Briggs & Stratton Victa 46 23HP Manual Del Operador página 94

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 22
2. Weka na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A,
Kielelezo 3).
3. Ondoa kifaa cha kupima oili na ukague kiwango cha oili.
Kiwango sahihi cha oili ni kuwa juu ya alama inayoashiria
kujaa (B, Kielelezo 3) iliyo kwenye kifaa cha kupima kiwango
cha oili.
4. Iwapo kiwango cha oili kiko chini, polepole weka oili kwenye
eneo la kujazia oili ya injini (C, Kielelezo 3). Usijaze kupita
kiasi. Baada ya kuongeza oili, subiri dakika moja na kisha
ukague kiwango cha oili.
Kumbuka: Usiongeze oili kupitia eneo la kutoa oili haraka, ikiiwa
lipo. Ili kupata eneo, tazama Vipengele na Vidhibiti.
5. Weka tena na ukaze kifaa cha kupima kiwango cha oili (A,
Kielelezo 3).
Shinikizo la Oili
Ikiwa shinikizo la oili liko chini sana, swichi ya shinikizo (ikiwa
ipo) itazima injini au kuwasha kifaa cha onyo kwenye kifaa. Hili
likifanyika, zima injini na ukague kiwango cha oili ukitumia kijiti
cha kupima oili.
Ikiwa kiwango cha oili kiko chini ya alama inayoonyesha
ONGEZA (ADD), ongeza oili hadi ifike alama inayoonyesha
IMEJAA (FULL). Washa injini na ukague shinikizo linalofaa
kabla ya kuendelea kuendesha.
Ikiwa kiwango cha oili kiko kati ya alama inayoonyesha ONGEZA
(ADD) na ile inayoonyesha IMEJAA (FULL), usiwashe injini.
Wasiliana na muuzaji aliyeidhinishwa ili kurekebisha tatizo la
shinikizo la oili.
Mapendekezo ya Mafuta
Mafuta ni lazima yatimize mahitaji haya:
• Petroli safi, freshi, isiyo na lead (unleaded).
• Kiwango cha chini zaidi cha okteni 87 / 87 AKI (91 RON).
Kwa matumizi ya maeneo ya nyanda za juu, tazama hapa
chini.
• Petroli iliyo na hadi ethanoli 10% (gasohol) inakubalika.
Notisi Usitumie petroli ambayo haijaidhinishwa, kama vile
E15 na E85. Usichanganye oili kwenye petroli au kurekebisha
injini ili itumie mafuta mbadala. Utumizi wa mafuta ambayo
hayajaidhinishwa yatasababisha uharibifu wa vipengele vya
injini, jambo ambalo halitasimamiwa na hakikisho.
Ili kulinda mfumo wa mafuta kutokana na utengenezaji wa gundi,
changanya kiimarishaji mafuta ndani ya mafuta. Tazama
Uhifadhi. Mafuta yote sio sawia. Iwapo matatizo ya kuwasha
au utendakazi yatatokea, badilisha unakonunua mafuta au
ubadilishe aina. Injini hii imeidhinishwa kuendeshwa kwa
kutumia petroli. Mfumo wa kudhibiti mafukizo wa injini hii ni EM
(Engine Modifications (Marekebisho ya Injini)).
Mwinuko wa Juu
Katika mwinuko zaidi ya fiti 5,000 (mita 1,524), kiwango cha
chini cha oktani ya 85//85 AKI (89 RON) cha petroli kinakubalika.
94
Kwa injini iliyo na kabureta, marekebisho ya mwinuko wa juu
yanahitajika ili kudumisha utendakazi. Uendeshaji bila
marekebisho haya unaweza kusababisha kupunguka kwa
utendakazi, matumizi ya mafuta kuongezeka, na uchafuzi
kuongezeka. Wasiliana na Muuzaji Aliyeidhinishwa wa Briggs
& Stratton ili kupata maelezo ya marekebisho ya mwinuko wa
juu. Uendeshaji injini katika mwinuko wa chini ya futi 2,500 (mita
762) na marekebisho ya mwinuko wa juu hayapendekezwi.
Kwa injini za Uingizaji Mafuta wa Kielektroniki (EFI), hakuna
marekebisho ya mwinuko wa juu yanahitajika.
Kuongeza Mafuta
Onyo
Mafuta na mvuke wake unaweza kuwaka moto na kulipuka
kwa haraka sana.
Moto au mlipuko unaweza kusababisha majeraha mabaya
ya kuchomeka au kifo.
Wakati wa Kuongeza Mafuta
• Zima injini na uwache injini ipoe kwa angalau dakika 3
kabla ya kuondoa kifuniko cha mafuta.
• Jaza tangi la mafuta nje au katika eneo lenye hewa nyingi
safi.
• Usijaze tangi la mafuta kupita kiasi. Ili uruhusu uvukizi wa
mafuta, usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la
mafuta.
• Weka mafuta mbali na spaki, moto ulio wazi, taa za gesi,
joto, na vyanzo vingine vya mwako.
• Kagua tundu, tangi, kifuniko kama kuna nyufa na uvujaji.
Badilisha kama itahitajika.
• Mafuta yakimwagika, subiri mpaka pale ambapo
yatayeyuka kabla ya kuwasha injini.
1. Safisha kifuniko cha mafuta kutokana na uchafu na vifusi.
Ondoa kifuniko cha mafuta (A, Kielelezo 4).
2. Jaza tangi la mafuta kwa mafuta. Ili uruhusu uvukizi wa
mafuta, usijaze hadi juu ya chini ya shingo la tangi la mafuta
(B).
3. Weka upya kifuniko cha Mafuta.
Kuwasha Injini
Onyo
• Ikiwa huelewi jinsi gani haswa kidhibiti hufanya kazi, au
bado haujasoma kwa kikamilifu fungu la Vipengele na
Vidhibiti, fanya hivyo sasa hivi.
• USIJARIBU kuendesha trekta bila ya kuwa mjuzi kwanza
na eneo na utendaji wa vidhibit vyote.
1. Wakati umekaa katika kiti cha mwendeshaji, hakikisha
switchi ya PTO imezimwa na wenzo za kudhibiti kasi ya

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido