Briggs & Stratton Victa 46 23HP Manual Del Operador página 89

Tabla de contenido

Publicidad

Idiomas disponibles
  • ES

Idiomas disponibles

  • ESPAÑOL, página 22
Onyo
Hatari ya Uendeshaji Usio Salama
Usipakie kifaa hiki cha kugeukia mahali pamoja kwenye trela
au gari kubwa kwa kutumia ngazi mbili tofauti. Tumia ngazi
moja tu ambayo angalau ina mguu mmoja mpana zaidi kuliko
upana wa magurudumu ya nyuma ya kifaa hiki. Kifaa hiki
kinaweza kugeukia au kuzungukia mahali pamoja na
magurudumu ya nyuma yanaweza kuanguka kwenye ngazi,
au kifaa kinaweza kupinduka na kumjeruhi mwendeshaji au
watu waliosimama kando.
Uendeshaji kwenye Mteremko
Miteremko ni kipengele kikubwa kinachohusika na ajali
zinazotokana na kupoteza udhibiti na kupinduka, ambazo
zinaweza kupelekea jeraha mbaya au kifo. Uendeshaji katika
miteremko yote unahitaji tahadhari ya ziada. Ikiwa una wasiwasi
kwenye mteremko, usikate nyasi huko.
Udhibiti wa mashine ya kutembea nyuma au kuendesha ukiwa
juu yake kwenye mteremko hautaweza kurejeshwa kwa kuweka
breki. Sababu kuu za kupoteza udhibiti ni: matairi kukosa
kukanyaga chini vya kutosha, kasi ya juu zaidi, breki zisizotosha,
aina ya mashine haifai kwa kazi iliyopo, kukosa kufahamu
mazingira ya ardhi, ufungaji usio sahihi na usawa wa mzigo.
1. Kata nyasi kwenda juu na chini ya miteremko, sio kutoka
upande mmoja hadi mwingine.
2. Kuwa mwangalifu kutambua mashimo, matope, au matuta.
Mandhari ambayo si tambarare inaweza kufanya kifaa
kupinduka. Nyasi ndefu zinaweza kuficha vikwazo.
3. Chagua kasi ya chini ili usilazimike kusimama au kubadilisha
kasi wakati uko kwenye mteremko.
4. Usikate nyasi zilizo na majimaji au unyevunyevu. Matairi
yanaweza kupoteza nguvu ya kuvuta.
5. Daima weka kifaa kikiwa na gia haswa wakati wa kuteremka
kwenye miteremko. Usihamishie gia huru unapoteremka
kwenye mteremko.
6. Epuka kuanza, kusimama, au kugeuka ukiwa kwenye
mteremko. Matairi yakipoteza nguvu ya kukamata ardhi,
zima visu na uendelea polepole moja kwa moja kuelekea
chini ya mteremko.
7. Hakikisha kwamba mienendo yote kwenye miteremko ni
ya polepole na utaratibu. Usifanye mabadiliko ya ghafla
katika kasi au mwelekeo, ambayo yanaweza kufanya
mashine kubingirika.
8. Kuwa mwangalifu zaidi unapoendesha mashine nyenye
vifaa vya kukamata nyasi au viambatisho vingine; vinaweza
kuathiri ustawi wa kifaa. Usitumie kwenye miteremko mikali.
9. Usijaribu kustawisha mashine kwa kuweka mguu wako
ardhni (vifaa vinavyoendeshwa ukiwa juu yake).
10. Usikate nyasi karibu na sehemu zenye mishuko, mitaro, au
matuta. Mashine ya kukata nyasi inaweza kupinduka ghafla
ikiwa tairi lipo ukingoni mwa jabali au mtaro, au ikiwa ukingo
unashuka ghafla.
11. Usitumie vifaa vya kukamata nyasi katika miteremko mikali.
12. Usikate nyasi katika miteremko ambapo hauwezi kurudi
nyuma.
13. Mwone muuzaji/muuzaji rejareja wako aliyeidhinishwa ili
kupata mapendekezo ya uzito wa matairi au uzito wa vifaa
ili kuboresha ustawi.
14. Ondoa vizuizi kama vile mawe, matawi ya miti n.k.
15. Tumia kasi ya chini. Matairi yanaweza kupoteza nguvu ya
kukamata ardhi katika miteremko hata ingawa kuwa breki
zinafanyakazi vizuri.
16. Usipige kona katika miteremko isipokuwa ikiwa inahitajika,
na kisha, piga kona polepole na kwa utaratibu
unapoteremka kwenye miteremko, ikiwa inawezekana.
Onyo
Hatari ya Uendeshaji Usio Salama
Usiwahi kuendesha kwenye miteremko mikubwa inayozidi
mwinamo wa asilimia 17.6 (10°) ambapo ni mwinuko wa futi
3-1/2 (106 cm) kiwima katika futi 20 (607 cm) mlalo.
Unapoendesha katika miteremko tumia uzito wa ziada wa
matairi au uzito wa viambatanishi. Mwone muuzaji/muuzaji
rejareja wako ili kung'amua ni uzito gani unaopatikana na
unaofaa kifaa chako.
Chagua kasi ya chini ya ardhini kabla ya kuendesha kwenye
mteremko. Kwa kuongezea katika uzito wa mbele, kuwa
mwangalifu zaidi unapoendesha katika miteremko ukiwa
umeweka vifaa vya kukamata nyasi vya nyuma.
Kata nyasi ukienda JUU na CHINI kwenye mteremko, usiwahe
kata nyasi kutoka upande moja hadi mwingine, kuwa
mwangalifu unapobadilisha mielekeo na USIANZE WALA
KUSIMAMA KWENYE MTEREMKO.
Vifaa Vilivyokokotwa (Vifaa vya Kuendesha ukiwa
Juu Yake)
1. Kokota tu na mashine ambayo ina sehemu ya kuvuta
iliyoundwa ili kukokota. Usiunganishe kifaa cha kukokotwa
ispokuwa katika sehemu ya kuvutia.
2. Fuata mapendekezo ya mtengenezaji kuhusu kipimo cha
uzito wa vifaa vilivyokokotwa na kuhusu kukokota kwenye
miteremko.
3. Kamwe usiwaruhusu watoto au watu wengine kuingia ndani
au juu ya vifaa vinavyokokotwa.
89

Publicidad

Tabla de contenido
loading

Tabla de contenido