Briggs & Stratton Victa 46 23HP Manual Del Operador página 86

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 22
Soma Mwongozo
Mwongozo wa mwendeshaji una taarifa muhimu za usalama
unazohitaji kufahamu KABLA ya kuendesha kifaa chako na
vilevile WAKATI wa uendeshaji.
Mbinu salama za uendeshaji, maelezo kuhusu vipengele na
vidhibiti vya bidhaa, na taarifa ya udumishaji zimejumuishwa ili
kukusaidia kunufaika zaidi kutokana na uwekezaji wako kwenye
kifaa chako.
Hakikisha umesoma kikamilifu Sheria na Maelezo ya Usalama
yaliyo kwenye kurasa zifuatazo. Pia soma kikamilifu sehemu
ya Uendeshaji.
Watoto
Ajali za kuhuzunisha ninaweza kuwapata watoto. Usiwaruhusu
wawe mahali popote karibu na mahali kifaa kinaendeshewa.
Mara nyingi watoto huvutiwa na kifaa hicho na shughuli ya
kukata nyasi. Usiwahi dhania kwamba watoto watasalia kukaa
pale ulipowaona mara ya mwisho. Ikiwa kuna hatari kwamba
watoto wanaweza kuingia kwenye eneo linalokatwa nyasi, kuwa
na mtu mwingine mzima atakayewachunga.
USIWABEBE WATOTO KWENYE KIFAA HIKI! Hili linawahimiza
kuja karibu na kifaa wakati ujao kikiwa kinaendeshwa, na
wanaweza kujeruhiwa vibaya sana. Kisha wanaweza kukaribia
kifaa ili wabebwe wakati hautarajii, na huenda ukawakanyaga.
Kurudi Nyuma
86
Usikate nyasi ukirudi nyuma isipokuwa kama inahitajika. Daima
tazama chini na nyuma kabla na wakati unaporudi nyuma hata
kama visu vya kukatia nyasi vimezimwa.
Uendeshaji kwenye Mteremko
Unaweza kujeruhiwa vibaya sana au hata kuuliwa ukitumia kifaa
hiki kwenye mteremko mkali. Kutumia kifaa kwenye mteremko
ulio mkali sana au mahali ambapo kifaa hakishiki chuini vyema
kunaweza kukufanya upoteze udhibiti au ubingirike.
Kanuni muhimu ya kukumbukwa ni kwamba usiendeshe kwenye
mteremko wowote kwa ambao hauwezi kurudi nyuma ( katika
mfumo wa uendeshaji ukitumia magurudumu mawili). Haufai
kwendesha kwenye miteremko iliyoinuka kwa zaidi ya futi 3.5
(1,1 m) kwenye umbali wa futi 20.0 (6,0 m). daima endesha
kwenda juu na chini: si kutoka upande moja hadi mwingine.
Pia kumbuka kwamba eneo ambapo unaendeshea linaweza
kuathiri pakubwa ustawi na udhibiti. Nyasi yenye maji au njia
yenye barafu inaweza kuathiri sana uwezo wako wa kudhibiti
kifaa.
Ukihisi wasiwasi kuhusu kuendesha kifaa kwenye mteremko,
basi usiendeshe kifaa. Haina haja kujihatarisha.
Sehemu Zinazosonga
Kifaa hiki kina sehemu nyingi zinazosonga ambazo linaweza
kukujeruhi wewe au mtu mwingine. Hata hivyo, ikiwa umeketi
kwenye kiti ipasavyo, na ufuate sheria zilizo katika kitabu hiki,
kifaa hiki ni salama kuendesha.
Deki ya mashine ya kukatia nyasi ina visu vinavyozunguka
ambavyo vinaweza kukata mikono na miguu. Usimruhusu mtu
yeyote akaribie kifaa hiki wakati kinaendeshwa!
Ili kukusadia wewe, kama mwendeshaji, tumia kifaa hiki kwa
njia salama, kina mfumo wa usalama wa wakati mwendeshaji
yupo. USIJARIBU kuhitilafiana na mfumo. Mwone muuzaji wako

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido