katika Kielelezo 16. 
• 180 in-lbs (20 Nm), AU 
• Mzunguko 1/2 wakati unaweka tena plagi asilia ya spaki.
Mzunguko 1/4 wakati unaweka plagi mpya ya spaki. 
Sukuma Trekta kwa Mikono
Ili kusukuma trekta, fanya yafuatayo:
1. Zima swichi ya PTO (A, Kielelezo 17).
2. Zima injini.
3. Vuta sehemu ya gia ili ifunge ndani ya eneo lililo wazi.
4. Trekta inaweza kusukumwa kwa mikono
Onyo
Kukokota kifaa kutasababisha uharibifu kwenye klachi na
gea. Usitumie gari jingine kusukuma au kukokota mashine
hii. Usisongeze wenzo wa kubadilisha gia wakati injini
imewashwa.
Vifaa Vinavyokokotwa
1. Kabla ya kukokota kifaa, hakikisha kwamba sehemu ya
kuvutia imetengenezwa kwa ajili ya ukokotaji.  
2. Usiunganishe kifaa cha kukokotwa isipokuwa katika
sehemu ya kuvutia. 
3. Kwa vifaa zinavyokokotwa na kukokota vifaa kwenye
miteremko, fuata mapendekezo ya upeo wa uzani
yaliyoorodheshwa hapa chini.
• Jumla ya juu zaidi ya uzito (trela na mzigo) ni pauni
400 (181.4 kg). 
• Upeo wa pauni 20 (9.1 kg) kwa futi juu au chini
kwenye ulimi. 
• Nenda kutoka kipimo cha 10° hadi 5° kwenye
mteremko wowote. 
4. USIWARUHUSU watoto au watu wengine kupanda
kwenye kifaa kinachovutwa. 
5. Uzito wa kifaa kinachovutwa unaweza kusababisha
kupoteza nguvu ya kukamata ardhi na kupoteza udhibiti. 
6. USIHAMISHIE kwenye gia huru na kuteremka kwenye
mteremko. 
Safisha Deki ya Mashine ya Kukatia
Nyasi (ikiwa ipo)
Kumbuka: 
Tumia lango la kuoshea (C, Kielelezo 18) ili kusafisha upande
wa chini wa deki ya mashine ya kukatia nyasi. 
1. Weka kifaa kwenye eneo tambarare na laini. 
2. Unganisha sehemu ya haraka kutenganisha
(A, Kielelezo 18) kwenye mfereji wa bustani (B) na kisha
uunganishe kwenye lango la kuoshea (C) kwenye deki ya
mashine ya kukatia nyasi. 
3. FUNGULIA maji. 
4. Washa injini. 
5. Weka Urefu wa Kukata katika mkao wa juu zaidi. 
6. Washa swichi ya Kuwasha Nishati (PTO) ili kuwezesha
visu vya kukata nyasi. Mzunguko wa visu na maji yale
ya mfereji utasafisha sehemu ya chini ya deki la ukataji
nyasi. 
7. Tenganisha Kuwasha Nishati na uzime injini. 
8. FUNGA maji. 
9. Ondoa mfereji wa bustani na sehemu ya kutenganisha
haraka kutoka kwenye eneo la kusafishia (C). 
Uhifadhi
Onyo
Kamwe usiweke kifaa (kikiwa na mafuta) katika jengo
lisilo wazi, na bila hewa tosha. Mivuke ya mafuta inaweza
kusafiri hadi kwenye chanzo cha mwako (kama vile tanuu,
hita ya kuchemshia maji, n.k) na kusababisha mlipuko. 
• Hifadhi mbali na tanuu, stovu, hita za kuchemshia maji,
au vifaa vingine ambavyo vina taa za moto au vyanzo
vingine vya mwako kwa sababu vinaweza kuwasha
moto kwenye mvuke wa mafuta. 
Vifaa 
ZIMA swichi ya Kuwasha Nishati (PTO), na uweke breki ya
kuegesha. Ondoa ufunguo wa kuwashia. Acha mashine ipoe.
Ukiondoa betri, muda wa kudumu wa betri utaongezeka.
Hakikisha kwamba betri ipo mahali pasipo na joto, na pakavu,
na uiweke ikiwa imejaa chaji. Ikiwa betri imeachwa ndani ya
kifaa, tenganisha kebo hasi. 
Mfumo wa Mafuta 
Mafuta yanaweza kuharibika yanapohifadhiwa katika kontena
ya uhifadhi kwa zaidi ya siku 30. Kila mara unapojaza
kontena kwa mafuta, ongeza kiimarishaji mafuta kwenye
mafuta kama ilivyobainishwa na maagizo ya mtengenezaji.
Hii inafanya mafuta kukaa yakiwa safi na kupunguza matatizo
75

Publicidad

loading

Este manual también es adecuado para:

2691498