Briggs & Stratton Victa 46 23HP Manual Del Operador página 98

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 22
2. Pindua sehemu ya ubadilishaji uzito wa awali (B, Kielelezo
15) ielekee kwenye alama ya (-) ili kupunguza uzito wa
awali, au kwenye alama ya (+) ili kuongeza uzito wa awali.
Hakikisha shoki zote zimewekwa kwenye kiwango sawa
cha uzito wa awali.
Udumishaji
Ratiba ya Udumishaji
Onyo
Spaki zinazotokea bila kusudi zinaweza kusababisha moto
au mrusho wa stima.
Uwashaji usiotarajiwa unaweza kusababisha kunaswa,
kukatwa kwa viungo kwa kiwewe, au majeraha makali ya
ukataji wa ngozi.
Kabla ya kufanya marekebisho au ukarabati:
• Tenganisha waya ya plagi ya spaki na uiweke mbali na
plagi ya spaki.
• Tenganisha betri katika kichwa hasi (negative) (injini tu
zenye kianzishi cha umeme).
• Tumia zana sahihi pekee.
• Usihitilafiane na springi ya kidhibiti, viungo, au viungo
vingine ili kuongeza kasi ya injini.
• Sehemu za kubadilishia ni lazima ziwe za aina sawia na
ziwekwe katika eneo sawia kama sehemu asilia. Sehemu
nyingine huenda zisitfanye kazi kwa njia sawia, zinaweza
kuharibu kifaa, na inaweza kusababisha majeraha.
• Usigonge gurudumu la kuongeza kasi ya injini kwa nyundo
au kifaa kigumu kwa sababu gurudumu la kuongeza kasi
ya injini linaweza kuvunjika wakati wa kuendesha.
TREKTA NA MASHINE YA KUKATIA NYASI
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
Kagua mfumo wa kiusalama wa intaloki
Safisha vifusi kwenye trekta na deki ya mashine ya kukatia nyasi
Safisha vifusi kwenye chumba cha injini
Kila Baada ya Saa 25 au Kila Mwaka *
Kagua muda wa kusimama wa visu vya mashine ya kukatia nyasi
Kagua trekta na mashine ya kukatia nyasi kama kuna sehemu zilizolegea
Kagua hewa kwenye tairi
Baada ya saa 50 au Kila Mwaka *
Kagua breki za trekta
Safisha betri na kebo
Mtembelee Muuzaji Kila Mwaka ili
Kulainisha trekta na mashine ya kukatia nyasi
Kagua visu vya mashine ya kukatia nyasi **
* Yoyote ile inayotangulia
** Kagua visu mara nyingi zaidi katika maeneo yenye udongo
wenye mchanga au yenye hali za vumbi nyingi.
98
INJINI
Saa 5 za Kwanza
Badilisha oili ya injini
Kila Baada ya Saa 8 au Kila Siku
Kagua kiwango cha oili ya injini
Kila Baada ya Saa 25 au Kila Mwaka *
Safisha chujio la hewa ya injini na kisafishaji cha awali **
Baada ya saa 50 au Kila Mwaka *
Badilisha oili ya injini
Badilisha chujio la oili
Kila Mwaka
Badilisha chujio la hewa
Badilisha kisafishaji cha mwanzo
Mtembelee Muuzaji Kila Mwaka ili
Chunguza mafla na kishika spaki
Badilisha plagi ya spaki
Badilisha chujio la mafuta
Safisha mfumo injini wa kupoesha hewa
* Yoyote ile inayotangulia
** Safisha mara nyingi zaidi katika mazingira yenye vumbi au
wakati vifusi vinavyorushwa hewani vipo.
Huduma ya Udhibiti wa Mafukizo
Udumishaji, ubadilishaji, au ukarabati wa vifaa na mifumo
ya kudhibiti mafukizo unaweza kutekelezwa na kituo
chochote au mtu yeyote wa kukarabati injini. Hata hivyo, ili
kupata huduma ya kudhibiti mafukizo ya "bila malipo", ni lazima
kazi ifanywe na mtoa huduma aliyeidhinishwa na kiwanda.
Tazama Taarifa ya Udhibiti wa Mafukizo.
Kukagua Pumzi ya Matairi
Pumzi ya matairi inafaa kukaguliwa mara kwa mara (tazama
Kielelezo 16), na kudumishwa katika viwango vilivyoonyeshwa
katika Chati ya Maelezo. Kumbuka kwamba viwango hivi vya
pumzi vinaweza kutofautiana kidogo na "Pumzi ya Juu zaidi"
iliyoonyeshwa kwenye upande wa matairi. Vipimo vya pumzi
vivilivyoonyeshwa vinakupa nguvu nzuri ya mwenendo na
kurefusha maisha ya matairi.
Kagua Muda wa Kusimama wa Visu vya
Mashine ya Kukatia Nyasi
Visu vya kukatia nyasi na mkanda wa kuendeshea mashine ya
kukatia nyasi zinafaa kusimama kabisa ndani ya sekunde tano
baada ya swichi ya umeme ya PTO kuzimwa.
Onyo
Hatari ya Uendeshaji Usio Salama
Visu vya mashine ya kukatia nyasi vikikosa kusimama kabisa
ndani ya sekunde 5, ni lazima visu visongeshwe. Usiendeshe
mashine hiyo mpaka urekebishaji mwafaka uwe umefanywa
na muuzaji aliyeidhinishwa.

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido