Hatari
Kifaa hiki cha kukatia nyasi kina uwezo wa kukata mikono
na miguu.
• Zima mashine ya kukatia nyasi wakati watoto au watu
wengine wapo karibu.
• Weka watoto mbali na eneo linalokatwa nyasi na chini
ya uangalizi mkubwa wa mtu mzima anayewajibika.
• Usiwahi kubeba watu, hasa watoto, hata kama kisu(vi)
vimezimwa. Watoto wanaweza kuanguka na kujeruhiwa
vibaya sana au kuhitilafiana na uendeshaji salama
wa mashine. Watoto ambao wamewahi kubebwa na
kifaa hapo awali huenda wakatokea ghafla katika eneo
linalokatwa nyasi wakitaka kubebwa tena na wagongwe
au kusukumwa na mashine hiyo.
• Kuwa mwangalifu unapokaribia kona usizoweza kuona
mbali, vichaka, miti, au vitu vingine ambavyo vinaweza
kuzuia kuona.
Majaribio ya Mfumo wa Usalama wa
Intaloki
Kifaa hiki kimewekwa Mfumo wa Usalama wa Intaloki.
Usijaribu kupita pembeni au kuhitilafiana na swichi na vifaa.
Onyo
Mashine ikikosa kupita jaribio la usalama, usiendeshe
mashine. Tembelea muuzaji aliyeidhinishwa.
Jaribio la 1 — Injini HAIPASWI kuwaka ikiwa
• Swichi ya Kuwasha Nishati (PTO) IMEZIMWA, AU
• Pedali ya breki HAIJASUKUMWA kabisa (breki ya
kuegesha IMETOLEWA).
Jaribio la 2 — Injini INAPASWA kuwaka na kuguruma
ikiwa
• Swichi ya PTO IMEZIMWA, NA
• Pedali ya breki imesukumwa kabisa (breki ya kuegesha
IMEWEKWA).
Jaribio la 3 — Injini inafaa KUZIMA ikiwa
• Mwendeshaji atainuka kutoka kwenye kiti wakati PTO
imewashwa, AU
• Mwendeshaji anainuka kutoka kwenye kiti huku pedali ya
breki ikiwa HAIJASUKUMWA kabisa (breki ya kuegesha
IMETOLEWA).
Jaribio la 4 — Kagua Muda ambao Visu vya Kukatia
Nyasi Vinachukua Kusimama
• Visu vya kukatia nyasi na mkanda wa kuendeshea
mashine ya kukatia nyasi zinafaa kusimama kabisa ndani
ya sekunde tano baada ya swichi ya PTO KUZIMWA.
• Ikiwa ukanda wa kuendesha mashine ya kukatia nyasi
hausimami ndani ya sekunde tano, mtembelee muuzaji
aliyeidhinishwa.
Jaribio la 5 — Ukaguzi wa Chaguo la Ukataji Nyasi
Ukirudi Nyuma (RMO)
• Injini inapaswa kuzima ikiwa utajaribu kuendesha nyuma
wakati PTO IMEWASHWA na RMO haijawezeshwa.
• Taa ya RMO inapaswa kuwaka wakati RMO
imewezeshwa.
Hatari
Kukata nyasi ukirudi nyuma kunaweza kuwa hatari kwa
waliosimama kando. Ajali za kuhuzunisha zinaweza
kutokea ikiwa mwendeshaji hayuko makini kwa kuwepo
kwa watoto. Usiwahi wezesha Chaguo ya Kukata Nyasi
Ukirudi Nyuma (RMO) ikiwa watoto wapo. Mara nyingi
watoto huvutiwa na mashine hiyo na shughuli ya ukataji
nyasi.
Injini
Kagua na Uongeze Oili ya Injini
Tumia oili Zilizoidhinishwa na Hakikisho la Briggs & Stratton
ili kupata utendakazi bora. Oili nyingine za usafishaji
zinakubalika ikiwa zimebainishwa kwa huduma ya SF, SG,
SH, SJ au ya juu zaidi. Usitumie vitegemezi maalum.
Hali joto ya nje inaamua mnato sahihi wa oili kwa injini.
Tumia chati kuchagua mnato bora zaidi kwa hali joto ya nje
inayotarajiwa.
A SAE 30 - Chini ya 40 °F (4 °C) matumizi ya SAE 30 yatasababisha
ugumu wa kuwasha.
B 10W-30 - Juu ya 80 °F (27 °C) matumizi ya 10W-30 yanaweza
kusababisha ongezeko la matumizi ya oili. Kagua kiwango cha oili
mara nyingi zaidi.
C 5W-30
D Sinthetiki 5W-30
E Vanguard™ Synthetic 15W-50
*Chini ya 40°F (4°C) matumizi ya SAE 30 yatasababisha ugumu wa kuwasha
**Zaidi ya 80°F (27°C) matumizi ya 10W-30 huenda yakasababisha matumizi
zaidi ya oili. Kagua kiwango cha oili mara nyingi zaidi.
1. Weka trekta katika eneo tambarare (Kielelezo 4).
2. Zima injini na uondoe ufunguo.
3. Safisha eneo la kujazia oili kutokana na vifusi vyovyote.
4. Ondoa kifaa cha kupima oili na ukipanguse ukitumia
kitambaa safi.
5. Ingiza kabisa kifaa cha kupima oili.
.
69